Tanzania kuwakilishwa na timu nne katika mashindano ya kimataifa

Kwa mjibu wa TFF wanasema shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limeidhibitishia Tanzania kuwa itawakilishwa na timu 4 kwenye michuano ya Caf kwa msimu wa 2019/20 ikiwa timu 2 klabu bingwa Afrika (Caf Champions League) na timu 2 kombe la shirikisho (Caf Confederation Cup)
.
.

Hiyo imekuja baada ya klabu ya Simba kufika robo fainali na kupandisha pointi za Tanzania na kuwa taifa la 12 kwenye viwango vya ubora barani Afrika. Kwa mjubu wa kanuni za ligi kuu Tanzania itawakilishwa na vilabu vya Simba na Yanga kwenye klabu bingwa Afrika huku Azam FC na KMC zikiwakilisha kombe la shirikisho.

Mtaa wa Samata… Kuzinduliwa….

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta @samagoal77 amepewa heshima ya moja ya mtaa kuitwa jina lake‬ ‪Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda amesema mtaa huo utazinduliwa kabla ya Taifa Stars kurejea kutoka kwenye mashindano ya AFCON na utakuwa katika Manispaa ya Temeke‬

#CloudsDigitalUpdates

GWAJIMA. KUONANA..NA RAISI MAGUFULI.. IKULU


Rais Magufuli amekutana na kuzungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima leo Juni 3, 2019 Ikulu jijini Dar

Askofu Gwajima aliambatana na ujumbe wake lakini pia Naibu Waziri Ofisi wa Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde alikuwepo na baada ya mazungumzo walipiga picha ya pamoja

d

Yanga… Kuleta mashine mpya

Golikipa Metacha Mnata amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga.

Metacha alianzia soka lake kwenye academy ya Azam FC baadaye akapandishwa timu ya wakubwa lakini kwa sababu hakufanikiwa kupata nafasi msimu uliopita akapelekwa kwa mkopo Mbao FC ya Mwanza.
.
Raundi ya kwanza ya msimu huu alipelekwa Tanzania Prisons lakini baadaye akarudishwa tena Mbao, tayari ameshamaliza mkataba na Azam na sasa amejiunga na timu ya wananchi.

Mashindano ya SportPesa yaliyofanyika Januari mwaka huu Metacha alifanya vizuri, kwenye mchezo wao dhidi ya Simba aliibuka mchezaji bora wa mchezo (Man of the Match).

Design a site like this with WordPress.com
Get started