

– Klabu ya Brighton inaongoza mbio za vilabu vya Uingereza kumuwania Mshambuliaji hatari wa Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta.. Kwa mujibu wa @thesunfootball.
.
– Aston Villa, Leicester, Watford na Burnley vilabu vyote vinatajwa hivi karibuni kutoa dau la Β£12m kumsajili nahodha huyo wa timu ya taifa ya Tanzania; Na Samatta, mwenye umri wa miaka 26, inaeleweka kuwa ana nia ya kuhamia England baada ya msimu bora katika Ligi Kuu ya Ubelgiji.
.
– Samatta 26; Alifunga mabao 23 na kuisaidia Genk kutwaa Ubingwa wa Ligi, huku yeye akishinda tuzo ya Shoe Ebony – tuzo itolewayo kwa mchezaji bora wa Ubelgiji anaetokea Bara la Afrika.. hapo awali imewahi kuchukuliwa na Mastaa kama Romelu Lukaku, Vincent Kompany na Michy Batshuayi.
.
– Samatta ataongoza mashambulizi akiwa Kama nahodha katika timu yake ya taifa ya Tanzania kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika baadaye mwezi huu – ni kwa mara ya kwanza Tanzania inafuzu Michuano hiyo tangu 1980; lakini baada ya mashindano hayo kumalizika, anatarajia kuondoka Genk, ambayo alijiunga nayo Januari 2016 kutoka klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, na nia yake ni kucheza Ligi Kuu ya Uingereza.
.
– Brighton imekuwa ikimfuatilia Samatta kwa muda na aliyekuwa kocha wao, Chris Hughton alikuwa shabiki mkubwa, wakati kocha mpya, Graham Potter pia anamkubali Mchezaji Hugo bora Mara Moja wa Afrika.
.
– Lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa wapinzani wenzao katika Ligi, Watford na Aston Villa na klabu za AS Roma na Lyon ya Ufaransa…
#Updates #transfers
@Sokawaytz