TAIFA STARS. YAONDOKA KWENDA MISRI….. AFCON


Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo kimeondoka nchini kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kuweka kambi maalum ya maandalizi ya michuano ya AFCON itakayofanyika nchini huo kuanzia Juni 21

Kocha wa Stars, raia wa Nigeria Emanuel Amunike amesema kuwa amechagua timu yenye vipaji ambayo ana imani italeta matokeo kwa ajili ya Taifa la Tanzania

Amesema “Vijana wengi wa Tanzania wana vipaji na ndio ambao nimewajumuisha kwenye kikosi changu, wapo ambao nimewaacha na sababu kubwa ni kushindwa kuwa na nidhamu, pia wapo wale ambao walishindwa kutimiza mazoezi na wengine hawapo fiti.”

Ameongeza kuwa “Najua kwamba kila mmoja anachaguo lake ila hamna namna ni lazima niwe na kikosi makini kitakachopambana, kwa vijana wadogo nimewajumuisha ili wapate uzoefu.”

Orodha ya waamuzi… Watakao..amua mashindano ya Afcon… 2019

WAAMUZI AFCON 2019: Hii ndiyo orodha kamili ya waamuzi 26 na waamuzi wasaidizi 30 waliothibitishwa kuchezesha michuano ya AFCON2019 inayotarajia kuanza Juni 21 hadi Julai 19 nchini Misri..Kenya, Rwanda, Burundi na Uganda wametoa isipokuwa Tanzania..
#TotalAFCON2019 @caf_online #AFCON

Ronaldo. Kutimiza hat trick. Ya 53…..

– Cristiano Ronaldo Sasa katimiza Kufunga jumla ya hat trick 53 katika maisha yake ya Soka kwa Klabu na kwa timu ya taifa kwa ujumla.
:
– Ana hat trick Saba akiitumikia timu yake ya taifa ya Ureno, katimiza idadi hiyo jana akiisambalatisha Switzerland na kuipeleka Ureno fainali ya UEFA Nations League kwa kupata ushindi wa 3-1. 🇵🇹
#NationsLeague
@Sokawaytz

Je.. De gea… Kwenda PSG…..?

@thetimes | Mabingwa wa Ufaransa klabu ya Paris St-Germain inajiandaa kumsajili mlinda lango wa Klabu ya Manchester United, David de Gea 28, ili kuwa mbadala wa Mkongwe Gianluigi Buffon, 41.
.
– Buffon hatoongezwa Mkataba mpya na Mabingwa hao na siku ya jana walithibitisha kuwa ataondoka Baada ya Mkataba wake kufikia mwisho mwezi huu, wanamuona Mhispania wa United, De Gea Kama chaguo Lao La kwanza kutua hapo Parc Des Princes..
#transfers #Updates

RAISI WA CAF… AKATWA


Rais wa Shirikisho la Soka Barani Africa(The Confederation of African Football – CAF), Ahmad Ahmad(59) amekamatwa leo jijini Paris akijiandaa kushiriki Mkutano wa FIFA

Inadaiwa kukamatwa kwake kuna uhusuano na kuvunjwa kwa mkataba baina ya CAF na Kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Ujerumani, Puma ili kuingia mkataba na Kampuni ya Technical Steel ya La Seyne-sur-Mer

Ahmed anadaiwa kusaini mkataba unainufaisha kampuni hiyo, Technical Steel huku mmoja wa Wakuu wa Kampuni hiyo akisema walimlipa Rais huyo jumla ya Euro 739,000(Tsh. 1,916,153,100) ili mkataba huo uweze kusainiwa

AMSHONA MWANAE MDOMO KWA KUTOFANYA VIZURI SHULENI

K


Mkazi mmoja Mwanamke wa Maai Mahiu mjini Naivasha, Kaunti ya Nakuru amemshona mdomo mtoto wake wa kiume anayesoma darasa la tano kwa sababu ya kushuka kimasomo

Tukio hilo la Jumamosi liliwaacha majirani midomo wazi kwa kutoamini kilichotokea huku mkazi mmoja akisema Mwanamke huyo anayefanya kazi kwenye saluni ya urembo, aliumizwa na maendeleo ya mtoto wake shuleni

Kamishna Msaidizi wa Kaunti hiyo, Julius Nyaga amesema katika kumuadhibu mwanaye, Mama alimshona mdomo mtoto wake kwa kutumia sindano kabla ya majirani kuingilia kati

Amesema Polisi wanamtafuta Mama wa mtoto huyo baada ya uongozi wa shule kuripoti kwenye mamlaka

Aidha, amewataka Wazazi kuacha kuwafanyia vitendo vya kikatili watoto na badala yake ni vyema wazazi kutafuta msaada wa kitaalamu kuwasaidia watoto kuliko kuchukua hatua kali zinazosukumwa na hasira

6 WAFARIKI….. 50 HAWAJILIKANI WALIKO NCHINI UGANDA

M

APOROMOKO YA ARDHI UGANDA: SITA WAFARIKI, 50 HAWAJULIKANI WALIPO

Nyumba zaidi ya 150, mifugo na mimea imefunikwa na matope huku shughuli za uokoaji zikiwa zinaendelea baada ya maporomoko hayo kutokea katika Wilaya ya Bududa

Vijiji viwili vya Bunamwana na Bukobero katika Kata ya Buwali kwa mara nyingine ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, vinaomboleza tena kufuatia maporomoko hayo usiku wa kuamkia leo

Msemaji wa Shirika la msalaba Mwekundu, Irene Nakasiita amesema uokoaji unaendelea lakini hakuna taarifa zaidi za uharibifu ingawa Wakazi wa eneo hilo wanasema uharibifu huo ni mkubwa

Tukio la leo linajiri mwaka mmoja baada ya mto Suume kuvunja kingo zake kufuatia mvua kubwa na kusababisha maporomoko makubwa ya ardhi yaliyopelekea vifo vya watu 40

Bududa inayopatikana karibu na mlima Elgon, Kilomita 260 kutoka Kampala, imekuwa sehemu hatari kwa makao ya watu kila msimu wa mvua, ikirekodiwa kuwa na maporomoko ya ardhi kila mwaka

Design a site like this with WordPress.com
Get started