Klabu ya simba yapanga kujitoa kagame cup


Klabu ya Simba SC imepanga kujitoa kwenye michuano ya Kagame Cup yanayotarajia kufanyika Julai 07 hadi 21 nchini Rwanda

Mkurugenzi wa klabu hiyo, Crescentus Magori amesema watapeleka barua rasmi kwenye Shirikisho la soka Tanzania kuwajulisha kutoshiriki mashindano hayo kwasababu za kiufundi

Magori amesema iwapo watashiriki mashindano hayo hawatapata muda wa kuweka kambi nje ya nchi kwa ajili ya mashindano ya Afrika Caf Champions League raundi ya awali yatakayoanza Agosti 9 mpaka na ligi kuu Tanzania Bara itakayoanza mwishoni mwa mwezi wa nane

Amedai kutokana na sababu za kubadilika kwa ratiba ya CAF, michuano ya Afcon itakayofanyika Misri itakuwa ngumu kwa klabu ya Simba kushiriki mashindano ya Kagame Cup

Simba inatarajia kwenda kuweka kambi ya mwezi mmoja nje ya nchi kujiandaa na msimu wa 2019/20

Rasmi.. Hazard… Kuitumikia. Real. Madrid

Muda uliosubiriwa hatimae umetimia; Eden Hazard amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Real Madrid akitokea Chelsea kwa dau La uhamisho wa €100 (£88m / $112m), na amekubali kusaini mkataba utakaofikia kikomo Juni 30, 2024; Real Madrid Imethibitisha kuwa Hazard atatambulishwa Rasmi Ndani ya Santiago Bernabeu siku ya Juni 13 Baada ya kumaliza Majukumu ya timu yake ya taifa..
.
– Blancos iliwatuma wawakilishi wake Jijini London mapema wiki hii kukutana na mkurugenzi wa Chelsea, Marina Granovskaia, na Hazard sasa amehamia rasmi Madrid baada ya misimu saba katika kkabu ya Chelsea; Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 hakufanya siri ya kutaka kujiunga na Real Madrid, akitoa kauli ya kusema ni ndoto kujiunga na Mabingwa hao wa Kihistoria Barani Ulaya..
.
– Hazard amekuwa mchezaji ghali namba Saba wa muda wote Duniani. Hazard kawa mchezaji ghali namba mbili kusajiliwa na Real Madrid (1⃣ Gareth Bale). Hazard kavunja rekodi ya uhamisho wa Cristiano Ronaldo akitokea @manchesterunited na Sasa kawa Sawa na Uhamisho wa Cr7 kwenda Juventus 🙌..Takwimu za Hazard akiitumikia Chelsea kwa Miaka Saba.
🏟 352 Games
⚽ 110 Goals
🎯 92 Assists

2 🏆🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Premier League
2 🏆🇪🇺 Europa League
1 🏆🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 FA Cup
1 🏆🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 League Cup

4 🏅 🔵 Chelsea Player of the Year
1 🏅🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 PL Player of the Year
👋 @hazardeden10
#Updates #transfers
@Sokawaytz

Wanandoa wauwana kutokana na ugomvi wa shamba la familia


Wakazi wa Kijiji cha Masengwa wilayani Shinyanga, Manyara Ndelema (48) na mkewe Nyamizi Mserengeti (40), wameuawa kwa kuchinjwa kwa madai ya kuwapo kwa migogoro ya mashamba ya familia

Inadaiwa Ndelema alinunua mashamba ya familia yao baada ya kuuziwa na wanafamilia ili wapate kumaliza matatizo yaliyokuwa yakiwaandama, lakini baada ya ndugu zake hao kukosa mahali pa kulima, waliibua mgogoro kuyataka mashamba hayo na kusababisha mauaji yake pamoja na mkewe

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Richard Abwao, alisema baada ya mauaji hayo, wahusika walikimbia kusikojulikana na Jeshi la Polisi lilifanya msako mkali na kuwakamata wawili na baadaye kuwakamata watuhumiwa wengine wanne juzi Nzega mkoani Tabora

Tanzania yang’ara kwenye mashindanoya miss. Landscape. Dunian


Mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Miss Landscape ya dunia, Anitha Mlay ameibuka mshindi wa pili, huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na mrembo kutoka Marekani katika fainali za mashindano zilizofanyika jana, Juni 5

Shindano hilo la urembo la kimataifa linalobeba kampeni za utunzaji mazingira, kupiga vita ujangili pamoja na kutangaza utalii limeshirikisha warembo kutoka mataifa 41

Mratibu wa mashindano hayo nchini, Happy Maina amesema lengo kuu la Kushiriki katika Miss Landscape International ni kujishirikisha katika masuala ya jamii, kama utunzaji mazingira pia kutumia fursa hii kuitangaza nchi kimataifa

China yadaiwa kufadhilia serikali ZA kidikteta. Kuwaadhibu raia

CHINA YADAIWA KUZIFADHILI SERIKALI ZA KIDIKTETA KUWADHIBITI RAIA

Wabunge nchini Marekani na Watetezi wa #HakiZaBinadamu wanaishutumu China kwa kueneza mfumo wa kiimla huku ikiziunga mkono Serikali za kidikteta zenye ukandamizaji duniani, kuwapeleleza na kuwadhibiti raia wake

Shutuma hizo zinajiri miaka 30 baada ya ukandamizaji uliyofanywa dhidi ya Waandamanaji katika eneo la uwanja wa Tiananmen Square, nchini China

Mwenyekiti wa ngazi ya juu wa Kamati ya Uhusiano wa Kimataifa katika baraza la seneti, Bob Menendez amesema ni lazima Marekani ichukue hatua madhubuti zaidi kuhakikisha haki za binadamu zinaheshimiwa

Waliotoa ushahidi wameeleza kuhusu uwekezaji mkubwa wa China katika teknolojia ya kufuatilia watu walipo, katika mawasiliano na mitandao na kuzijengea uwezo huo Serikali katika bara la Afrika, Asia, mpaka Amerika ya Kati

Aidha, Seneta wa Republikani, James Risch amesema China inatumia fursa ya uwazi katika kuendeleza demokrasia kukandamiza uhuru wa kujielezea

Raisi magufuli aeleza changamoto ZA biashara upande wa serikali. Na wafanyabiashara

RAIS MAGUFULI AELEZA CHANGAMOTO ZA BIASHARA UPANDE WA SERIKALI NA WAFANYABIASHARA

Rais Magufuli anazungumza na Wafanyabiashara watano kutoka kila Wilaya nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa ili kufahamu changamoto za Wafanyabiashara na kusikiliza mawazo yao

Rais amesema “Mpaka sasa tumeshafuta tozo zipatazo 101, kwenye kilimo, uvuvi na ufugaji, tumefuta pia baadhi ya kodi za Wachimbaji wadogo wa madini baada ya kufanya mkutano na wao”

Aidha, amebainisha kuwa nchi ina tatizo la kuwa na Taasisi nyingi za udhibiti ambazo wakati mwingine unakuta zinaingiliana kimajukumu. Taasisi hizi wakati mwingine zimekuwa kikwazo cha kuanzisha na kuendesha shughuli za biashara nchini

Lakini pia amesema “Baadhi ya Wafanyabiashara sio Waaminifu, mnakwepa kodi mnatoa rushwa, wengine mmekuwa mkifanya kazi za udalali au kujihusisha na vitendo vya ushirika wa kiuhalifu. Tumeyashuhudia hayo kwenye biashara ya sukari, mafuta ya kula na hata biashara ya korosho”

Huku akisema kuwa anataka akimaliza muda wake Tanzania iwe na Mabilionea Wafanyabiashara, amesema kuwa ana taarifa kuwa baadhi ya Wafanyabiashara wamejenga viwanda kama geresha tu, huku wakivitumia kupokelea au kutunzia bidhaa kutoka nje bila kulipa kodi stahiki

CHINA NA URUSI ZATIA SAINI KUZUIA. MATUMIZI YA FEDHA ZA MAREKANI

CHINA NA URUSI ZATIA SAINI KUZUIA MATUMIZI YA FEDHA YA MAREKANI

Rais Xi Jinping wa China ametangaza habari ya kutiwa saini mapatano ya kufutwa kwa sarafu ya dola ya Marekani katika miamala ya kibiashara ya nchi yake na Urusi

Kwa mujibu wa mapatano ya nchi hizo, dola itafutwa kabisa katika mabadilishano ya kibiashara kati yao na badala yake sarafu za mataifa hayo zitachukua nafasi ya dola katika mabadilishano

Sambamba na matamshi hayo ya Xi Jinping Serikali ya Urusi, kupitia tovuti rasmi ya Serikali ya Moscow, imetoa amri ya kuanza kutekelezwa kwa mapatano hayo ya mabadilishano ya kibiashara kwa kutumika sarafu za nchi hiyo(Ruble) na China(Yuan)

Mapatano hayo yametiwa saini katika safari ya Rais Xi Jinping mjini Moscow

Manchester United yasajili kiungo mpya …

: Klabu ya Manchester United imekubaliana na klabu ya Swansea City dau la Paundi Milioni 15 ili kumsajili Kiungo wake Mshambuliaji, Daniel James

Mchezaji huyo mwenye miaka 21, raia wa Wales amekamilisha vipimo vya Afya pale Old-Trafford kwa siku ya jana na kukubaliana mambo binafsi

Aidha, uhamisho huo unasubiri dirisha la usajili la kimataifa la FIFA kufunguliwa ifikapo Juni 11, 2019 ili uweze kukamilika

Design a site like this with WordPress.com
Get started