Kamata Ratiba ya Soka Leo

:

👉 VodacomPremierLeague
19:00 Simba SC vs Namungo FC
:
👉England – Premier League
22:45 West Ham United vs Liverpool
:
👉England – EFL Cup
22:45 Manchester City vs Manchester United
:
👉Spain – Copa del Rey
23:00 Leonesa vs Valencia
23:00 Rayo Vallecano vs Villarreal
23:00 CD Badajoz vs Granada
23:00 Real Sociedad vs Osasuna
23:00 Real Zaragoza vs Real Madrid
:
👉Italy – Coppa Italia
22:45 Inter vs Fiorentina
:
👉France – Cup
20:30 Epinal vs Lille
20:30 Pau vs Paris Saint-Germain
23:05 Marseille vs Strasbourg
:
👉Belgium – First Division A
22:30 Sporting Charleroi vs Club Brugge
:
👉Egypt – Premier League
18:00 Al Masry vs El Gounah
20:30 FC Masr vs Pyramids FC
:
👉Kenya – Premier League
15:00 Gor Mahia vs Sofapaka
15:00 Zoo FC vs Mathare United
:
👉Tunisia – Ligue I
16:00 Sportif de Chebba vs Esperance
:
Prepared by @officialchristz
#SokaplaceUPDATES
@danirito_thomson

Kamata Matokeo Ya Soka Jana

:
👉England – EFL Cup
FT Aston Villa 2 – 1 Leicester City
:
👉England – Championship
FT Blackburn Rovers 2 – 1 Queens Park Rangers
FT Brentford 0 – 1 Nottingham Forest
FT Cardiff City 2 – 1 West Bromwich Albion
FT Hull City 1 – 2 Huddersfield Town
FT Leeds United 3 – 2 Millwall
FT Luton Town 3 – 2 Derby County
FT Wigan Athletic 2 – 1 Sheffield Wednesday
FT Reading 0 – 1 Bristol City
:
👉Spain – Copa del Rey
FT Tenerife 3 – 3 Athletic Bilbao
P (2-4)
:
👉Italy – Coppa Italia
DT Milan 4 – 2 Torino
:
👉France – Cup
FT ASM Belfort 0 – 0 Montpellier
P(5-4)
FT Angers 4 – 5 Rennes
FT FC de Limonest 1 – 2 Dijon
FT Monaco 0 – 1 Saint-Etienne
:
👉Netherlands – KNVB Beker
FT Fortuna Sittard 1 – 2 Feyenoord
:
👉Egypt – Premier League
FT Wadi Degla FC 1 – 1 El Zamalek
:
👉International – Friendlies :: women
FT Thailand 1 – 1 Myanmar
FT Morocco 2 – 1 Tunisia
:
Prepared by @officialchristz
#SokaplaceUPDATES
@danirito_thomson

Togo limethibitisha kumuongeza mkataba wa miaka mitatu kocha wao mkuu Claude Le Roy raia wa Ufaransa

Shirikisho la soka nchini Togo limethibitisha kumuongeza mkataba wa miaka mitatu kocha wao mkuu Claude Le Roy raia wa Ufaransa
•
Le Roy mwenye umri wa miaka 71 kwa sasa, alianza kuinoa Togo mwaka 2016 na amepewa masharti mawili kwenye mkataba huo mpya
•
kuhakikisha timu hiyo ya taifa ya Togo”The Hawks” inafuzu kwenye michuano ya mataifa ya Afrika AFCON mwaka 2021 pia kuhakikisha timu inafuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia mwaka 2022
•
Le Roy ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa ni kocha mwenye uzoefu na soka la Afrika kwani aliwahi kufundisha timu za taifa za mataifa mbali mbali zikiwemo Ghana, Congo DR, Senegal, Cameroon na zingine kama Oman na Malaysia

#dailysporttz

klabu ya SSC Napoli imethibitisha kumsajili winga wa kimataifa wa Italia Matteo Politano

OFFICIAL: klabu ya SSC Napoli imethibitisha kumsajili winga wa kimataifa wa Italia Matteo Politano kutoka Inter Milan kwa mkopo mpaka mwaka mmoja na nusu
•
Politano alijiunga na Millan mwaka 2018 kwa mkopo akitokea Sasoulo, ameichezea Inter michezo 36 na kuweza kuifungia jumla ya goli 5
•
Napoli wamekamilisha dili hilo kwa dau la €19m huku kwenye mkataba huo kukiwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja baada ya mkataba huo kumalizika

#dailysporttz

Klabu ya Kaizer Chiefs ” Amakhosi” ya Afrika Kusini imetuma salamu za pole kwa familia

Klabu ya Kaizer Chiefs ” Amakhosi” ya Afrika Kusini imetuma salamu za pole kwa familia ya Legend wa mpira wa kikapu nchini Marekani Kobe Bryant ambaye amefariki dunia hivi karibuni kwa ajali ya ndege na mwanae Gianna ” Gigi” na watu wengine waliokuwepo kwenye ndege hiyo
•
Amakhosi wamesema ni huzuni kubwa kwa familia ya Bryant pia ulimwengu wa Basketball umepoteza mtu muhimu na ambaye alikuwa kioo cha vijana wengi wenye ndoto za kufika mbali kupitia mchezo huo

#dailysporttz

Klabu ya Rayon Sports kujenga uwanja wakimataifa

Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda iko kwenye mpango wa kutaka kujenga uwanja wa kisasa nchini humo watakao kuwa wakitumia kwenye mechi zao za michuano mbali mbali
•
Rayon leo wameweka wazi juu ya mpango wao wa kujenga uwanja huo utakao itwa “Gikundiro Stadium” huku wakisema ujenzi huo utaanza mapema mwaka huu

#dailysporttz

Eriksen kafuzu vipimo vya afya Inter Milan

Kiungo wa Tottenham Hotspurs Christian Eriksen amefuzu vipimo vya afya na sasa yupo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wake wa kutoka Tottenham kujiunga na Inter Milan.

Eriksen amefuzu vipimo vya afya baada ya kukamilisha zoezi hilo usiku wa leo, hivyo anajiandaa kusaini mkataba wa kuitumikia Inter Milan kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 17.5, utakaomuwezesha kulipwa pound 130,000 kwa wiki kabla ya kodi.

Taarifa zinaeleza kuwa staa huyo wa Denmark atasaini mkataba wa miaka minne na nusu kuitumikia Inter Milan, Eriksen aliwasili Tottenham 2013 kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 11 akitokea Ajax.

MO Dewji amkaribisha Simba SC Rais wa FIFA

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba SC MO Dewji leo amefanikiwa kukutana na Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) Gianni Infantino, MO Dewji amekutana na kujadiliana na Rais huyo, MO ame-share picha zake na Infantino katika mitandao ya kijamii.

Leo nimekutana na Gianni Infantino, Rais wa FIFA katika makao yao makuu. Kwa kweli nimefurahishwa sana, kwa dira na shauku ya kuendeleza mpira wa ushindani na wa kuvutia Afrika. Nia yao ni kuboresha maendeleo ya mpira, na najua chini ya uongozi wa Gianni mpira wa miguu kwenye bara letu utaenda next level”>>>MO Dewji

Hii sio mara ya kwanza kwa MO Dewji kutembelea timu kubwa duniani na kukutana na viongozi wa soka, aliwahi kwenda katika club ya Juventus pia lakini hajaweka wazi nini hasa amekusudia kufanya katika kukutana kwake na viongozi hao.

Design a site like this with WordPress.com
Get started