Kocha mkuu wa taifa stars Emmanuel amuneke azungumza. Kuelekea afcon..kuanza

– Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Emmanuel Amuneke amesema kuwa upande wao utajitahidi kufuzu hatua ya Mtoano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka hui 2019.. Taifa Stars imefanikiwa kufuzu kucheza mashindano haya baada ya miaka 39 na wamepangwa pamoja na Miamba wa Afrika Magharibi timu ya taifa ya Senegal, Algeria kutoka Afrika ya Kaskazini na wapinzani wenzao kutoka Afrika Mashariki, timu ya taifa ya Kenya “Harambee Stars” katika Kundi la C.
.
– Katika maandalizi ya Kuelekea Michuano hii, Tanzania Imecheza mechi mbili za Kirafiki, Mechi ya kwanza ni dhidi ya Misri wakipoteza kwa Kufungwa 1-0 na mechi ya pili ni dhidi ya Zimbabwe ikimalizika kwa Sare ya goli 1-1..
.
🗣 Amunike 🗣.. “Lengo letu kucheza mechi za kirafiki ni kujiweka fiti kiasi ambacho tunaweza Kwa bora katika Mashindano..
🗣 “Bila shaka tunacheza katika kundi gumu, lakini tutajitahidi kucheza vizuri kwa ubora wetu kufuzu raundi ya Pili..
.
– Kuhusu Kukosekana kwa Sadio Mane katika Mchezo wa kwanza wa kundi, Kocha amefunguka..
🗣 “Sidhani kwamba Senegal itakuwa dhaifu bila Mane, yeye ni mchezaji mkubwa lakini wana wachezaji wengine wengi wakubwa na wenye majina makubwa wa kuweza kushindania Mashindano”.
.
– Tanzania itaanza kampeni yao katika mashindano dhidi ya Senegal siku ya Juni 23, kisha kucheza dhidi ya Harambee Stars siku nne baadaye kabla ya mchezo wao wa mwisho wa Kindi Julai 01 dhidi ya Algeria..
#TotalAFCON2019 #AFCON2019 #zamuyetu2019🇹🇿⚽ @Sokawaytz

ISRAEL: MKE WA WAZIRI MKUU AHUKUMIWA KWA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA SERIKALI

ISRAEL: MKE WA WAZIRI MKUU AHUKUMIWA KWA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA SERIKALI

Sara Netanyahu amehukumiwa kulipa faini ya Dola za Kimarekani 15,000 sawa na Tsh. 34,582,500 leo Juni 16 baada ya kukutwa na hatia ya kutumia vibaya fedha za Serikali katika manunuzi ya chakula

Sara pamoja na Wafanyakazi wengine wa Serikalini walishtakiwa kwa kutumia vibaya Dola za Kimarekani 100,000 sawa na Tsh. 230,550,000 kununulia vyakula katika migahawa ya kifahari kati ya Mwaka 2010 hadi 2013

Hukumu hiyo inafikisha mwisho wa moja ya kesi za muda mrefu dhidi ya familia hiyo, lakini Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu bado anakabiliwa na kesi tatu za rushwa zitakazosikilizwa baadaye mwaka huu, hata hivyo yeye amekana mashtaka hayo

INDIA YAONGEZA USHURU KWA BIDHAA ZA MAREKANI

INDIA YAONGEZA USHURU KWA BIDHAA ZA MAREKANI

Wizara ya Fedha ya India imesema Serikali yake imeamua kuongeza ushuru kwa bidhaa 28 zinazoagizwa kutoka Marekani kuanzia jana, Juni 16, 2019

Juni, 2018 India ilianza kuandaa orodha ya bidhaa za Marekani zinazoweza kuongezwa ushuru ili kulipiza kisasi kutokana na Marekani kuongeza ushuru wa bidhaa za chuma na aluminium zinazoingizwa nchini humo

Hapo awali India iliahirisha muda wa kuongeza ushuru wa bidhaa hizo, ili kuhimiza mazungumzo husika na Marekani

June 5, 2019 Marekani ilitangaza kuiondoa India kutoka kwenye Mfumo wa Upendeleo GSP kwa kuwa India haitoi soko la haki na wazi kwa Marekani na hivyo kuharibu uhisiano wa kibiashara kwa nchi hizo

MTU MWENYE DALILI KAMA ZA EBOLA AONEKANA KENYA, MAMLAKA ZA AFYA ZACHUKUA TAHADHARI

MTU MWENYE DALILI KAMA ZA EBOLA AONEKANA KENYA, MAMLAKA ZA AFYA ZACHUKUA TAHADHARI

Mamlaka za Afya katika Kaunti ya Kericho zimejiweka tayari na kuchukua tahadhari baada ya Mwanamke mmoja aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola kulazwa katika hospitali ya rufaa kwenye Kaunti hiyo

Mamlaka hizo zinaeleza kuwa Mwanamke huyo aliyetoka Mabala, mpakani mwa Kenya na Uganda alipoenda kumsalimia Mume wake, baada ya kufika hospitali jana amelazwa katika chumba cha peke yake

Aidha, Idara ya Afya ya Kaunti hiyo ikishirikiana na Serikali Kuu inafuatilia kwa karibu suala hilo kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa ili kulinda usalama wa Wananchi wengine

DR CONGO MASHARIKI: ENEO LENYE UTAJIRI WA MITI INAYOZALISHA DAWA AINA YA QUININE

DR CONGO MASHARIKI: ENEO LENYE UTAJIRI WA MITI INAYOZALISHA DAWA AINA YA QUININE

Jimbo la Kivu(Kusini na Kaskazini) linafahamika kwa kuwa na hifadhi kubwa ya miti aina ya Cinchona ambayo hutumika kutengeneza dawa aina ya Quinine

Miti hiyo ililetwa na Wakoloni wa Kibelgiji waliolitawala Taifa hilo. Dawa ya Quinine hutumika kutibu Malaria, ugonjwa ambao ni tatizo kwa Mataifa ya Afrika

Licha ya uwepo wa miti hiyo lakini bado Taifa la DR Congo linatajwa kuwa na idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Malaria

Mwaka 2017 pekee, takribani watu 435,000 walifariki kutokana na ugonjwa wa Malaria

MATOKEO YA SOKA JANA JUMAPILI NA RATIBA YA HII LEO:

MATOKEO YA SOKA JANA JUMAPILI NA RATIBA YA HII LEO:
:
– Copa America – Group B.
FT Paraguay 2 – 2 Qatar
.
– Copa America – Group C.
FT Uruguay 4 – 0 Ecuador
.
– World Cup Women – Group F
FT Sweden 5 – 1 Thailand
FT USA 3 – 0 Chile
.
– CONCACAF – Gold Cup:: group B
FT Haiti 2 – 1 Bermuda
FT Costa Rica 4 – 0 Nicaragua
.
– International – Friendlies.
FT Morocco 2 – 3 Zambia
FT Nigeria 0 – 1 Senegal
FT Tanzania 1 – 1 Zimbabwe
FT Algeria 3 – 2 Mali
FT Egypt 3 – 1 Guinea
.
– Euro U-21 – Group A.
FT Poland U21 3 – 2 Belgium U21
FT Italy U21 3 – 1 Spain U21
:
RATIBA YA HII LEO JUMATATU.
– Copa America – Group C
02:00 Japan
Chile
.
– World Cup Women – Group A
22:00 Korea Republic
Norway
22:00 Nigeria
France
.
– World Cup Women – Group B
19:00 China
Spain
19:00 South Africa
Germany
.
CONCACAF – Gold Cup:: group C
02:00 Curacao
El Salvador
04:30 Jamaica
Honduras
.
International – Friendlies
21:15 Tunisia
Burundi
.
– Euro U-21 – Group B
19:30 Serbia U21
Austria U21
22:00 Germany U21
Denmark U21
#Updates #fixtures
@Sokawaytz

PATRICK GAKUMBA AMBAYE NI WAKALA WA MEDDIE KAGERE, KAFUNGUKA KUHUSU NYOTA HUYO KUTUA ZAMALEK…

– PATRICK GAKUMBA AMBAYE NI WAKALA WA MEDDIE KAGERE, KAFUNGUKA KUHUSU NYOTA HUYO KUTUA ZAMALEK… Hii leo kumeibuka taarifa kwamba @simbasctanzania imepata Tshs 1.2b kumuuza Mrwanda wao kwenda kwa miamba hao wa Misri..
:
— “Ningependa kuwatangazia Watanzania, na watu wa East Africa na Mashabiki wa mpira wa miguu na hususa ni Mashabiki wa Simba SC Wekundu wa Msimbazi, kwamba habari mlizoona kuwa Meddie Kagere “MK14” Amenunuliwa na Zamalek “SIO KWELI”… Mimi Kama agent wake Super Manager nazungumza, Walio andika hizo habari nadhani ni Wapinzani waliotaka tu kuchemsha tu vichwa vya Mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi lakini sio Kweli”
.
— Hapa nilipo nipo na Kagere tupo tunaelekea Gisenyi kidogo (Rwanda) tupo kwenye gari naendesha nipo na MK14 tunaenda kula Maisha kidogo… Kwahiyo hizo habari tunaziona Kama mnavyoziona… Simba ndio timu yenye uwezo wa kuzungumza kuhusu timu inayomtaka MK14 sio watu wa Nje, kwa Sababu bado wapo kwenye Mkataba.
.
— “Mimi ni professional Agent na Mchezaji wangu ni professional Player hatuwezi kufanya mambo ya kijinga au mambo ambayo hayaeleweki ya kuwa na tamaa ya Kusaini huku na kule… Woote walio andika hivi ni unprofessional journalists, uwezi kupost vitu ambavyo havina uhakika wala uthibitisho…
#transfers #Updates
@Sokawaytz

SAMATTA… KUELEKEA.. LAZIO. ITALI

Klabu ya SS Lazio ya Italy ipo tayari kutoa kiasi cha €16m ambacho ni sawa na bilioni 40 ili kupata saini ya nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji. .
.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwenye mtandao wa The Laziali wa nchini humo umeripoti kuwa tayari klabu hiyo imeliweka jina la Samatta kwenye orodha ya wachezaji itakaowasaka kwa namna yoyote kuhakikisha inapata saini yake. .
.
Dau hilo huenda likawa na nguvu kubwa hasa baada ya baadhi ya timu za uingereza kumhitaji Samatta kwa dau dogo ambalo ni €12m

Design a site like this with WordPress.com
Get started