MATOKEO YA SOKA JANA JUMATATU, NA RATIBA YA HII LEO. :

Copa America – Group C.
FT Japan 0 – 4 Chile
.
– World Cup Women – Group A June 17
FT Korea Republic 1 – 2 Norway
FT Nigeria 0 – 1 France
.
– World Cup Women – Group B.
FT China 0 – 0 Spain
FT South Africa 0 – 4 Germany
.
– CONCACAF – Gold Cup:: group C.
FT Curacao 0 – 1 El Salvador
FT Jamaica 3 – 2 Honduras
.
– International – Friendlies
FT Tunisia 2 – 1 Burundi
.
– Euro U-21 – Group B.
FT Serbia U21 0 – 2 Austria U21
FT Germany U21 3 – 1 Denmark U21
:
RATIBA YA HII LEO.
World Cup Women – Group C
22:00 Italy
Brazil
22:00 Jamaica
Australia
.
– CONCACAF – Gold Cup:: group D.
02:30 Panama
Trinidad & Tobago
04:30 USA
Guyana
.
– Copa America – Group A.
00:30 Bolivia
Peru
03:30 Brazil
Venezuela
.
– International – Friendlies
19:00 Benin
Mauritania
.
– Euro U-21 – Group C
19:30 Romania U21
Croatia U21
22:00 England U21
France U21
#Updates #fixtures
@Sokawaytz

RIPOTI: KIWANGO CHA SILAHA ZA NYUKLIA CHAPUNGUA DUNIANI

RIPOTI: KIWANGO CHA SILAHA ZA NYUKLIA CHAPUNGUA DUNIANI

Ripoti mpya ya Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Amani cha Stockholm(Stockholm International Peace Research Institute – SIPRI) imesema kiwango hicho kimepungua katika kipindi cha mwaka mmoja ila Mataifa yanatengeneza silaha za kisasa zaidi

Kulingana na hiyo, mwanzoni mwa mwaka 2019 Mataifa ya Marekani, Urusi, Uingereza, Ufaransa, China, India, Pakistan, Israel na Korea Kaskazini yalikuwa na shehena ya silaha 13,865 za nyuklia ikiwa ni pungufu ya silaha 800 ikilinganishwa na mwaka 2018

Hata hivyo SIPRI imesema, Mataifa yenye silaha za nyuklia yanaboresha shehena zao za silaha huku China, India na Pakistan zinaongezeka kiwango cha silaha zake za nyuklia

SIPRI imesema, mafanikio hayo yanatokana na Mataifa ya Urusi na Marekani kutimiza wajibu wake kwenye mkataba wa mwaka 2010 unaoweka kikomo cha umiliki wa silaha za nyuklia

HUAWEI KUPATA HASARA YA DOLA BILIONI 30 KWA MIAKA 2 IJAYO –

HUAWEI KUPATA HASARA YA DOLA BILIONI 30 KWA MIAKA 2 IJAYO

Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Hiawei, amesema kampuni yake itapata hasara hiyo huku akiilaumu Marekani kwa kupinga biashara yake

Ren Zhengfei amesema mauzo ya nje ya bidhaa za kampuni hiyo yameshuka kwa asilimia 40

Kampuni za Facebook na Google zimesitisha kufanya biashara ya Huawei kwa shinikizo la Serikali ya Marekani na siku mpya zinategemewa kutokuwa na uwezo wa kutumika kwa ajili ya Facebook na Google

Huawei ni kampuni ya China iliyoathirika zaidi katika vita ya kiuchumi kati ya Taifa hilo na Marekani

NIGERIA: WATU 30 WAMEFARIKI KATIKA MASHAMBULIO MATATU YA BOMU

NIGERIA: WATU 30 WAMEFARIKI KATIKA MASHAMBULIO MATATU YA BOMU

Watu wengine 40 wamejeruhiwa katika milipuko hiyo iliyotokea nje ya ukumbi huko Konduga Borno, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria

Kwa mujibu wa Wakala wa Majanga ya Dharura, katika ukumbi huo Mashabiki wa mpira walikuwa wakifuatilia mechi kupitia runinga iliyopo ukumbini

Kikundi cha Boko Haram kinashutumiwa kuhusika na mashambulio hayo japokuwa chenyewe hakijasema kuhusuka ila kinashutumiwa kutokana na kufanya mashambulio ya mara kwa mara kwenye maeneo hayo

Aidha, kutokana na mashambulio ya mara kwa mara ya kikundi hicho, hadi sasa kimeshaua zaidi ya Watu 27,000 na kulazimisha wengine zaidi ya Milioni 2 kukimbia makazi yao

WEMA SEPETU KWENDA MAHABUSU KWA SIKU 7

WEMA SEPETU KWENDA MAHABUSU KWA SIKU 7

Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar imeamuru msanii huyo kukaa mahabusu hadi Juni 24, 2019 akisubiri uamuzi wa dhamana baada ya kukiuka masharti

Juni 11, 2019 Mahakama iliamuru Wema akamatwe baada ya kushindwa kufika Mahakamani kwa mara nyingine tena huku kupitia Wakili wake akieleza kuwa aliugua ghafla

Katika shauri hilo Wema Sepetu anashtakiwa kwa kosa la kusambaza picha za ngono kwenye mitandao ya kijamii

INDIA: MFANYAMAZINGAOMBWE APOTELEA MTONI AKIJARIBU KUONESHA UJUZI WAKE

INDIA: MFANYAMAZINGAOMBWE APOTELEA MTONI AKIJARIBU KUONESHA UJUZI WAKE

Chanchal Lahiri aliyejaribu kuiga muujiza maarufu wa kutumbukizwa mtoni akiwa kichwa chini miguu juu huku amefungwa mikono na miguu anahofiwa kufariki hapo jana

Alijaribu kuiga kiini macho cha Harry Houdini, mcheza mazingaombwe maarufu duniani ambapo alitarajiwa kujinasua na kutoroka lakini hakuibuka kutoka kwenye mto huo uliopo katika jimbo la Bengal Magharibi

Watu waliokusanyika kushuhudia mazingaombwe hayo wamewaarifu Maafisa wa Polisi ambao wameeleza kwamba wanamtafuta mwanamazingaombwe huyo, maarufu Mandrake na hadi jana jioni alikuwa hajapatikana

Alifungwa kwa makufuli sita na minyororo wakati watu wakimtazama kutoka kwenye boti mbili na wengine wengi walikusanyika ufukweni katika daraja la Howrah kumuangalia

NADO ASAINI MIAKA MIWILI AZAM FC

NADO ASAINI MIAKA MIWILI AZAM FC

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imekamilisha usajili wa winga Idd Seleman ‘Nado’, kutoka Mbeya City ya Mbeya.. Nado ambaye ataanza kuitumikia timu hiyo msimu ujao, amesaini mkataba wa miaka miwili leo jioni mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ na Mratibu wa timu, Phillip Alando.
:
– Usajili wa winga huyo aliyeifungia Mbeya City mabao 10 msimu uliopita, ni sehemu ya mapendekezo ya Kocha Mkuu mpya wa Azam FC, Etienne Ndayiragije… Huo ni usajili wa kwanza mpya kwa Azam FC, ambayo kwa mujibu wa ripoti ya kocha mpya, anahitaji nyota wapya wanne tu, wawili wakiwa wazawa na wawili kutoka nje.
#transfers #azamfc

Sadio mane… Kuikosa taifa stars.. Afcon.

– Sadio Mane atakosa game ya kwanza ya Kombe La Mataifa ya Afrika wakati timu yake ya taifa ya Senegal itakapocheza dhidi ya Tanzania kutokana na kuwa na kadi mbili za Njano.
.
– Nyota huyo wa Liverpool atakosa game hiyo ambayo itapigwa ndani ya Dimba La 30 June Stadium siku ya Juni 23… Mane alipata kadi ya njano ya kwaza katika ushindi wa 1-0 wa Senegal dhidi ya Equatorial Guinea huko Malabo mnamo Novemba 17, na Kadi ya pili alipata katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Madagascar tarehe 23 Machi..
.
– Baada ya kukosekana huko, Mane atarudi katika mechi dhidi ya Algeria na Juni 27 na atamaliza kwa kucheza game ya mwisho ya kundi dhidi ya Kenya Julai 1..
#TotalAFCON2019 #AFCON2019 #Updates
@Sokawaytz

Design a site like this with WordPress.com
Get started