



#

KonaYaKiufundi Samatta Vs Licester City…
.
Part 1
.
1.Mfumo wa 3:4:3 ulionekana kuwa na tija kubwa kwake kutokana na shape inavyoonekana kwenye uhalisia, kwa maana ya kuwajumuisha washambulizi watatu kwenye eneo la juu, lakini unatakiwa kujua mfumo ni kitu kimoja na namna ya kuutimia mfumo huo ni jambo lingine, Smith alicheza mind game kwa licester, Jack Grealish na El Ghazi walicheza chini zaidi,mpango haukuwa Samata afunge, mpango ulikuwa licester wasipitie kati, wawalazimishe wapitie pembeni ambapo ni rahisi kutrap mitego yao…..
.
2. Samatta alikuwa muhimu sana kwa namna Smith alivyoicheza 3:4:3 yake, eneo la kati lilikuwa gumu mno kupitika,licester wakifika eneo lao la ubinifu wanakutana na watu sita, inakuwa changamoto kwao kupita na wakifika kwenye final third yao Villa wanakuwa 9 alafu nyuma ya mpira, hapa Samatta alitumika kuwapa presha mabeki wa licester wasifanye buildup kuanzia chini, na kwenye hilo alifanikiwa…..
.
3.Samatta wakati Villa wanashambulia, alionekana wazi kuwa na mikimbio yenye hatari mno, na hiyo kwa wasiofahamu ndio silaha kubwa ya Mbwana, kila mkimbio wake mmoja unaweza kuinufaisha timu, tatizo lilikuwa ni ugeni alionao, Grealish, Ghazi,Targett hawakumfahamu hasa anachostahili Mbwana kupewa, muda mwingi wakati Samatta anaondoka unakuta Grealish anatani anapeleka mpira anakokujua yeye, mara moja tu Grealish alifanya alichotakiwa kufanya akampa Samata pasi ambayo nusra atupie,haikuwa hivyo akastua misuli na kutolewa nje…..
.
INAENDELEA…….
.
#bakinasisi__ #njookwetu #TupoNawePaleUlipo
#

AzamUpdates โข Popat atua kwa miamba wa Soka Al Ahly
–
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, hiyo jana alitembelea makao makuu ya Al Ahly, akiwa na lengo la kujifunza mambo mbalimbali ya soka, pamoja na kujionea uwekezaji uliofanywa na klabu hiyo ya karne barani Afrika. .
–
Popat aliongozwa na mwenyeji wake, Amgad Alghoniny, ambaye ni Mhariri wa kitengo cha habari cha timu hiyo.
–
Pia Popat alipata fursa ya kukutana na Nahodha wa zamani wa Azam FC, Himid Mao ‘Ninja’, anayekipiga nchini humo katika timu ya ENPPI.
.
#bakinasisi__






#NjooKwetu
#TupoNawePaleUlipo
.
โ๏ธ Majira ya saa 1:00 usiku katika dimba la Taifa utapigwa mtanange wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Simba dhidi ya Namungo ya mkoani Lindi.
.
KOCHA NAMUNGO ANASEMAJE .
โ๏ธ Akizungumzia kuhusu pambano hilo kocha mkuu wa Namungo HITIMANA Thiery amesema anatarajia upinzani mkubwa kutoka kwa wapinzani wake (Simba Sc) na mchezo wenye ushindani na kuwa ataingia uwanjani kwa tahadhari kubwa huku wakiwa na malengo ya kupata alama tatu muhimu mbele ya SIMBA
.
NAFASI ZILIZOPO TIMU HIZI
โ๏ธ Namungo ipo nafasi ya 5 kwenye msimamo ikiwa na alama 28 baada ya kucheza michezo 16 huku Simba wao wakijimwambafai kileleni mwa msimamo (nafasi ya kwanza) na alama zao 41 baada ya kucheza mechi 16.
.
MECHI ZAO ZA MWISHO
โ๏ธ Mechi iliyopita Namungo ilishinda mabao 3-2 dhidi ya Tz Prisons Uwanja wa Samora huku Simba wao wakiigaragaza Alliance magoli 4-1 katika dimba la CCM Kirumba huko MWANZA.
.
UTABIRI WAKO ____?
.
#bakinasisi__ #NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo
.
Inaandikwa na @danirito_thomson
.
Bonge moja la game, Aston Villa waliingia na plan, walikaa nyuma ya mpira jumla ya wachezaji 9 katika nusu yao na 10 wakiwa katika nusu ya Leicester
.
Kitendo cha kumuacha Samatta juu peke yake Leicester akiwa katika nusu ya pili upande wa Leicester, inaonesha kocha ametambua uwezo wake kwenye kuhold mpira baada ya kupokea long balls za kuanzisha counter attack
.
Hii ikamlipa, lile goli la kwanza, kwenye NBA tunaita “Pass to Assist” Samatta aliweza kuhold kwa haraka na kutoa pasi iliyo sababisha Assist mpaka goli
.
Samatta alikuwa mtulivu, hakutaka kufanya movement nyingi sanaaa, hii ilimsaidia pale alipofanya mikimbio kwenye migongo ya mabeki basi ilikua mikimbio ya hatari, alifanya hivi mara mbili kipind cha kwanza ile V-Pass aliyo miss, na kipindi cha pili ile chance aliyomiss kutoka kwenye ile pinpoint cross ya Jack Grealish
.
Striker ni sawa mwindaji tu mbugani, wazungu wanasema “when you hunt, take a spot, hold your breath, aim, take a shot” yaani ukiwa unawinda, chukua nafasi, bana pumzi, lenga, piga. Yani sio kila ukiona mnyama pori unapiga tu na striker vivyo hivyo
.
Basi kuna mda Samatta akamwita Grealish akamwambia “wewe kamkabe yule Ricardo Pereira anaenda kuiomba”, we Samatta Captain wako yule ๐
.
Kipindi Samatta hana mpira, wakati Aston Villa wanapika mashambilizi toka nyuma, alikaa kwenye njia ya pasi kati kati ya Wilfred Ndidi na ukuta wake na kuzuia pasi kwenda kwa mwanae Ndidi
.
Nakamba ama Makamba, mgosi huyu aliloea tu kule kwa Mugabe Zimbabwe, pale kati alikiwasha sana mguu ule na touchez kama Fred pale United, ana hatari, alishikilia ramani ya uwanja, aliuita mpira ukaitika, aliutuma ukafika
.
Jack Grealish, The British Dinho, huyu mwamba huchukui mali mguuni, ndie anaeongoza kuchezewa fouls nyingi zaidi, anaujua mpira, nyie mpelekeeni yeye ndo nahodha ataamua, akinyang’anywa basi pigeni makofi alafu mpeni tena
.
Samatta alikuwa suprised na ile kasi ya Uingereza na ndicho kilimfanya kuisikia misuli, ndo ivo Poppa bana hawa jamaa wanafika miguuni sio poa jikaze tu kuna kina Burnley, kasi ya Uingereza ni kubwa sana, Ila Samatta naamini ni swala
.
#sokaplaceUPDATES

HATEEM BEN ARFA AMEJIUNGA NA REAL Valladolid YA HISPANIA KWA MKATABA WA MUDA MFUPI
HATEEM Amejiunga na Valladolid kama mchezaji huru baada ya kuwa nje kwa muda tangu alipomalizana mkataba na RENNES
WENGI WANAMKUMBUKA huyu mwamba pale EPL katika klabu ya………………….?

Klabu ya Tottenham ya uingereza imepeleka โฌ30m kwa PSV ili kumnyakua kijana STEVEN BERGWIJN WA PSV Eindhoven Ya uholanzi ili azibe pengo LA ERIKSEN
STEVEN Alikosekana mchezo wa jipili PSV 1-1 fc Twente kwa kile kinachoaminika nyota huyo amegomea kucheza kwakua anahitaji kuonda PSV na kuhitaji kujiunga na JOSE MOURINHO
Alipoulizwa kocha wa muda wa PSV ERNEST FEBER kukosekana kwa nyota huyo alitolea ufafanuzi kuwa hawezi kumpa nafasi mchezaji ambae 100% fikra zake hazipo PSV ,ANahitaji kuwa na MTU ambae yupo tayari kujitoa kwaajili ya PSV
Kocha wa Aston villa anampanga kikosi cha Kwanza ..
Ila kitaalamu Kocha wa Aston Villa anapata mtihani baina ya *kumtumia Samatta kwa Manufaa ya kufunga ama kulinda mpango mkuu wa Mechi dhidi ya timu yenye nguvu , sharpness na speed Leicester city*
Anaamua kulinda Mpango wa maslahi makubwa ya Kikosi,
Samatta anafanikiwa kuji adjust na maslahi ya Kikosi, Anabana njia za viungo wa wapinzani, Ana press, anafukuza kuanzia wide, ana link up vyema anaingia katikati ya mabeki , anapata chances chache anapambana kutafuta Goli *ANAKOSA*
Kosa la kawaida kabisa hata Messi ,De lima, maradona na Cr7 wamekosa sana chances za namna hii.. In An overall Kocha wa aston Villa lazima atakuwa amegundua Samatta akiwa vyema kwenye *Speed, Stamina , Sharpness, Epl Power requirements na Composure improvements* Aspects ambazo zinajengeka, Samatta anaweza tengenezewa Combination bora ya kumfanya ashinde zaidi kuliko kukaba na kutafuta *half Chances* ..
Possibly Combinations ya Jack Grielish, Mo Trenzguet na Samatta inaweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga ..
ila zaidi Samatta anahitaji kuhakikisha anagundua , *ili uweze kukimbia KM 12 per game in Epl lazima ukimbie atleast KM 20 mazoezini per day WITH POWER ,ILI KUWEZA KUJENGA UFALME WA MAGOLI KATIKA JIJI LA VILLA PARK*
Najua amegundua anapaswa kusalimia Gym ya club, Anapaswa kutafuta Nutritionist wa kumpambania usahihi wa Lishe , na anapaswa kuanza kuDamka Mazoezini kuongeza hizo Aspects nimeshauri hapo juu.. *Maombi ya wananchi zaidi ya milioni 100 Afrika Mashariki na kati yote ni Ya Neema na dua njema kwa Mbwana, Isiwe pressure iwe Hamasa na Ari kumfanya Aheshimu Muda umnyooshee ubora binafsi ndani ya epl kabla EPL haijashuhudia Ubora wa Popa Kapteni Diego* *Mwisho wa siku Klabu ya Aston Villa inatembelea Kivuli cha Mbwana Samatta* kushinda , Walibeti mkeka bora kumsajili Samatta๐๐๐ผ
Taifa limesimama kumtazama Mtanzania anayecheza Uingereza , Vitu hapa Bar vimeuzwa kwa Mkopo , Discounts na Nyongeza Juu๐..
Iwe Mwanzo kwa Mbwana na hamasa kwa wafuasi wake wote Taifa Stars Player . Credit @ommie_newtons
…
…
Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers amesema kuwa VAR haikumpa faida ya adhabu baada ya Marvelous Nakamba aliyeonekana kuunawa mpira kwenye eneo la hatari jana kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Carabao cup dhidi ya Aston Villa …..
Rodgers anadai kuwa ilikuwa penati je kwa upande wako unaona yuko sahihi ?????

Kikosi cha Azam Fc kimeanza mazoezi rasmi ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya mtibwa Sugar. Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tarehe 30/1/2020.
#fullsokatzupdates