

👉🏻 Ijumaa ya Wiki hii Rasmi Michuano ya Kombe La Mataifa ya Afrika “AFCON 2019” itaanza kutimua vumbi kwa jumla ya Mataifa 24 kuwania kuwa Bingwa mmoja mpya wa Afrika..
:
– KUNDI A… Kuna Wenyeji ambao ni Misri..
✍🏻 Misri hujiita “Pharaoh” 🇪🇬 wanafuzu AFCON Kwa Mara ya 24… Ni Mabingwa wa Kihistoria wakitwaa Ubingwa huu Mara Saba, licha ya kutwaa Ubingwa Pia wamepigwa fainali Mara Mbili, Wamemaliza mshindi wa tatu Mara tatu na Mshindi wa Nne Mara tatu… Tayari wametangaza Kikosi Chao cha Wachezaji 23 (Pichani)… (Kufuzu mtoano 9.5/10).
:
✍🏻 DR Congo 🇨🇩, Hawa ni Mabingwa wa Afrika Mara mbili, na Pia wameweza kushika nafasi ya tatu Mara mbili… DR Congo wamekuwa washindi wa Nne mara moja…Tayari wametangaza Kikosi Chao cha Wachezaji 23 (Pichani)… (Kufuzu Mtoano 8/10).
:
✍🏻Uganda 🇺🇬, Wanajiita The Cranes wanacheza AFCON kwa Mara ya Saba.. Historia yao hawajawahi kuwa Mabingwa zaidi ya kupoteza Fainali Mara moja, Waganda hawa Pia wamemaliza nafasi ya Nne Mara Moja… (Kufuzu Mtoano 6.5/10).
:
✍🏻 Zimbabwe 🇿🇼, Kama kocha wao Alivyosema wanaingia kwenye kundi Kama Underdog, kwani hawana historia yoyote Kama wapinzani wao walivyo licha ya kuwa na Timu Bora na Wachezaji wazoezu zaidi… Wanaingia katika AFCON yao ya Nne mwaka huu, Mara yao ya mwisho kushiriki ni 2017, 2006 na 2004; Mara zotee hizo wameishia tu hatua ya makundi.. (Kufuzu Mtoano 6/10).
:
👉🏻 Mechi ya kwanza itapigwa Juni 21,2019 kwa mujibu wa Ratiba ya CAF… Ratiba kamili mpaka mwisho wa kundi hilo La A… Games zote zitapigwa Dimba La Cairo International Stadium isipokuwa mechi ya mwisho ya Kundi hili itapigwa 30 June Stadium..
📅 Juni 21,2019; Misri v Zimbabwe
📅 Juni 22,2019; DR Congo v Uganda.
📅 Juni 26,2019.
Misri v DR Congo
Uganda v Zimbabwe
📅 Juni 30,2019.
Uganda v Misri
Zimbabwe v DR Congo
#TotalAFCON2019 #AFCON2019
@sokawaytz