MATOKEO YA SOKA JANA JUMANNE NA RATIBA YA HII LEO:

MATOKEO YA SOKA JANA JUMANNE NA RATIBA YA HII LEO:
:
– Copa America – Group A.
FT Bolivia 1 – 3 Peru
FT Brazil 0 – 0 Venezuela
.
– World Cup Women – Group C
FT Italy 0 – 1 Brazil
FT Jamaica 1 – 4 Australia
.
– CONCACAF – Gold Cup:: group D.
FT Panama 2 – 0 Trinidad & Tobago
37′ USA 1 – 0 Guyana
.
– International – Friendlies.
FT Benin 3 – 1 Mauritania
.
– EURO U-21 – Group C
FT Romania U21 4 – 1 Croatia U21
FT England U21 1 – 2 France U21.
:
RATIBA YA HII LEO.
Copa America – Group B.
00:30 Colombia
Qatar
03:30 Argentina
Paraguay
.
– World Cup Women – Group D.
22:00 Japan
England
22:00 Scotland
Argentina
.
– CONCACAF – Gold Cup:: group A.
03:00 Cuba
Martinique
05:30 Mexico
Canada
.
– International – Friendlies.
15:30 Zambia
Ivory Coast
18:30 South Africa
Angola
.
– EURO U-21 – Group A.
19:30 Spain U21
Belgium U21
22:00 Italy U21
Poland U21
.
– Tanzania – Nusu Fainali U20
16:00 Yanga SC U20
Azam FC U20
19:00 Simba SC U20
Mtibwa Sugar FC U20
#Updates #fixtures
@Sokawaytz

TAKUKURU INAWATAFUTA WALIOTOROKA NA FEDHA ZA KUJENGA KIWANDA CHA SARUJI

TAKUKURU INAWATAFUTA WALIOTOROKA NA FEDHA ZA KUJENGA KIWANDA CHA SARUJI

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) inawatafuta Wamiliki wa Kampuni ya Meis Industries LTD wanaodaiwa kutoroka na Tsh. Bilioni 46 kwa ajili ya kujenga kiwanda cha saruji mkoani Lindi

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema wamebaini kampuni hiyo ilikabidhiwa fedha hizo kama mkopo mwaka 2011 kutoka sehemu ya fedha za uwekezaji zilizotolewa na Libya kwa Tanzania

Amefafanua kuwa “Mwaka 2009 Serikali zote mbili zilisaini mkataba wa nyongeza ambao uliitaja Kampuni ya Meis kupewa Dola za Kimarekani 20,000,000 kwa ajili ya uwekezaji wa ujenzi wa kiwanda cha saruji eneo la Machole.”

Aidha, amewataja wahusika wa Kampuni hiyo, wanaotafutwa kuwa ni Islam Balhabou, Merey Awadh Saleh, Sabri Kuleib na Abdallah Bin Aliya na kuwataka Wananchi wenye taarifa zao kuwasiliana na TAKUKURU

RUVUMA: WATU NANE MBARONI WAKIDAIWA KUTAKA KUMTOA MTOTO KAFARA

RUVUMA: WATU NANE MBARONI

WAKIDAIWA KUTAKA KUMTOA MTOTO KAFARA

Watuhumiwa hao, Wanne kutoka Mkoani Njombe na wanne kutoka mkoani Ruvuma Wanashikiliwa na Polisi Wilayani Namtumbo kwa kufanya ramli chonganishi na kutaka kumtoa kafara mtoto mdogo

Walikamatwa katika Mlima Mgwijima wakiwa na mtoto mdogo pamoja na vifaa mbalimbali vinavyodaiwa kutumika katika kafara wakiwemo Mbuzi mmoja mweusi, kuku wawili(mmoja mweusi na mwingine mweupe)

Inadaiwa Polisi baada ya kupata taarifa za kiintelijensia walifika katika mlima huo na kuwakamata Watuhumiwa hao ikiwa ni pamoja na Mganga wa Kienyeji, lakini baada ya mahojiano wamekana madai hayo

Awali, mmoja wa Watuhumiwa, Mwanamke ambaye yupo na mtoto huyo akiwa ametokea Njombe, mara tu baada ya kufika Kituo cha Polisi ‘alipandisha mashetani’ na kuanza kujigaragaza akisema wale wengine hawana makosa ila yeye

Baadaye alipotulia na kuhojiwa alikana madai hayo na kudai kuwa yeye ni mgonjwa, hivyo alioteshwa kutoka Njombe kwenda kwenye mlima huo ili kupona. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo

JESHI LA POLISI LIMEWATAMBUA WALIOSABABISHA KIFO CHA MWANAFUNZI WA KIU

J

ESHI LA POLISI LIMEWATAMBUA WALIOSABABISHA KIFO CHA MWANAFUNZI WA KIU

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema Jeshi la Polisi tayari limewatambua wahusika

Ameliagiza Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua kali wahalifu ili liwe fundisho kwa wengine

Anifa Mgaya(21) alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali baada ya kuvamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni vibaka. Alifariki dunia baada ya kuvuja damu nyingi

Alikuwa Mwanafunzi wa Mwaka wa pili wa Stashahada katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala(KIU) tawi la Tanzania

Design a site like this with WordPress.com
Get started