
INDIA: JOTO LAZIDI KUONGEZEKA, WATU 92 WAFARIKI
–
Joto limezidi kuwa kali katika Jimbo la Bahir katika kipindi hiki ambapo India inakumbana na kipindi kidogo cha mvua katika kipindi cha takribani miongo 10 iliyopita
–
Vifo vingi huko Bahir vimerekodiwa katika maeneo ya Aurangabad, Gaya, na Nawada, ambapo joto limefikia jotoridi 45, huku watu 562 wakiwa wamelazwa na kuongeza hofu ya vifo kuongezeka
–
Mamlaka zinasema kuwa idadi kamili ya vifo haitakuja kujulikana kwa hakika kwa sababu vifo vingine vinavyotokea na kuhusishwa na joto, ndugu huzika miili kabla haijathibitishwa rasmi
–
Mamlaka zimewataka watu kukaa ndani, shule na vyuo vimefungwa, masoko yametakiwa kufunguliwa kuanzia saa kumi na moja alifajiri hadi saa kumi na moja jioni
–
Joto hilo ilimeathiri takribani mbili ya tatu ya nchi ya India, huku Jimbo la Magharibi la Rajasthan lilirekodi jotoridi 50 na Jimbo la Maharashtra lilikumbwa na ukame mkubwa kwa kipindi cha miaka 47










