TETESI ZA SOKA: POGBA AMPIGIA SIMU SARRI. DE GEA KUONGEZA MKATABA MAN UTD

TETESI ZA SOKA: POGBA AMPIGIA SIMU SARRI. DE GEA KUONGEZA MKATABA MAN UTD

Kwa mujibu gazeti la Italia la Tuttosport, Kiungo wa Manchester United, raia wa Ufaransa, Paul Pogba amempigia simu Kocha mpya wa Juventus, Maurizio Sarri kumshawishi amsajili

Mchezaji huyo aliyesajiliwa Manchester United akitokea Juventus mwaka 2016 kwa ada ya Paundi Milioni 89(Tsh. 260,583,489,549) inawezekana akaondoka United kipindi hiki cha joto baada ya kukiri kuwa anatafuta changamoto mpya

Wakati huo huo, inadaiwa kuwa Manchester United ipo tayari kumpa mkataba mnono wa miaka mitano wenye thamani ya Paundi 350,000(Tsh. 1,024,788,755) kwa wiki, Kipa wake David De Gea anayenyemelewa kwa karibu na Paris Saint-Germain

De Gea aliyepoteza nafasi ya kwanza katika kikosi cha Uhispania kwa kuwa na msimu mbovu uliopita, anadaiwa yupo tayari kusaini mkataba mpya ila anaweza kuchelewa ili kuangalia usajili utakaofanywa na United msimu huu

MZOZO WA IRAN NA MAREKANI: NDEGE ZA KIMATAIFA ZAEPUKA ANGA LA IRAN –

MZOZO WA IRAN NA MAREKANI: NDEGE ZA KIMATAIFA ZAEPUKA ANGA LA IRAN

Mashirika kadhaa ya ndege yamefuta safari zao au kuepuka anga la Iran baada ya ndege ya ujasusi ya Marekani isiokuwa na rubani kudunguliwa na Majeshi ya Ulinzi ya nchi hiyo

Mamlaka ya usafiri wa angani nchini Marekani imetoa agizo la kuzuia mashirika ya ndege ya Marekani kupaa juu ya anga la ghuba ya Uajemi na Oman

Jeshi la Iran lilidungua ndege hiyo ya kijesusi ya Marekani isiokuwa na rubani siku ya Alhamisi, likisema kuwa ndege hiyo ilikiua sheria ya anga lake na hatua hiyo imetuma ujumbe maalum kwa Marekani

Hata hivyo Marekani inasisitiza kuwa ndege hiyo ilikua ikipaa juu ya maji ya Kimataifa kabla kudungulia na kulaani hatua hiyo ikisema ni shambulizi la kichokozi lililofanywa na jeshi la IRGC

Kwa mujibu wa shirika la Habari la Reuters, haya ndio mashirika ya ndege yaliobadilisha njia za ya ndege zao: Cathay Pacific, Emirates, FlyDubai, British Airways, KLM, Qantas, Singapore Airlines na Lufthansa

HAWAII: NDEGE YAANGUKA YAUA WATU WOTE 9 WALIOKUWEMO NDANI

HAWAII: NDEGE YAANGUKA YAUA WATU WOTE 9 WALIOKUWEMO NDANI

Ndege hiyo ndogo yenye ‘Engine’ mbili imeanguka na kuwaka moto karibu na Uwanja wa ndege wa Dillingham huko Oahu, nje kidogo ya eneo la Mokuleia katika Kaunti ya Honolulu

Kwa mujibu wa Idara ya Usafirishaji ya Hawaii, imesema kuwa taarifa za awali zinaonesha kuwa ndege hiyo ilikuwa imebeba watu tisa na hakuna aliyenusurika katika ajali hiyo

Haijaeleweka bado kama ndege hiyo ilikuwa inapaa au kutua katika uwanja huo ambao unatumiwa pia na Jeshi la Marekani na kwa mbali ulikuwa unaonekana moshi ukitoka kwenye eneo la ajali

Alexis Sánchez amefunga Magoli Mawili katika michezo mawili ya #CopaAmerica

– Alexis Sánchez amefunga Magoli Mawili katika michezo mawili ya #CopaAmerica akiwa na Timu ya taifa ya Chile 🇨🇱 Mwaka huu 2019 ni magoli mengi zaidi ya michezo 27 aliyoicheza ndani ya Klabu yake ya Manchester United kwenye Mashindano yote msimu wa 2018/19.. #CopaAmericaUpdates

Mabingwa vinara wa Kundi C katika Michuano ya Copa America, Chile 🇨🇱 Sasa imecheza mechi Saba bila kupoteza za Copa America (W6, D1)

– Mabingwa watetezi na vinara wa Kundi C katika Michuano ya Copa America, timu ya taifa ya Chile 🇨🇱 Sasa imecheza mechi Saba bila kupoteza za Copa America (W6, D1) hivi karibuni hawajawahi kuweka rekodi hiyo… Mara ya mwisho ilikuwa 1945 (W5, D2)… Katika Kundi hili wanaongoza na watamaliza kucheza dhidi ya Uruguay..
:
– Mabingwa wa kihistoria, Uruguay 🇺🇾 wenye safu kalii ya Ushambuliaji wanafuatia nafasi ya pili wakiwa na nafasi kubwa ya kifuzu Mtoano…Uruguay watacheza na Chile kwenye vita ya kutafuta nani amalize Kinara wa Kundi..
.
– Underdog wa Kundi; Japan watacheza na Ecuador game ya mwisho; Ecuador 🇪🇨 ambao mpaka Sasa hawana pointi katika Kundi hili.. Ecuador ambao chini ya kocha wao Hernán Darío Gómez wamepoteza mechi Saba Kati ya Nane za #CopaAmerica, (W1 L2 mwaka 2001, L3 mwaka 2004, L2 mwaka 2019)… Mechi zoote hizo za mwisho zitapigwa Alfajiri Juni 25:..
#CopaAmericaUpdates #CopaAmerica
@Sokawaytz

Kocha wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameiambia klabu hiyo imuuze kiungo wake Paul Pogba

Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameiambia klabu hiyo imuuze kiungo wake Paul Pogba kwenda kwenye klabu itakayoweka dau kubwa zaidi ili kutunisha mfuko wake kwenye usajili msimu huu (Star)

Kocha wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameiambia klabu hiyo imuuze kiungo wake Paul Pogba

Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameiambia klabu hiyo imuuze kiungo wake Paul Pogba kwenda kwenye klabu itakayoweka dau kubwa zaidi ili kutunisha mfuko wake kwenye usajili msimu huu (Star)

Design a site like this with WordPress.com
Get started