AC Milan wameshinda michezo mitano kati ya sita iliyochezwa tangu Zlatan Ibrahimovic afike

AC Milan wameshinda michezo mitano kati ya sita iliyochezwa tangu Zlatan Ibrahimovic afike:
🏟 Mechi 6️⃣
✅ Ushindi 5️⃣
🤝 Sare 1️⃣
⚽ Magoli 1️⃣0️⃣
⚽ Magoli ya Kufungwa 5️⃣
:
🙌 Hapo awali Rossoneri ilipata Ushindi katika mechi sita tu kwenye michezo 17 ya msimu huu.. 😀🤔
#ACMilan #ZlatanIbrahimovic
@Harunlugoyah

#dailysporttz

Golikipa wa Kenya Harambee Ian Otieno kujiunga na klabu ya Zesco United

Golikipa wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Ian Otieno yuko kwenye hatua za mwisho za kijamii dili lake la kujiunga na klabu ya Zesco United ya Zambia

Otieno pia amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya Zanaco ya hapo hapo Zambia

Endapo dili hili litakamilika Otieno atakuwa ni mkenya wa tatu ndani ya kikosi cha Zesco kwa Sasa akiungana na wenzake Jesse Were na David Owino

#dailysporttz

YANGA YAMUITA KABWILI JUU TUHUMA DHIDI YA SIMBA


Uongozi wa klabu ya Yanga umemuita mlinda mlango wao Ramadhani Kabwili baada ya kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa @simbasctanzania kuwa walitaka kumpa rushwa apate kadi ya njano ili asicheze mchezo unaofuata dhidi ya mabingwa hao msimu uliopita.

Juzi Kabwili aliongeza na kituo kimoja cha radio hapa jijini Dar es Salaam kuwa viongozi wa Simba walimuahidi kumpa gari aina ya IST kama angepata kadi ya njano ili asiwepo kwenye mechi dhidi yao ingawa mwenyewe alikataa.

Msemaji wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli amesema hilo ni suala la jinai hivyo wamemuita mchezaji huyo ili kuwapa ushahidii ambao wataupeleka kwenye vyombo vya usalama kwa ajili ya hatua za kisheria. “Hili ni suala la jinai hivyo tumemuita Kabwili atupe ushahidi ili tupeleke kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki.

#dailysporttz

wachezaji wawili tu ambao wamepiga shots 100+, Dribbles 100+ na kutengeneza nafasi 100+ katika Ligi Kuu nchini Uholanzi

– Ni wachezaji wawili tu ambao wamepiga shots 100+, Dribbles 100+ na kutengeneza nafasi 100+ katika Ligi Kuu nchini Uholanzi, Eredivisie tangu kuanza kwa msimu uliopita:
🇲🇦 Hakim Ziyech
🇳🇱 Steven Bergwijn
:
🙌 Ni Hakim Ziyech (40) tu ametoa Assist nyingi zaidi kwenye Eredivisie tangu kuanza kwa msimu wa 2017/18 kuliko Steven Bergwijn (29)… na Bergwijn alifunga mabao 27 🙄🙄
:
Spurs new No.23. ⚪️
#Tottenham #PremierLeague
@Harunlugoyah

#dailysporttz

Kikosi cha Gor Mahia ambacho kinatarajiwa kuanza dhidi ya Sofapaka ligi kuu ya Kenya •

Kikosi cha Gor Mahia ambacho kinatarajiwa kuanza dhidi ya Sofapaka ligi kuu ya Kenya

David Mapigano (GK), Michael Apudo, Bernard Ondiek, Joash Onyango, Charles Momanyi, Ernest Wendo, Boniface Omondi, Lawrence Juma, Kennedy Otieno, Kenneth Muguna, Clifton Miheso

Akiba
Fredrick Odhiambo (GK), Geoffrey Ochieng’, Joakim Oluoch, Alfa Onyango, Samuel Onyango, Juma Balinya

#dailysporttz

BRUNO FERNANDES MBIONI KUJIUNGA NA MANCHESTER UNITED –

Mchezaji huyo wa Klabu ya Sporting Lisbon ameonekana mwenye furaha wakati akijiandaa kupanda ndege kuelekea Old Trafford kwenye Vipimo vya Afya

Sporting Lisbon imekubali kumuuza Bruno (28) kwenda Manchester United kwa ada ya Paundi Milioni 68 baada ya dau la kwanza la Paundi Milioni 46.6

Kiungo huyo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano na ‘Mashetani hao wa Manchester’ lakini bado hajakubalina nao masuala binafsi

Ameonekana kueleka England baada ya rafiki yake Carolina Deslandes kuweka picha ya wawili hao katika Mtandao wa Instagram wakiwa katika lifti na kuweka emoji ya ndege

Je, unadhani Kiungo huyo aliyefunga magoli 14 katika michezo 28 ya Klabu na Kitaifa kwa msimu huu, atakuwa Mkombozi wa United?

Rungu La FIFA latua kwa Al Masry

# .
.
✍️ Shirikisho la kandanda duniani FIFA, limeipiga marufuku klabu ya Al Masry ya Misri kutosajili katika madirisha matatu yajayo kwa kosa la kumsajili Cheick Moukoroo Raia wa Ivory Coast kinyume na sheria za usajili.
.
✍️ Taarifa kutoka Shirikisho la kandanda Misry EFA limethibitisha kupokea barua hiyo ya FIFA siku ya Jumanne ikisema “Masry imepigwa marufuku kuingia sokoni madirisha matatu yajayo kutosajili mchezaji yeyote.” Huku barua hiyo ikieleza wazi kuwa kuanzia dirisha hili adhabu hiyo imeanza kufanya kazi. Pia Shirikisho hilo (FIFA) limetoa ofa kwa klabu hiyo kukata rufaa kuhusu adhabu hiyo. .
.

✍️ Moukoroo mwenye Umri wa miaka 28, tayari alikuwa akimalizia adhabu yake kutojihusisha na kandanda kwa kosa la kukatisha mkataba pasipo makubaliano na klabu yake aliyokuwepo (Al Hilal Oubeid) ya Sudan katika dirisha kubwa la usajili 2017.
.
#bakinasisi__ #NjooKwetu
#TupoNawePaleUlipo

KIUNGO NAMBA 6 NA MAENDELEO YA SOKA:

#REPOST
.


.
Moja kati ya nafasi muhimu katika football ni ile ya kiungo, muhimu zaidi ni kiungo namba 6 maarufu kama kiungo mkabaji, tuanzie hapo
.
Kiungo mkabaji kama wengi wanavyomuita, inamaminika ni nafasi ya kufanya kazi chafu, wengine umuita “msafishaji” na kuamini sifa mama kwake ni kuwa na uwezo mkubwa wa kukaba na kulinda safu ya ulinzi katika mashambulizi ya kushtukiza
.
Nafasi hii kwa wafaransa waliipa jina “Water Carrier ” ikiaminika wako kila mahali. Klabu ya Nantes pale France ilisifika kuwazalisha viungo aina hii, France pale walitoka kina Christian Karambeu, Claude Makelele, Marcel Deschamps
.
Waswahili tunawaita “wakata umeme” labda chanzo ni mahusiano yetu na Tanesco 😂. Zidane aliwaita “Engine” kule Argentina nafasi hii wanaiita namba 5, Ureno ni “Trico”
.
Kutokana na maendeleo ya soka, Italia wanawaita “Regista”. Wakiamini kiungo kama huyo hapewi majukumu ya kukaba sana ama kuzuia, wanaamini nafasi yake ni kuchezesha timu(deep lying playermaker) mfano Jorginho Frello, Sandro Tonali, na Adre Pirlo
.
Italy wanaendelea kuamini kiungo mkabaji anabidi awe pembeni mwa kiungo huyo kama Matuidi anayekaa eneo la pembeni kwa Pjanic na Allan anachokifanya kwa Napoli, ama alichokifanya Mauricio Sarri pale Chelsea, alimchezesha Kante pembeni mwa Jorginho
.
Pale Barcelona na timu zenye ufanano wa falsafa ambayo ilitengenezwa na Johan Cruyff hususani timu ya taifa ya Uhispania kiungo ni kiunganishi wa eneo la walinzi na wachezaji wengine akitakiwa kuwa na uwezo mkubwa wa kupiga pasi zenye kuvuka mistari(pasing lanes) ama kuelekea pembeni (sideways) pia aweze kuzuia vertical passes zinazokuja eneo lake, hapa sasa Sergio Bousquet anahusika
.
Kuanzia miaka ya 2018 kumekuwa na namna nyingine ya kiungo huyu wa kati akiaminika kuwa (CDM), anakuwa anajumuika na mabeki wa kati wawili na kutengeneza jumla ya wachezaji watatu, kitaalam “third man concept”
.
Klopp tangu 2019 amekuwa muumini wa “third man concept” akimtumia Fabinho na Henderson kurudi kati ya Gomez na Van Djik ama pair yoyote ya Centre Back za Liverpool, yote hii ni kuwapa uhuru mabeki wake wa pembeni kuanzisha mashambulizi
.
RIPOTI YA SKAUTI NA @prosperbarthalomew

klabu ya Al Ittihad ya Saud Arabia imethibitisha kumsajili Wilfried Bony

OFFICIAL: klabu ya Al Ittihad ya Saud Arabia imethibitisha kumsajili mshambuliaji zamani wa vilabu vya Swansea City, Vittese, Stoke City na Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast Wilfried Bony kama mchezaji huru

Bony mwenye umri wa miaka 31 amejiunga na Ittihad akitokea klabu ya Al Arab ambayo alikuwa akiitumikia kwa mkopo akitokea Swansea City

Bony aliitumikia Al Arab kwenye jumla ya michezo 7 na kufanikiwa kuifungia goli 5

#dailysporttz

Design a site like this with WordPress.com
Get started