Klabu ya Crystal Palace imekubali dau la £45m na nyongeza ya £8 kutoka Manchester Utd ili kumuuza beki wake wa kulia Aron Wan-Bissaka

Klabu ya Crystal Palace imekubali dau la £45m na nyongeza ya £8 kutoka Manchester Utd ili kumuuza beki wake wa kulia Aron Wan-Bissaka.
.
.
Bissaka anatarajia kusafiri kwenda katika jiji la Manchester muda wowote kuanzia sasa ili kukamilisha taratibu za uhamisho huo. (The Sun)

– Mshambuliaji wa Kimataifa wa timu ya taifa ya Cameroon 🇨🇲, Joel Diederrick Tageu ameondolewa Mara Moja katika Kikosi

Mshambuliaji wa Kimataifa wa timu ya taifa ya Cameroon 🇨🇲, Joel Diederrick Tageu ameondolewa Mara Moja katika Kikosi cha timu hiyo ya taifa kilichopo kambini kujindaa na mechi zao za Makundi ya Fainali za AFCON nchini Misri kutokana na sababu za Kiafya..
.
– Jopo la Madaktari wa Timu hiyo wameweka wazi kuwa nyota huyo ana Matatizo ya Moyo hali ambayo inaweza kumfanya kupoteza maisha ikiwa ataendelea na Soka… Hivyo nafasi yake inatarajiwa kujazwa na Mchezaji mwingine muda mfupi ujao..
:
– Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaitumikia Klabu ya C.S Maritimò ya Nchini Ureno kwa mkopo akitokea Klabu ya Cruzeiro E.C ya Brazil..
#AFCONUpdates
@Sokawaytz

MBUNGE AOMBA MUONGOZO JUU YA MADAI TAIFA STARS KUKATWA POSHO

MBUNGE AOMBA MUONGOZO JUU YA MADAI TAIFA STARS KUKATWA POSHO

Mbunge wa Mbozi, Paschal Haonga(CHADEMA) ameomba muongozo Bungeni akihoji ni kwanini wachezaji wa Stars wamekatwa posho na Serikali akidai kuna tetesi kwamba walitakiwa kupewa posho ya Dola 300 kwa siku lakini Serikali imewapa Dola 70

Haonga aliomba muongozo huo leo kwa Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson akitaka apewe majibu huku akidai kwamba kuna mgomo wa kimya kimya katika timu hiyo na kuna siku wachezaji waligoma kufanya mazoezi

Dkt. Tulia amesema hawezi kujibu jambo hilo kwa sababu halijatokea ndani ya Bunge

Jana Stars ilikubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Senegal katika Michuano ya Mataifa ya Afrika(AFCON) nchini Misri

– Klabu ya Newcastle United Imethibitisha kuwa meneja wao, Rafael Benitez ataondoka klabuni

– Klabu ya Newcastle United Imethibitisha kuwa meneja wao, Rafael Benitez ataondoka klabuni hapo wakati mkataba wake utakapomalizika tarehe 30 mwezi huu wa Juni.
.
– Benitez Ameiongoza The Magpies kumaliza nafasi ya 13 katika Ligi Kuu Uingereza msimu uliopita… Mhispania Benitez, ambaye alichukua mikoba Machi 2016, Ameripotiwa kupokea ofa za vilabu vya China..
#EPLTransfersUpdates

Design a site like this with WordPress.com
Get started