

– Kocha wa zamani wa Chelsea na Leicester City, Claudio Ranieri anapewa nafasi kubwa ya kuwa mbadala wa Kocha Rafa Benitez ndani ya Klabu ya Newcastle, kwa mujibu wa @skysports.
.
– Ranieri hana timu tangu kumaliza Mkataba wake wa muda mfupi ndani ya Klabu ya AS Roma alipokaa tangu Machi 2019 mpaka Mei 2019… Mara ya mwisho ndani ya Premier league aliifundisha Fulham ambapo alitimuliwa kwa matokeo mabovu.. Alidumu na Klabu hiyo ya London tangu Novemba 2018 mpaka February 2019.. 🔜 ⚫⚪.
#EPLTransfersUpdates

#Repost @simbasctanzania Mchezaji mwingine kutoka Brazil mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya beki wa kati na kiungo mkabaji, Gerson Fraga Vieira (26) amesaini mkataba wa miaka miwili na Mabingwa wa nchi. Vieira ambaye amewahi kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 17 ya Brazil iliyokuwa na wachezaji maarufu kama Neymar, Philippe Coutinho, Casemiro na golikipa Alisson, pia alicheza timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 20 na alicheza klabu kadhaa za Brazil ikiwepo Grêmio amejiunga na klabu yetu akitokea ATK FC ya India.



















