
MFANYABIASHARA ADAIWA KUTEKWA JIJINI DAR
–
Mfanyabiashara Raphael O. Ongangi anadaiwa kutekwa siku ya Jumatatu tarehe 24 Juni, 2019 na watu wenye silaha akiwa anaelekea nyumbani kwake maeneo ya Masaki
–
Mke wake aliyejulikana kwa jina la Veronica anaelezwa kutoa taarifa Polisi na kuujulisha Ubalozi wa Kenya kuhusu tukio hilo ambalo hadi sasa sababu yake haijajulikana
–
Balozi wa Kenya nchini, Dan Kazungu amethibitisha kupokea taarifa hiyo na amesema wanashirikiana na Polisi katika kushughulikia suala hilo na kuwa watatoa taarifa kila hatua itakayofikiwa
–
Aidha, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar, Lazaro Mambosasa amesema kuwa Jeshi la Polisi linachunguza tukio hilo
–
Ongangi anayeendesha biashara za kusafirisha mizigo katika maeneo ya Dar es Salam, DRC Congo, Zambia and Rwanda, alikuwa mshauri wa karibu wa ndugu Zitto Kabwe kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015
















