.
Inaandikwa na @danirito_thomson
.
Simba iliendelea na 4-2-3-1na Namungo walicheza 4-3-3 pia 4-1-4-1
.
Namungo walicheza open football, hawakukaa nyuma kama timu nyingi zikicheza na Simba, walitupa soka zuri
.
Namungo walinza na goal kick fupi kwa beki za kati wakati mabeki wa pembeni wanarikaribia eneo la kati na kuwafanya Simba kuto kupress juu, holding midfielder anaungana na mabeki wa kati na wanatoka kwa pasi fupi ila kabla ya kuvuka nusu ya uwanja walicheza sana long balls
.
Walipiga long balls kwenye half space katikati ya Nyoni na Zimbwe nadhani wameelewa wana faida ya ganzi ya miguu ya Nyoni ambae amekuwa sio mwenye kasi sana
.
Bao la pili la Namungo, mpira mrefu ulipigwa kwenye pembe ya box katikati ya Kapombe na Wawa (half space), na ikagongwa kichwa mpira ukaangukia eneo ambalo ni uzembe ukiwa na viungo wawili wakabaji wote kutokuwepo, Shiboub na Mkude wote walikua likizo, second ball ikatua kwa Kikoti, bang what a screamer 2-2
.
Dilunga amekuwa na faida sana kimfumo, lile goli alidrible kutoka nafasi ya winga akaenda kushoot eneo la namba10, vyote si anaweza bana na anakupa katika ubora uleule ang’avu wa HD, amerudia alichofanya dhidi ya Mbao
.
Siri ya Sven kimbinu kwa wing zake mbili, Kahata anakua ndani ya box mpira ukiwa winga ya kulia, Dilunga anaingia mpira ndani ya box na kupiga low cross maji marefu muachie Kapombe, Dilunga kama mpira upo winga ya Kahata anasimama kama namba10, Kagere anakaa post ya chini tayari kwa krosi ndefu
.
Kahata kile kichwa uwa anapiga mwanangu Chicharito, pure pocher
.
Mkude aliendelea kuwa bora sana akiwa na mpira, aliachia kwa wakati sahihi
.
Rotation ya Chama na Ajibu, kama beki ama kiungo mkabaji hii sub inakupa wakati mgumu, jana walicheza vizuri sana
.
John Bocco alibadilisha sura ya timu, huyu ndie aliwapa wakati mgumu Namungo japo kwa muda mfupi
.
Simba wana tatizo kuwa sehemu sahihi wakati wa kukaba, hii si sawa
.
Kapombe alikuwa katika kiwango bora sana, anamwaga maji sana huyu kiumbe kama SIMTANK bovu
.
Goli la Kagere ni clear offside, uzembe waamuzi unawapa lawama mbaya TFF na kuna muda unaweza sema hizi Simba na Yanga zinahonga kumbe ni uzembe wao binafsi
.
#sokaplaceUPDATES