

– Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kitamkosa kiungo wake mahiri, Mudathir Yahya Abbas kwenye mchezo wa mwisho wa kundi C dhidi ya Algeria, Julai Mosi kutokana na kiungo huyo kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano.
.
– Kadi ya njano ambayo Mudathir alipata mnamo dakika ya 49 kwenye mechi ya jana dhidi ya Kenya ni ya pili kwake baada ya kupata nyingine mchezo dhidi ya Senegal jambo ambalo kikanuni linamlazimisha kutumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja unaofuata, ambao ni dhidi ya Algeria ambao @taifastars_ itakuwa inakamilisha ratiba ya Michuano ya AFCON.
#AFCONUpdates
















