Chelsea wameitahadharisha Atletico Madrid kuwa watasitisha mkopo wa mshambuliaji, Alvaro Morata

– Chelsea wameitahadharisha Atletico Madrid kuwa watasitisha mkopo wa mshambuliaji, Alvaro Morata, iwapo Atletico Madrid hawatatoa pauni milioni 50 kwa ajili ya uhamisho wa kudumu… Atletico wanamtaka Moratta awe Mchezaji wao na tayari Mhispania hiyo kaweka wazi hatorejea viunga vya Stamford bridge..
#EPLTransfersUpdates

FULL-TIME Madagascar 🇲🇬 2-0 🇳🇬 Nigeria

FULL-TIME | Kutoka Dimba la Alexandria Stadium jijini Alexandria na Al-Salam Stadium jijini CAIRO; Mechi za kuhitimisha hatua ya Makundi ya Fainali za AFCON Kundi B.
:
Madagascar 🇲🇬 2-0 🇳🇬 Nigeria
[Lalaina Nomenjanahary, Carolus Andriamahitsinoro]
:
Burundi 🇧🇮 0-2 🇬🇳 Guinea
[Mohamed Yattara 2X]
:
– Msimamo baada ya Kukamilika kwa hatua hiyo..
Q. Madagascar 🇲🇬 7pts
Q. Nigeria 🇳🇬 6pts
3. Guinea 🇬🇳 4pts
E. Burundi 🇧🇮 0pts
✍🏻 Katika Mara yao ya kwanza kabisa kwenye historia yao ya kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika, timu ya taifa ya Madagascar inafuzu 16 Kama Vinara wa Kundi B kufuatia Ushindi wao wa hii leo dhidi ya Nigeria wanafikisha pointi Saba (D1, W2, L0) .
✍🏻 Baada ya kipigo, Nigeria nao wanafuzu 16 bora wakiwa nafasi ya pili na pointi zao Sita… Guinea wanafuatia wakiwa na pointi Nne na Burundi wanaoshiriki Mara ya kwanza wanamaliza bila ushindi wowote katoka game zao tatu wakipoteza zote… 👉🏻 Well Done Madagascar 👏🏻👏🏻👏🏻
#TotalAFCON2019 #AFCONUpdates #AFCON2019

DRC: WATU 43 WAMEPOTEZA MAISHA KWENYE MAPOROMOKO YA UDONGO

DRC: WATU 43 WAMEPOTEZA MAISHA KWENYE MAPOROMOKO YA UDONGO

Watu 43 wamefariki na wengine kadhaa wajeruhiwa katika maporomoko ya ardhi yaliyotokea kwenye mgodi wa shaba huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Hapo awali taarifa zilizotolewa zilisema kuwa watu 34 ndio waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea Alhamisi na kwa sasa idadi imeongezeka na kufikia watu 43

Mgodi huo unamilikiwa na shirika la Uingereza la Kamoto Copper Company

TRUMP AKUTANA NA KIM JONG-UN, AKANYAGA ARDHI YA KOREA KASKAZINI

TRUMP AKUTANA NA KIM JONG-UN, AKANYAGA ARDHI YA KOREA KASKAZINI

Rais wa Marekani na Kiongozi wa Korea Kaskazini leo wamefanya tukio la kihistoria baada ya kukutana, kupeana mikono na Trump kuwa Rais wa kwanza wa Marekani kukanyaga ardhi ya Korea Kaskazini akiwa madarakani

Wawili hao walikutana mpakani mwa Korea Kaskazini na Kusini kabla ya mkutano na waandishi wa habari wakiwa na kiongozi wa Korea Kusini Moon Jae-in

Akizungumza na waandishi, Trump ameeleza kuwa amefurahi sana kuruhusiwa kuvuka mstari wa mpaka kati ya Korea Kaskazini na Kusini na hiyo inaonesha kuwa uhusiano kati yao na mataifa yao umekuwa mzuri sana

Kim pia ameonesha kufurahishwa na mkutano huo ambao amesema anaamini unaenda kufuta uhasama wa nyuma na kuleta wakati ujao wenye mafanikio

Rais Trump ameipongeza Korea Kaskazini kwa kutofanya majaribio ya makombora ya masafa marefu hivi karibuni ingawa amesema vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini viko pale pale licha ya ziara hiyo ya kihistoria na mazungumzo yaliyofanyika

Mshambuliaji wa Kimataifa wa DR Congo, Deo Kanda Á Mukok amewasili nchini tayari kujiunga na Klabu ya Simba SC

OFFICIAL | Mshambuliaji wa Kimataifa wa DR Congo, Deo Kanda Á Mukok amewasili nchini tayari kujiunga na Klabu ya Simba SC kwa mkopo Akitokea Miamba wa Soka kutoka Lubumbashi, DR Congo Klabu ya TP Mazembe.
.
– Mukok 29; Ambaye ni Bingwa wa Afrika Mara Moja 2010, Pia kawahi kucheza Kombe La Dunia kwa Vilabu akiwa na TP Mazembe na Raja Club Casablanca ya Morocco, anatarajia kukipiga kwa mkopo ndani ya Mabingwa wa Tanzania kuanzia msimu ujao.
.
– Mukok Alianza Rasmi kuitumikia Mazembe mwaka 2009 baada ya kutimka DC Motema Pembe, Alicheza mpaka 2013 na kwenda kufanya majaribio ndani ya Klabu ya Al Ahly ya Misri lakini dili lilifeli na kutua Raja Casablanca ya Morocco kwa Mkataba wa miaka mitatu lakini alicheza msimu mmoja na kurejea DRC katika Klabu ya AS Vita Club alicheza msimu mmoja na kutimkia AEL FC (Athilitiki Enosi Larissa) ya Ugiriki msimu mmoja nako akatimka… February mpaka Novemba 2015 hakuwa na timu Baada ya kutoka Ugiriki, kisha akatua tena TP Mazembe na kutolewa kwa mkopo January 2016 kwenda 4 De Abril FC ya Angola, Oktoba 2016 akarejea na mpaka Sasa anatua @simbasctanzania.
#TPLTransferUpdates
@sokawaytz_

Design a site like this with WordPress.com
Get started