Beki wa Klabu ya Azam FC, Agrey Moris, anatarajia kuwa nje dimba kwa muda wa miezi miwili ijayo baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti

Beki wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Agrey Moris, anatarajia kuwa nje dimba kwa muda wa miezi miwili ijayo baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti nchini Misri juzi.

Moris aliumia kwenye mchezo wa kirafiki wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Misri wakati ikijiandaa na michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) inayoendelea kutimua vumbi nchini Misri.

Kwa mujibu wa ripoti ya Daktari wa Azam FC, Dr. Mwanandi Mwankemwa, aliyewasili nchini misri kushugulikia matibabu yake inaeleza kuwa, beki huyo kisiki alikuwa na uvimbe kwenye kisahani kidogo juu ya goti (patella) na kuchanika kidogo kwa mtulinga wa pembeni wa goti lake..
#TPLUpdates

Klabu ya Simba SC Imethibitisha kumsajili kwa mkopo Mshambuliaji wa Kimataifa wa DR Congo kutoka Klabu ya TP Mazembe

CONFIRMED!! Klabu ya Simba SC Imethibitisha kumsajili kwa mkopo Mshambuliaji wa Kimataifa wa DR Congo kutoka Klabu ya TP Mazembe ya Lubumbashi, DR Congo… Deo Kanda Á Mukok mwenye umri wa miaka 29.
.
– Mukok atacheza Msimbazi kwa msimu mmoja tu Kama ilivyo Makubaliano ya Mazembe na Mabingwa hao wa Tanzania Bara… Mukok ni mmoja wa wachezaji ambao waliiwezesha TP Mazembe kushinda Ubingwa wa Afrika mwaka 2009, 2010 (aliifungia goli kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Esperance) na 2013 lakini pia akiwa ameshiriki Kombe la Dunia la Vilabu mwaka 2009, 2010, 2013..
#TPLTransferUpdates
@sokawaytz_

Mataifa ambayo tayari yamefuzu kucheza hatua ya 16 bora ya Fainali za Mataifa ya Afrika 2019:

Mataifa ambayo tayari yamefuzu kucheza hatua ya 16 bora ya Fainali za Mataifa ya Afrika 2019:
🇩🇿 Algeria
🇨🇩 DR Congo (Best loser).
🇪🇬 Egypt
🇬🇳 Guinea (Best loser).
🇨🇮 Ivory Coast
🇲🇬 Madagascar
🇲🇦 Morocco
🇳🇬 Nigeria
🇸🇳 Senegal
🇺🇬 Uganda
:
– Timu nyingine Sita kujulikana hii leo baada ya kukamilika Kwa mechi za Makundi mawili, E na F… Timu mbili vinara na timu mbili zitakazoshika nafasi ya pili kwa Makundi yote zitafuzu Moja kwa Moja. Timu mbili za nafasi ya tatu zitaenda kuwania nafasi ya 16 bora Kama best loser..
#TotalAFCON2019 #AFCONUpdates

INDIA: WATU 16 WAMEKAMATWA KWA KUMCHAPA AFISA MISITU –

INDIA: WATU 16 WAMEKAMATWA KWA KUMCHAPA AFISA MISITU

Wanaume 16 wamekamatwa baada ya umati wa watu kumpiga vibaya kwa fito Afisa mwanamke wa misitu wakati maafisa wa Polisi wakitazama katika jimbo la Kusini, Telangana

Umati huo ulioongozwa na mfuasi wa chama kikuu cha kisiasa katika jimbo hilo, ulikuwa ukilalamika kuhusu kampeni ya upandaji wa miti iliyoidhinishwa Jumapili

Afisa huyo wa misitu anapatiwa matibabu katika hospitali baada ya kujeruhiwa vibaya

Maafisa wawili wa Polisi waliokuwa katika eneo hilo wakati wa shambulio wamesimamishwa kazi kwa kushindwa kumlinda Afisa huyo

INDIA: WATU 13 WAFARIKI BAADA YA UKUTA WA MPAKA KUANGUKA –

INDIA: WATU 13 WAFARIKI BAADA YA UKUTA WA MPAKA KUANGUKA

Takriban watu 13 wamefariki na wengine 4 kujeruhiwa baada ya ukuta wa mpaka kuporomoka mjini Mumbai asubuhi ya leo kutokana na mvua kubwa kunyesha siku chache zilizopita

Baadhi ya watu wanadhaniwa kukwama chini ya vifusi vya ukuta huo na timu ya Jeshi la Maafa ya Taifa pamoja na Zimamoto na Polisi wanaendelea na operesheni ya uokoaji

Huu ni ukuta wa pili kuporomoka ambapo siku ya Jumamosi watu wasiopungua 15 walifariki baada ya ukuta kuporomoka huko Kondhwa mjini Pune, Kusini Mashariki mwa Mumbai

Mji wa Mumbai umeshuhudia mvua kubwa katika siku chache zilizopita na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi

MAREKANI: Watu 10 wamepoteza maisha katika jimbo la Texas baada ya kutokea kwa ajali ya ndege katika eneo la Addison kwenye kiwanja cha ndege

MAREKANI: Watu 10 wamepoteza maisha katika jimbo la Texas baada ya kutokea kwa ajali ya ndege katika eneo la Addison kwenye kiwanja cha ndege

Pindi ikiruka, ndege hiyo ilipoteza muelekeo na hatimaye kujibamiza na kuwaka moto na mpaka sasa mamlaka hazijatoa sababu ya ajali hiyo

Kati ya waliofariki, watu 4 ni ndugu wa familia moja

URUSI: KIONGOZI WA UPINZANI AFUNGWA JELA SIKU 10 KWA KUANDAMANA

URUSI: KIONGOZI WA UPINZANI AFUNGWA JELA SIKU 10 KWA KUANDAMANA

Mpinzani mkubwa wa Serikali ya Rais Vladimir Putin, Alexei Navalny amesomewa hukumu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki maandamano yasiyo halali mwezi uliopita

Katika maandamano hayo yaliyofanyika Juni 12, zaidi ya Watu 500 walikamatwa na kushikiliwa na Vyombo vya Usalama

Wananchi wa Urusi waliandamana kupinga kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari za kiuchunguzi, Ivan Golunov

Mwanahabari huyo alikamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya #DawaZaKulevya tuhuma ambazo zilifutwa siku 2 baadaye kwa kukosekana kwa ushahidi

Ni Mataifa Matatu tu yametoka bila ya pointi hata Moja katika AFCON ya mwaka huu…

#AFCONUpdates – Ni Mataifa Matatu tu yametoka bila ya pointi hata Moja katika AFCON ya mwaka huu… Namibia, Burundi na Tanzania; Lakini katika hizo ni Tanzania ndio Kinara wa kufungwa Magoli mengi zaidi ya Mataifa yaliyopo kushiriki Fainal za Mataifa ya Afrika nchini Misri.
#AFCON2019

Design a site like this with WordPress.com
Get started