:
👉VodacomPrimierLeague
FT Azam FC 1-1Mtibwa Sugar 👉Spain – Copa del Rey
FT Barcelona 5 – 0 Leganes
FT Mirandes 3 – 1 Sevilla
:
👉France – Cup
FT Nice 1 – 2 Lyon
:
👉International – Club Friendlies
FT Austria Wien 2 – 0 Zemplin Michalovce
FT Ull/Kisa 0 – 7 Vaalerenga
FT Altach 3 – 1 Ruzomberok
FT FC Midtjylland 0 – 1 Fredericia
FT Austria Wien 3 – 0 SC Dnipro-1
FT Wolfsberger AC 3 – 2 Jagiellonia Bialystok
FT Nashville SC 0 – 0 Elfsborg
:
👉Egypt – Premier League
FT Ismaily SC 3 – 2 El Entag El Harby
FT Al-Ittihad Al-Sakandary 1 – 1 Smouha SC
:
Prepared by @officialchristz
#SokaplaceUPDATES
@danirito_thomson
Mshambuliaji wa Barcelona Carles Perez amejiunga kwa mkopo katika klabu ya As Roma

Mshambuliaji wa Barcelona Carles Perez amejiunga kwa mkopo katika klabu ya As Roma hadi mwishoni mwa msimu huu huku kukiwa na kipengele kwenye mkataba wake kunacho wapa nafasi Roma ya kumnunua moja kwa moja kwa kiasi cha £,milioni 11
Everton wamekataa ofa ya €100m (£85m) kutoka Barcelona

– Everton wamekataa ofa ya €100m (£85m) kutoka Barcelona kwa mshambuliaji wao wa Kimataifa wa Brazil 🇧🇷, Richarlison… Everton walikataa ofa hiyo mara moja, hawakutaka kumuuza moja ya nyota wao kwani kwasasa wanaonekana kuimarisha kikosi chao.
.
– Richarlison amekuwa ni “target” ya muda mrefu ya mkurugenzi wa michezo wa Barca, Eric Abidal ambaye aliuliza uwezekano wa kupatikana kwa Mbrazil huyo wa miaka 22 majira ya joto yaliyopita… Abidal anaamini Richarlison, ambaye alisaini mkataba mpya wa miaka mitano huko Everton mnamo Disemba, anafanana kabisa mtindo wa kucheza wa Mshambuliaji wao, Luis Suarez ambaye kwasasa ni majeruhi.
.
– Richarlison alijiunga na Everton kwa pauni 40m kutoka Watford mnamo Julai 2018, na amefunga mabao 24 katika mechi 60, ikiwa ni pamoja na 10 katika michezo 27 hadi sasa msimu huu… Barca, ambayo kwa sasa ina pointi tatu nyuma ya vinara wa La Liga Real Madrid, inatafuta mshambuliaji wa kuimarisha kikosi chao baada ya Suarez kuwa nje kwa miezi Minne kufuatia upasuaji wa goti mapema Januari.. Wana Mpaka Siku ya Kesho kabla ya Dirisha kufungwa, Barca pia ilimkosa mshambuliaji wa Valencia, Rodrigo..
#Everton #FCBarcelona #TransfersNews
@Harunlugoyah
___________
Kwa mahitaji ya vifaa bora vya michezo kama Viatu, gloves, mipira na vingine wasiliana nasi @sports_lady_tz kwa namba 0657908829 Whatsapp
•
Duka letu lipo Dar es salaam Ubungo Mataa
•
Kwa Dar es salaam Unaweza kuletewa bidhaa zetu popote ulipo, pia tunatuma mikoani popote tutakufikia
•
Follow @sports_lady_tz kwa vifaa bora vya michezo Tanzania
#dailysporttz
FullTime : Azam Fc 1-1 Mtibwa Sugar

FullTime
:
Azam Fc 1-1 Mtibwa Sugar
Ismail ⚽
Djodi ⚽
:
#VPLUpdates
#SokaplaceUPDATES
Timu ya Taifa ya Wasichana U20 imeondoka leo kuelekea Uganda

Timu ya Taifa ya Wasichana U20 imeondoka leo kuelekea Uganda kwenye mchezo wa Marudiano Kufuzu kombe la Dunia
#dailysporttz



James Agyekum Kotei amejiunga na klabu ya FC Slavia-Mozyr ya Belarus

RASMI | aliyekuwa kiungo wa klabu ya Simba sc James Agyekum Kotei amejiunga na klabu ya FC Slavia-Mozyr ya Belarus akitokea Kaizer Chiefs “Amakhosi” ya Afrika Kusini
•
Kotei ambaye ni raia wa Ghana mwenye umri wa miaka 26 kwa sasa pia aliwahi kuchezea vilabu vya Al- Oruaba, na BA Star’s
•
Kotei amejiunga na FC Slavia kwa mkataba wa mwaka mmoja
________________________________
Kwa mahitaji ya vifaa bora vya michezo kama Viatu, gloves, mipira na vingine wasiliana nasi @sports_lady_tz kwa namba 0657908829 Whatsapp
•
Duka letu lipo Dar es salaam Ubungo Mataa
•
Kwa Dar es salaam Unaweza kuletewa bidhaa zetu popote ulipo, pia tunatuma mikoani popote tutakufikia
•
Follow @sports_lady_tz kwa vifaa bora vya michezo Tanzania
#dailysporttz
Kocha Simba alia na ukuta ‘biskuti’ kila shambulizi wasiwasi tupu.

Kocha Simba alia na ukuta ‘biskuti’ kila shambulizi wasiwasi tupu.
–
“ Hatuwezi kulificha hili, tumeruhusu magoli mengi katika mechi zilizopita. Kila mpira ndani ya eneo letu la 18 inakuwa ni balaa kwetu. Tumelifanyia kazi na tunaendelea kulitafutia ufumbuzi hili suala. “
Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck akielezea tatizo la safu ya ulinzi kuendelea kuruhusu mabao
Cc @sokatanzania
_______________________________
Kwa mahitaji ya vifaa bora vya michezo kama Viatu, gloves, mipira na vingine wasiliana nasi @sports_lady_tz kwa namba 0657908829 Whatsapp
•
Duka letu lipo Dar es salaam Ubungo Mataa
•
Kwa Dar es salaam Unaweza kuletewa bidhaa zetu popote ulipo, pia tunatuma mikoani popote tutakufikia
•
Follow @sports_lady_tz kwa vifaa bora vya michezo Tanzania
#dailysporttz
#sokatanzania
YANGA YAPELEKA MALALAMIKO BODI YA LIGI JUU YA ADHABU WALIZOPEWA

Uongozi wa klabu ya Yanga umepeleka malalamiko Bodi ya ligi (TPLB) juu ya faini walizopewa katika mechi zao zilizochezwa mwezi uliopita kutokana na kutoridhishwa na jinsi hatua hizo zilivyo chukuliwa dhidi yao
•
Ofisa habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli amesema kuhusu kupigwa faini ya shilingi laki tano kutokana na kuto wasilisha majina ya wachezaji katika kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons msemaji huyo amebainisha kuwa walipeleka kwa kuchelewa kwakua mechi ilihamishwa ghafla kutoka uwanja Sokoine kwenda Samora, Iringa baada ya kutokuwa tayari kuchezewa baada ya mvua kunyesha
•
Kuhusu faini ya shilingi laki mbili kwa kutoingia kwenye vyumba rasmi katika mchezo dhidi ya Simba msemaji huyo alisema walipeleka malalamiko Bodi ya ligi kuwa vyumba vyao havikuwa salama na wakaruhusiwa kuingia katika vyumba vya timu B lakini wameshangaa kuona wamepigwa faini hiyo
•
Pia kuhusu mashabiki wao kurusha chupa za maji katika mchezo huo ni kutokana na wao kupeleka malalamiko Bodi ya juu ya mambo mbalimbali ambayo wanaona wanaonewa
•
Bumbuli ameongeza kuwa wanashangaa Bodi hiyo kuzuia pesa kutoka kwa mdhamini Vodacom bila kufanya majadiliano na klabu hiyo kitu ambacho ni kinyume na kanuni ambazo wameziweka wenyewe
Sponsor @sports_lady_tz
#dailysporttz
Mambo 10 nilioyaona Simba Vs Namungo

1: LUCAS KIKOTI 🙌 What a player👏 Mtulivu, akili nyingi, kila pasi yake inasimulizi. Achana na asisti, leo Kikoti amefunga bao ambalo limekwenda kuwapa jibu Simba, kua tatizo sio Manula. TATIZO NI NIDHAMU YAO YA KUJILINDA. Period.
2: Hassan Dilunga🙌 HD katika ubora wake👏 Ameanza kuonyesha ni jinsi gani ‘mguu wake wa kupandia kitandani’ ulivyokua na shughuli nyingine hatari kwa makipa wa VPL
3: Kocha wa Namungo, Thiery Hitimana ameonyesha kua alifanya ‘research’ yake ya kutosha kuwajua Simba. Timu ikawa na watu wagumu nyuma, ikajaa watu wenye upepo mbele. Kama si kiwango kibovu cha beki wake wa kushoto, Namungo walikaribia kupata pointi 3 za kwanza dhidi ya Simba.
4: Kwa utulivu mkubwa, leo nimeiona akili ya Svan kwa Shiboub na Mkude. Anataka kuwa na ‘double pivot’ lakini anakosa sifa ya ‘box to box’ kwenye option hizo mbili. Wote ni offensive mind player. Inawagharimu sana Simba hii..Kivipi? .
.
5: Shiboub na Mkude wanakua bora kwenye build up🙌 Wanapishana vyema wanapotoka nyuma kusogea mbele. Tabu inakuja wanapopoteza mpira. Wote hawana tabia ya kupenda kukaba. Nafikiri ni wakati sasa wa kumrejesha Fraga aje azunguke nyuma ya wawili hawa. Kikoti alinufaika sana na udhaifu huu.
6: Shomari Kapombe🙌 Hana Baya. Ni kama Dilunga. Simba ina matatizo ya kimbini lakini hayajaathiri ubora wao. Yuko moto kweli kweli.👏
.
.
7: Yule Miza Kristom ni kama ruba aisee🙌 Alihakikisha Kahata na Ajib wanakosa ‘space’ kila wanapokua na mpira kwenye eneo lake. Naendelea kumfatilia zaidi
8: Yule mshika kibendera hapana aisee🙌 Sawa presha ya mchezo ilikuwa kubwa, lakini kwanini baada ya kuruhusu kua lile ni bao halali, aliendelea kusimama palepale na sio kurudi kati? Alijishtukia au?
9: Svan anahitaji kubadilika au kubadilishwa. Kwa quality ya wachezaji wa Simba, sina hakika kama kuna shabiki wa Simba anafurahia pointi 3 ngumu namna hii..Timu ina shida ya kimbinu. Hili wala halihitaji ramli.
10: Bigirimana Blaise🙌 Straika mwenye sifa za kiungo. Aliwapa tabu sana Wawa na Nyoni kwa mikimbio yake. Kama Makang’a angekua kwenye kiwango bora Namungo wangekua hatari zaidi.
Nb: Ubingwa wa jasho na damu 😀
siku 12 za Mbwana Samatta ndani ya Aston Villa..mafanikio yaliyotokea

Ni kama siku 12 zimepita, tangu filamu ya Mbwana Samatta na Aston Villa ilipoanza
Filamu tamu, fupi na ya kusisimua
.
.
Katika kipindi hiko cha siku 12, Villa wamepata ongezeko la mashabiki (Followers) zaidi ya LAKI 2 (200K) kwenye mtandao wao wa Instagram
Kutoka followers LAKI 4.4 mpaka LAKI 6.5 kwa siku 12 tu, si jambo dogo aisee!
Hii imeifanya Villa ipande nafasi 3 na kushika nafasi ya 10 katika orodha ya timu za Ligi Kuu England zenye followers wengi.
Interaction (Muingiliano) wa watu kwenye post zao umepanda kwa kasi
Awali, kabla ya ujio wa Samatta, comment nyingi zaidi kwenye post zao ilikua 150
.
.
Baada ya Samatta, Villa wameshapata comments zaidi ya ELFU MOJA kwa post moja tu
.
.
Bila shaka, kitengo cha masoko cha Aston Villa kitakua kinaumiza kichwa jinsi ya kubadili namba hizo kua hela
Wako hivyo wenzetu. Wanawaza hivyo mara zote
.
.
Man United walipogundua usajili wa Angel Di Maria, umekua gumzo sana mitandaoni (Kuliandikwa makala zaidi ya 160. Kukawepo na post zaidi ya 13,500), wakabadilisha mpango wa kuitambulisha jezi yake.
Daley Blind pia usajili wake ‘uliboost’ sana mtandao wa twitter wa United. Wastani wa asilimia 72 ya watu waliongezeka kwenye comment za United
Namba hizi ni muhimu sana. Zina maana kubwa kibiashara kwa klabu. Inavutia makampuni makubwa, inaongeza thamani ya mapato ya haki za matangano nk
Tunajua pia jinsi CR7 anavyopiga pesa kupitia Instagram. Tunajua pia alivyoongeza thamani ya Juve kwenye soka la hisa
Kwa Villa, ukiondoa Mahmoud Hassan ‘Treveguet’, Samatta anafatia kwa kuwa na followers wengi.
Amemuacha mbali sana staa wa timu na nahodha, Jack Grealish. Hii ina maana kubwa sana kwa Poppa, kibiashara
Yako makampuni makubwa yanayoingiza bidhaa zake Afrika yatanasa kwenye brand yake. Watampa tu hela
Kubwa tuendelee kumfollow @samagoal77
Tuendelee kuifollow @avfcofficial
Binafsi naamini, mabosi wa Villa kwa sasa wanachosubiri ni mabao ya Samatta tu, upande wa masoko, ujumbe wameshaupata.
Wamesajili staa mkubwa kwenye timu yao. Namba hazidanganyi🙌