
1: Ditram Nchimbi🙌 Mchezaji wa kisasa katika mwili wa winga hatari wa kizamani. Nguvu, kasi, pasi ya moto👏 Huyu ndie Nchimbi aliyempa ufalme Salim Aiyee kule Mwadui
2: Mayanga alichagua kuanza na 4-1-3-2. Ilikua plan nzuri mpaka pale Gharam Naftal alipokata upepo. Alipochoka kutembea kwenye space kati ya Tshishimbi na Haruna, mzigo ukawaelemea mabeki. Kama si uimara wa kipa wao (Makaka), Ruvu wangefungwa mabao 3 kipindi cha kwanza
3: Kipindi cha pili Mayanga akaufungua mchezo zaidi. Akaingia kwenye 4-2-2-2 ( Sadat alipokuja kusimama mbele na Fully Maganga, Kisiga akiwa mstari mmoja na Jamal Mnyate, ngoma ikageuka. Presha ikawa kubwa sana kwa Yanga
4: Zuberi Dabi🙌 Yes, Ruvu wamefungwa lakini huwezi kusahau perfomance yake bora katikati ya kiwanja. Kipindi cha pilk alikata kabisa mawasiliano ya Haruna na Balama
5: Tatizo kubwa la Yanga kuonekana inakata pumzi ni kukosa huduma ya ukabaji kwa Niyonzima na Balama. Baada ya dakika ya 60, mzigo wote wa ukabaji hubaki kwa Tshishimbi. Bahati mbaya zaidi, mida hio pia timu inakosa straika mwenye uwezo wa kuhold mpira mbele. Mpira ukienda, sekunde unarudi
6: Juma Abdul👏 Asante kaka. Ilikua ngumu kuamini kama angerejea kwenye ushindani, inakua ngumu tena kwa sasa kuamini uwezo wake kwa mechi 4 mfululizo. He is back🙌
7: Lamine Moro👏 Beki kiongozi. Nimeona mara kadhaa akiipanga safu yake ya ulinzi na kipindi cha pili akawa msaada mkubwa kwa Tshishimbi kwenye kukaba
8: Omary Kindamba (Beki namba 2) wa Ruvu🙌 Alikuwa na dakika 90 bora sana. Ili kufanikiwa kudhibiti runs za Morrrison ni lazima ufanye majukumu yako ya msingi kwenye kukaba
.
.
9: Labda kama Tariq Seif hajawa fiti vizuri, lakini bila shaka yoyote, kuna Molinga na Yikpe ndani ya Tariq mmoja. Yanga inahitaji straika mgumu, mwenye akili kucheza na aina ya mabeki wabishi kama Ruvu
10: Metacha Mnata🤔 Hajaruhusu bao lakini amekua na makosa mengi sana ambayo kuna siku yatakuja kuigharimu Yanga, wakipatikana mastraika makini. Anatakiwa kuwa makini zaidi kwenye maamuzi yake
Nb: Yope ni Sadney mrefu😀