MKE WA MTAWALA WA DUBAI AKIMBILIA UINGEREZA NA KUOMBA HIFADHI YA UKIMBIZI

MKE WA MTAWALA WA DUBAI AKIMBILIA UINGEREZA NA KUOMBA HIFADHI YA UKIMBIZI

Haya bint Hussein ambaye ni Mtoto wa aliyekuwa Mfalme wa Jordan, ametoroka nchini humo pamoja na Watoto wake wawili na kukimbilia nchini Uingereza akimtuhumu mumewe kumnyanyasa

Haya ni Mke wa Sheikh Mohammed bin Rashid al-Maktoum ambaye ni mtawala wa Dubai na Waziri Mkuu wa Muungano wa Falme za Kiarabu(UAE)

Taarifa zinaeleza kuwa Haya ametoroka kwa msaada wa Mwanadiplomasia wa Ujerumani na kwa sasa yuko kwenye jumba la kifahari huko Kensington, England

Mbali na kuomba hifadhi kama mkimbizi Haya pia amefungua kesi nchini Uingereza akiishtaki Familia ya Kifalme ya mumewe

Mgogoro kati ya Haya na Mumewe ulidhihirika hivi karibuni baada ya Haya kuweka shairi katika akaunti yake ya Instagram shairi ambalo lililomchukiza mumewe

Wachezaji wapya wa Kimataifa wa Yanga SC wanatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa tayari kwa maandalaiizi ya Wiki ya Wananchi itakayofikia kilele Julai 27…

– Wachezaji wapya wa Kimataifa wa Yanga SC wanatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa tayari kwa maandalaiizi ya Wiki ya Wananchi itakayofikia kilele Julai 27… Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla alisema wachezaji hao watawasili Julai 5 na Julai 7 watakwenda Mkoani Morogoro kambini.
:
— “Tayari tumekwisha watumia tiketi wachezaji wote na wote watawasili nchini Julai 5,” alisema Msolla.
.
– Akizungumzia maandalzi ya wiki ya Wananchi, Msolla alisema sherehe zitaanza Julai 21 ambapo mashabiki na wanachama wa Yanga watafanya kazi mbalimbali za kijamii kabla ya kilele Julai 27.
—- “Tutatembelea na kutoa misaada katika vituo vya watoto Yatima, kuchangia damu na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini,” alisema Msolla.
:
– Wachezaji Wakimataifa wa Yanga SC ni mabeki, Lamine Moro (Ghana) na Mustapha Seleman (Burundi). Washambuliaji, Sadney Ukhob (Namibia), Issa Bigirimana (Burundi), Patrick Sibomana (Rwanda), Juma Balinya (Uganda) na Kalengo Maybin (Zambia).
#TPLUpdates
#TPLTransferUpdates

Shirikisho La Soka Barani Afrika, @caf_online limetangaza Kikosi Bora cha hatua ya Makundi ya Fainali za Mataifa ya Afrika 2019..

OFFICIAL | Shirikisho La Soka Barani Afrika, @caf_online limetangaza Kikosi Bora cha hatua ya Makundi ya Fainali za Mataifa ya Afrika 2019.. Hatua ya Makundi ya Michuano hii imehitimishwa siku ya jana na Siku ya Ijumaa ya wiki hii hatua ya 16 bora itaanza kutimua vumbi..
#AFCONUpdates #TotalAFCON2019

Angel Di Maria amefikisha mechi 100 akiwa na timu ya Taifa ya Argentina. Swali : Amefunga mabao mangapi na pasi za mabao ngapi mpaka

Angel Di Maria amefikisha mechi 100 akiwa na timu ya Taifa ya Argentina. Swali : Amefunga mabao mangapi na pasi za mabao ngapi mpaka sasa? #BRAxARG #Argentina #Brazil #DaniAlves #Messi #ArgentinavsBrazil #BrazilvsArgentina #CopaAmerica2019 #CopaAmerica #DiMaria #Otamendi #Firmino #Coutinho #Aguero #VamosArgentina #alissonbecker

Aliyekuwa mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Kelvin Sabato “Kiduku” amejiunga na Gwambina Fc

#DealDone Aliyekuwa mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Kelvin Sabato “Kiduku” amejiunga na Gwambina Fc inayoshiriki Ligi daraja la kwanza Tanzania FDL kwa mkataba wa mwaka mmoja.
.
.
Nyota wengine ni Ibrahim Job kutoka Lipuli Fc pamoja Raizin Hafidh akitokea Coastal Union wote wakisaini mwaka mmoja.

MUSIBA APEWA SIKU 7 KUWASILISHA MAJIBU KUHUSU MADAI YA MEMBE

MUSIBA APEWA SIKU 7 KUWASILISHA MAJIBU KUHUSU MADAI YA MEMBE

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imempa siku 7 mmiliki, Cyprian Musiba na wachapishaji wa gazeti la Tanzanite wawe wamewasilisha majibu dhidi ya madai ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe anayetaka kulipwa Tsh bilioni 10 kwa kuchafuliwa

Uamuzi huo umetolewa leo, mbele ya Jaji Joaquine Demelo baada ya kupitia maombi ya wajibu maombi ya kutaka waongezewe muda wa kuwasilisha utetezi na majibu kinzani

Jaji Demelo amesema wajibu maombi walitakiwa kuwasilisha utetezi na majibu kinzani ndani ya siku 21 baada ya shauri kufunguliwa Desemba mwaka jana lakini hawakufanya hivyo ambapo Musiba kupitia Wakili wake Majura Magafu waliomba kuongezewa muda japo wadai walipinga maombi hayo wakitaka yasikubaliwe

KENYA: MWANAHABARI ZA MTANDAONI ALIYETUHUMIWA KUSHIRIKIANA NA AL-SHABAAB AACHIWA KWA DHAMANA –

KENYA: MWANAHABARI ZA MTANDAONI ALIYETUHUMIWA KUSHIRIKIANA NA AL-SHABAAB AACHIWA KWA DHAMANA

Robert Alai Onyango alieshtakiwa kwa makosa mawili likiwemo la kuvujisha siri kwa nia ya kuwasaidia Wanamgambo wa Al-Shabaab na kuvuruga uchunguzi wa Polisi

Alai Onyango amekana tuhuma hizo dhidi yake na kuachiwa kwa dhamana iliyohusisha kiasi cha Shilingi za Kitanzania 11,163,165

Anatuhumiwa kwa kufanya makosa hayo mnamo Juni 17, 2019 ambapo ndani ya siku hiyo inaelezwa kuwa aliweka picha ya Askari Polisi aliyefariki kupitia mtandao wa WhatsApp

Aidha, inaelezwa kuwa aliweka picha hiyo kupitia akaunti yake ya Twitter kitendo kinachoelezwa ni kuharibu Uchunguzi wa Vyombo vya Dola

Kesi hii imeahirishwa hadi Julai 16, 2019

RAIS KENYATTA AKERWA NA KAULI YA ‘JAGUAR’, AMTUMIA UJUMBE RAIS MAGUFULI

RAIS KENYATTA AKERWA NA KAULI YA ‘JAGUAR’, AMTUMIA UJUMBE RAIS MAGUFULI

Ujumbe huo wa Rais wa Kenya, umeelezea msimamo wa Serikali yake kuhusu kukerwa na matamshi ya Mbunge jimbo la Starehe, Charles Njagua Kanyi maarufu kwa jina la Jaguar

Mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki alitoa kauli iliyowalenga raia wa nje(wakiwemo Watanzania) wanaofanya biashara nchini Kenya akiwataka waondoke la si hivyo ataamuru Wananchi wawapige

Alidai kuwa wafanyabiashara kutoka nje akizitaja nchi za Tanzania na Uganda kuwa wamekuwa wakichukua fursa za biashara katika eneo lake

Kufuatia kauli hiyo, Serikali ya Kenya kwa nyakati kadhaa ilieleza kuwa kauli hiyo si msimamo wake na baadaye vyombo vya usalama vilimkamata Mbunge huyo

Aidha, ujumbe wa Rais Kenyatta umewasilishwa leo (Jumanne, Julai 02, 2019) na Balozi wa Kenya nchini, Dany Kazungu na kupokelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais Magufuli

Design a site like this with WordPress.com
Get started