

CHINA NA UINGEREZA ZAZOZANA KUHUSU MASUALA YA HONG KONG
–
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uingereza Jeremy Hunt, ameahidi kuendelea kuishinikiza China kuhusu njia za nguvu inazotumia dhidi ya waandamanaji mjini Hong Kong huku mzozo wa kidiplomasia ukiongezeka
–
Hunt amerejelea kuwa kutakuwa na athari iwapo China itakiuka makubaliano yalioafikiwa kuhusu haki mjini Hong Kong wakati Uingereza ilipoikabidhi udhibiti
–
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya China imejibu kwa kumshtumu Hunt kwa kujiingiza katika nadharia za kikoloni
–
Balozi wa China nchini Uingereza, Liu Xiaoming alizungumza na waandishi wa habari na kuitaka Uingereza kukoma kuingilia masuala ya ndani ya Hong Kong
















