

TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA UCHAGUZI JIMBO LA LISSU KUFANYIKA JULAI 31, 2019
–
Leo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo katika Jimbo la Singida Mashariki lililokuwa likishikiliwa na Tundu Lissu
–
Tundu Lissu(CHADEMA) amefutiwa Ubunge wake kwa madai ya kutohudhuria vikao vya Bunge kwa muda mrefu bila ya taarifa rasmi
–
Akitangaza kumvua Ubunge, Spika Job Ndugai alisema hatua hiyo imechukuliwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge
–
Tundu Lissu kwa sasa yuko nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu ya majeraha ya risasi baada ya kushambuliwa Septemba 7, 2017

























