Gadiel Michael alimuagiza Wakala wake, Jemedari Said kuzungumza na Viongozi wa Yanga SC (Na sio timu nyingine yoyote) kuhusu Kusaini Mkataba mpya.

✍🏻 Suala lipo wazi Sasa!!

:
– Gadiel Michael alimuagiza Wakala wake, Jemedari Said kuzungumza na Viongozi wa Yanga SC (Na sio timu nyingine yoyote) kuhusu Kusaini Mkataba mpya. Wakala alifanya hivyo kwenda kukutana na Mwenyekiti, Makamu M/kiti , Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na kuwasilisha yote anayohitaji Mchezaji ili Kusaini Mkataba mpya….. Yanga walikubali vyote ikiwa Ni pamoja na Kipengele Cha kumruhusu kwenda kufanya majaribio au Kumuuza nje ya Nchi Kama timu itajiyokeza.
:
✍🏻 Yanga walikubali vyote hivyo pamoja na kumuongeza mashahara ikiwa atakuwa na kiwango chenye muendelezo mzuri Wakati Kipindi yupo na Klabu yake.. Baada ya muhafaka Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga SC, Frank Kamugisha akasafiri kwenda Misri tayari kumsainisha lakini Aligoma kwa kile kinachodaiwa mpaka ruksa kutoka kwa meneja wake. Meneja akapigiwa simu na kumruhusu asaini bila shida… Halikutimia hilo na Yanga kuishia kuwasajili Ally Mtoni na Mlinda lango, Farouk Shikalo.. Wakasema atasaini Baada ya AFCON.
:
✍🏻 Lipo wazi Yanga Imekata tamaa na Mchezaji huyo. Pia ipo wazi kwamba Gadiel Michael kafanya Mazungumzo na Klabu ya Simba SC wakiwa tayari kabisa kumsajili. Lipo wazi Gadiel Michael kafanya Mazungumzo na Klabu ya Bidivest Wits ya Afrika Kusini walio tayari kumsainisha Mkataba….🙌 Yupo wapi Gadiel Mbaga?! Subira tu!!…
:
✍🏻 Suala la Mlinda lango Farouk Shikalo kutua Yanga SC. Ni kweli Yanga wamefikia tu makubaliano Mchezaji na Yanga walipewa ruhusa kutoka Klabu yake ya Bandari FC kufanya Mazungumzo na Mchezaji. Walifikia muhafaka kila kitu Sasa Uongozi wa Yanga unatarajia kukutana na Viongozi wa Bandari FC kukamilisha uhamisho huo, Ikumbukwe Mchezaji alikuwa na Mkataba na Timu yake ya Bandari… 🔜 ✍🏻.
@Hawaii mpya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewasili Chato Tanzania na kupokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika ziara binafsi ya siku mbili. 📸ikulu

R

rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewasili Chato Tanzania na kupokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika ziara binafsi ya siku mbili.
📸ikulu

MATOKEO YA SOKA JANA IJUMAA NA RATIBA YA HII LEO.

MATOKEO YA SOKA JANA IJUMAA NA RATIBA YA HII LEO.
:
– Africa Cup of Nations – Round of 16.
AET Morocco 1 – 1 Benin *
FT Uganda 0 – 1 Senegal
.
– International – Club Friendlies.
FT Hobro 0 – 0 Fredericia
FT AC Horsens 0 – 4 AaB
FT FC Ufa 0 – 1 Viktoria Plzen
FT FC Twente 0 – 0 Al-Wahda
FT Austria Wien 2 – 1 Banik Ostrava
FT Sparta Rotterdam 1 – 0 Zaglebie Lubin
FT Xamax 1 – 5 FC Stade Lausanne-Ouchy
FT Grazer AK 2 – 0 Middlesbrough
FT LASK 1 – 0 Sparta Prague
FT Rijeka 1 – 2 PFC Sochi
FT Rubin Kazan 0 – 0 FC Tambov
FT Shakhtar Donetsk 2 – 1 FC Koebenhavn
FT AS Beziers 0 – 0 Nimes
FT FC Krasnodar 0 – 2 Ural
FT FK Akhmat 1 – 1 Inter Zapresic
FT Slovan Liberec 0 – 1 Dinamo Moscow
FT SpVg Frechen 20 1 – 7 1. FC Köln
FT VVV-Venlo 3 – 3 St.Truiden
FT Wolfsberger AC 1 – 0 SK Austria Klagenfurt
FT FC Emmen 1 – 1 PEC Zwolle
FT FC Groningen 2 – 0 Ross County
FT Kortrijk 2 – 0 OH Leuven
FT Lugano 2 – 2 Chiasso
FT SC Heerenveen 5 – 4 SV Meppen
FT Taffs Well 1 – 5 Cardiff City
FT AFC Wimbledon 0 – 3 Brentford
:
RATIBA YA HII LEO JUMAMOSI.
– Copa America – 3rd place W.
22:00 Argentina
Chile
.
– World Cup Women – 3rd place W.
18:00 England
Sweden
.
– Africa Cup of Nations – Round of 16.
19:00 Nigeria
Cameroon
22:00 Egypt
South Africa
#fixtures #Updates
@Sokawaytz_

FAMILIA 7 ZAKOSA MAHALI PA KUISHI BAADA YA NYUMBA ZAO KUBOMOLEWA –

FAMILIA 7 ZAKOSA MAHALI PA KUISHI BAADA YA NYUMBA ZAO KUBOMOLEWA

Familia 7 katika Mtaa wa Olasiti Kati jijini Arusha, hazina mahali pa kuishi kufuatia nyumba zao kubomolewa kwa amri ya Mahakama kutokana na mgogoro wa Ardhi uliokuwa ukiendelea baina yao na Mkazi wa Kiteto, Mwanamkasi Ramadhani

Wakiongea Mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqar wameeleza masikitiko yao jinsi nyumba zao zilivyovunjwa mapema leo na kusababisha uharibifu mkubwa wa Mali huku familia hizo wakiwemo watoto wadogo wasijue la kufanya

Baadhi ya wakazi hao wamedai zoezi hilo limetekelezwa bila kufuata utaratibu ambapo mapema leo wamejikuta wakivunjiwa nyumba zao bila kupewa muda wa kujiandaa

Akihojiwa na Mkuu wa wilaya, mmiliki wa eneo hilo Mwanamkasi Ramadhan amesema kuwa kubomolewa kwa nyumba hizo ni utekelezaji wa amri ya Mahakama baada ya kushinda kesi saba zikiwemo za rufaa katika mgogoro wa eneo hilo ulioanza mwaka 2006

UKRAINE: KUFUATIA KUTUNGWA KWA SHERIA YA KUZUIA MATUSI: WAZIRI ASEMA MATUSI NI MAZURI KWA AFYA

UKRAINE: KUFUATIA KUTUNGWA KWA SHERIA YA KUZUIA MATUSI: WAZIRI ASEMA MATUSI NI MAZURI KWA AFYA

Naibu Waziri wa Afya, Ulana Suprun amesema kuwa matusi ni mazuri kwa afya ya Mwanadamu. Amefafanua kuwa matusi ni mawasiliano mazuri ya kihisia baina ya Watu

Suprun ametoa kauli hiyo wakati akichangia mapendekezo ya sheria inayolenga kusitisha lugha chafu katika vyombo vya habari

Sheria hiyo imependekeza kuwa watu watakaokutwa na hatia ya kutukana katika maeneo ya umma na katika hotuba watatozwa faini ya Shilingi za Kitanzania 112,538

UKAGUZI WA BIDHAA: MAKONTENA 142 YALIKUTWA NA BIDHAA BANDIA –

UKAGUZI WA BIDHAA: MAKONTENA 142 YALIKUTWA NA BIDHAA BANDIA

Tume ya Ushindani imefanya ukaguzi katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita 2017/2018 wa makontena 3,312 na kubaini makontena 142 yalikuwa na bidhaa bandia

Mkurugenzi wa Utekelezaji Sheria, Dkt. John Nangala amesema ukaguzi huo ulifanywa katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma, Morogoro, Mwanza, Arusha, Mbeya na mipaka yote ya nchi

Aidha, Nangala amesema lengo la kufanya ukaguzi huo ni kujenga uelewa wa bidhaa bandia na katika kipindi hicho wamepokea kesi za ushindani malalamiko 60

Design a site like this with WordPress.com
Get started