Klabu ya Yanga Sc imekamilisha usajili wa beki wa kushoto Muharami Issa “Marcelo” kutoka Malindi Fc ya Zanzibar

#DealDone Klabu ya Yanga Sc imekamilisha usajili wa beki wa kushoto Muharami Issa “Marcelo” kutoka Malindi Fc ya Zanzibar kwa mkataba wa miaka mitatu na kupewa jezi namba 2 iliyokuwa ikivaliwa na Gadiel Michael
.
.
Issa wiki chache zilizopita alitangazwa kuwa amesajiliwa Singida Utd kwa mkataba wa miaka mitatu

#AFCON….VIKOSI⚽ *🇳🇬NIGERIA vs CAMEROON🇨🇲*

⚽ *🇳🇬NGA vs CMR🇨🇲*

*NGA🇳🇬*
16 Daniel Akpeyi (Goalkeeper)
20 Chidozie Awaziem (Defender)
5 William Troost-Ekong (Defender)
22 Kenneth Omeruo (Defender)
2 Ola Aina (Defender)
8 Oghenekaro Etebo (Midfielder)
4 Wilfred Ndidi (Midfielder)
15 Moses Simon (Midfielder)
18 Alex Iwobi (Midfielder)
7 Ahmed Musa (Midfielder)
9 Odion Ighalo (Forward)

*CMR🇨🇲*
1 André Onana (Goalkeeper)
4 Yaya Banana (Defender)
5 Michael Ngadeu Ngadjui (Defender)
14 Georges Mandjeck (Defender)
2 Collins Fai (Midfielder)
15 Pierre Kunde (Midfielder)
13 Eric Maxim Choupo-Moting (Midfielder)
6 Ambroise Oyongo (Midfielder)
11 Christian Bassogog (Forward)
9 Stéphane Bahoken (Forward)
7 Clinton N’Jie (Forward)

*

MAREKANI: WANASAYANSI WAFANIKIWA KUONDOA VVU KWA PANYA

MAREKANI: WANASAYANSI WAFANIKIWA KUONDOA VVU KWA PANYA

Watafiti nchini Marekani wamesema wamefanikiwa kuondoa Virusi Vya Ukimwi kutoka kwenye vinasaba (DNA) vya panya, mafanikio ambayo wanasayansi wanasema yanaweza kuwa hatua ya kwanza kuelekea kupata tiba ngumu ya ugonjwa huo kwa binadamu

Matokeo ya utafiti huo yaliyotangazwa wiki hii yamethibitishwa na wanasayansi zaidi ya 30 kutoka Vyuo Vikuu vya Temple na kile cha Tiba cha Nebraska

Mmoja wa watafiti waandamizi, Kamel Khalili amesema kutokana na mafanikio hayo endapo mamlaka za chakula na dawa zitathibitisha tiba hiyo kwa binadamu inaweza kuanza kutumika mapema mwaka ujao

Watafiti hao wanasema hatua hiyo imewezekana kwa kuchanganya dawa za kufubaza maambukizi ya virusi na kifaa kinachoitwa CRISPR ambacho kinaweza kubadilisha jeni

Watafiti hao waliondoa Virusi hivyo katika panya 9 kati ya 23 ambao mifumo yao ya kinga ilibadilishwa kulingana na ile ya binadamu

RAIA WA KIGENI MBARONI KWA KUSAFIRISHA DHAHABU BILA KIBALI

RAIA WA KIGENI MBARONI KWA KUSAFIRISHA DHAHABU BILA KIBALI

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watu watatu raia wa kigeni waliokuwa wakitokea Wilaya ya Chunya kuelekea Jijini Dar es salaam kwa kosa la kusafirisha madini aina ya dhahabu bila kuwa na kibali

Watuhumiwa hao ni Clive Rooney (62) raia wa Ireland, Ross Stephen Chertsey (34) pamoja na Robert Charles (58) wote raia wa Uingereza ambao walikamatwa na maafisa wa usalama wa uwanja wa ndege wa Songwe

Madini hayo yalikuwa na uzito wa gramu 1,044.95

| Mshambuliaji wa Klabu Chelsea, Alvaro Morata atajiunga na Atletico Madrid kwa Mkataba wa Moja kwa moja

OFFICIAL | Mshambuliaji wa Klabu Chelsea, Alvaro Morata atajiunga na Atletico Madrid kwa Mkataba wa Moja kwa moja kwa moja baada ya mkopo wake wa miezi 18 kumalizika mwishoni mwa msimu ujao.
:
– Morata, mwenye umri wa miaka 26, amekuwa kwa mkopo Rojiblancos tangu Januari, akifunga mabao sita katika michezo 17 kwa upande wa Klabu hiyo ya Hispania… Alijiunga Na Chelsea kaa rekodi ya Klabu kwa dau la £60m kutoka Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitano aliosaini mwezi Julai 2017 na tangu atue Stamford Bridge akafunga mabao 24 katika michezo 72 na kutwaa Ubingwa wa FA Cup.
:
– Atletico itamsajili Moratta kwa dau la uhamisho £50m siku ya Juni Mosi 2020, kwa Kipindi hiki bado atakuwa Kama yupo kwa mkopo mpaka Mwisho wa msimu wa 2019/20 ndio atasaini Rasmi kuelekea msimu wa 2020/21…
#TransferNewsUpdates
@Sokawaytz_

Kocha wa Taifa Stars Emmanuel Amunike amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kuzungumzia tathmini ya ushiriki wa timu hiyo kwenye michuano ya #AFCON2019

– Kocha wa Taifa Stars Emmanuel Amunike amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kuzungumzia tathmini ya ushiriki wa timu hiyo kwenye michuano ya #AFCON2019 inayoendelea nchini Misri ambapo @taifastars_ imeondoshwa Baada ya kufungwa game zote tatu za hatua ya Makundi.
.
– Kwa Ujumla, Amunike ambaye Ni legend wa Nigeria, akiwa Kama kocha wa Timu ya taifa ya Tanzania, kaiongoza katika Michezo 10, Akipoteza Mara Sita na Ushindi Mara mbili kisha Sare Mara mbili..
#Updates #TaifaStars

Design a site like this with WordPress.com
Get started