#

ExtraTime | Hassan Dilunga chini ya Sven yuko moto kweli kweli
Mpaka sasa amefunga Mabao 5. Kwa namba, Dilunga ndio mchezaji hatari zaidi kwenye kikosi cha Simba
Nini Sven amekiongeza kwa Dilunga kiufundi?
Chini ya Sven, huwa inacheza 4-2-3-1 ikiwa haina mpira, lakini huswitch kwenda kwenye 3-4-1-2 inapokwenda kushambulia
Ipi ‘role’ ya Dilunga hapa? Kwenye maratasi unaweza kumuona akipangwa kama winga wa kulia, lakini kimuundo huja kwenye eneo tofauti kabisa
Kitaalamu inatwa ‘Halbraum’. A half space midfielder
Anazunguka kwenye umbo la pembetatu (katikati ya kiungo wa ulinzi, beki wa kushoto na beki mmoja wa kati)
Simba ikiwa haina mpira anashiriki kutengeneza Balance ya timu kwa kukaa kwenye eneo ambalo mabeki wa timu pinzani watashindwa kufanya build up kutoka chini
.
.
Kwa jukumu hili, timu pinzani hulazimika kupiga mipira mirefu. (Hapa ndipo Svan anapochemka kuipanga timu yake nyuma baada ya kufanikiwa mtego wa mbele)
Simba ikiwa na mpira, anasaidia kuvuruga umakini wa beki wa kati na beki wa kushoto (pamoja na kiungo pindi anapoingia ndani)
Kwa jukumu hili, ndio unaona Kapombe amekua na eneo kubwa sana anapopanda.
Tazama bao lake lilivyokua.
Tazama movement za wachezaji wa mbele wa Simba zilivyokua. Fantastic👏
Kagere, Ajib waliasist hili bao kwa movement tu. Kitaalam inaitwa ‘Dispersal’ (Uwezo wa mastraika kuwaondoa mabeki kwenye nafasi zao)
Tazama Mobility ya Dilunga. Kwanza, alikimbia mbele, baadae akaghairi. Akanusa hatari. Aliporudi, akapokea mpiraa akiwa free.
Akakimbia na Kikoti. Wakati huo Kagere na Ajib wakiwa wameshaivuruga safu ya ulinzi kwa movement zao, Dilunga alipoturn tu, akajikuta macho yake yanamuona Balora kwa mita 23
.
.
Ana uwezo wa kupiga. Akapiga na kuweka bao safi👏
Hivo ndivyo falsafa ya Sven na ubora wake wa mbinu pindi timu inaposhambulia, ulivyoweza kumbadilisha Dilunga.