IRAN: TUTAJIBU HATUA YA UINGEREZA KUKAMATA MELI YETU YA MAFUTA

IRAN: TUTAJIBU HATUA YA UINGEREZA KUKAMATA MELI YETU YA MAFUTA

Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Iran, Meja Jenerali Mohammad Bagheri amesema leo kwamba hatua ya Uingereza kuikamata meli yake ya mafuta nje ya eneo la Gibraltar haitapita bila majibu

Jeshi la majini la Uingereza liliingia katika meli hiyo, Grace 1, nje ya pwani ya Gibraltar siku ya Alhamis na kuikamata kuhusiana na shutuma kwamba inavunja vikwazo kwa kupeleka mafuta nchini Syria

Iran imetaka kuachiwa mara moja kwa meli hiyo ya mafuta, huku Kamanda huyo wa Jeshi la Mapinduzi la Iran siku ya Ijumaa alitishia kukamata meli za Uingereza kwa kulipa kisasi

RAIS MAGUFULI AZINDUA HIFADHI YA BURIGI-CHATO, AMPONGEZA FARU RAJABU

RAIS MAGUFULI AZINDUA HIFADHI YA BURIGI-CHATO, AMPONGEZA FARU RAJABU

Rais Magufuli amempongeza faru Rajabu, ambaye ni mtoto wa Faru John kwa juhudi zake za uzalishaji na kuzidi kuongeza idadi ya faru hadi kufikia faru 140, katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti

Amesema hayo leo Julai 9, wakati wa Uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato, iliyopatikana mara baada ya mapori matatu ya akiba kuunganishwa, likiwemo pori la Burigi, Biharamulo na Kimisi

Amesema ”Hakuna budi kupongeza kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na faru Rajabu, mtoto wa faru John naambiwa kwasasa amezalisha watoto 40, nadhani wajina wangu John alikuwa hajitumi vizuriโ€

Aidha, amebainisha kuwa “Mwaka 2014 kulikuwa kuna Tembo 43,330 lakini hivi sasa baada ya kuanzisha kikosi cha kupambana na ujangili wamefikia zaidi ya 60,000โ€

MFUMUKO WA BEI WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 0.2 NDANI YA MWEZI

MFUMUKO WA BEI WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 0.2 NDANI YA MWEZI

Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi, Daniel Masolwa amesema mfumuko wa bei wa Taifa kwa Mwezi Juni, 2019 umeongezeka hadi asilimia 3.7 kutoka asilimia 3.5 kwa mwezi Mei, 2019

Amesema hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Juni, 2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya iliyokuwepo kwa mwezi Mei, 2019

Amefafanua kuwa hali hiyo imechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Juni, 2019 zikilinganishwa na bei ya bidhaa za mwezi Mei, 2019

Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa mwezi Juni, 2019 ni pamoja na unga wa mahindi kwa 3.6%, Unga wa ngano kwa 4.4%, mtama kwa 4.9%, samaki wabichi kwa 27.3%, dagaa kwa 16.5%, mafuta ya kupikia kwa 9.5%, maharage 3.0%, mihogo kwa 16.6% na viazi mviringo kwa 18.8%

Aidha, baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa mwezi Juni, 2019 ni pamoja na dizeli kwa 11.4%, petroli kwa 4.9%, gharama za kulala kwenye nyumba za wageni kwa 5.8% na vitabu vya shule kwa 2.4%

Lakini pia, mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi mwezi Juni, 2019 umeongezeka hadi asilimia 2.3 kutoka asilimia 2.2 kwa mwezi Mei, 2019

MIILI YA WAFANYAKAZI WATANO WA AZAM MEDIA GROUP YAAGWA –

MIILI YA WAFANYAKAZI WATANO WA AZAM MEDIA GROUP YAAGWA

Miili ya Wafanyakazi wa Azam Media Group waliofariki jana wakiwa ni miongoni mwa Watu 7 waliofariki katika ajali iliyohusisha Lori na basi mkoani Singida imeegwa leo Tabata jijini Dar katika Ofisi za Azam

Viongozi mbambali wamehudhuria tukio hilo akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe; Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na viongozi wengine

Wafanyakazi hao walikuwa wakielekea Chato mkoani Geita kwenye shughuli ya uzinduzi wa Hifadhi ya Burigi-Chato ambapo Rais Magufuli ni mgeni rasmi

– Rais wa Uganda ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ, Mh. Yoweri Kaguta Museveni Amekabidhi kitita cha fedha US$1 million (Tshs. 2.2b) kwenda kwa timu ya taifa ya @ugandacranes

– Rais wa Uganda ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ, Mh. Yoweri Kaguta Museveni Amekabidhi kitita cha fedha US$1 million (Tshs. 2.2b) kwenda kwa timu ya taifa ya @ugandacranes kwa kuonesha kiwango safi katika Michuano ya #AFCON2019 huko Misri ambapo walitolewa hatua ya 16 bora.
#TotalAFCON2019 #AFCONUpdates

Licha ya Dirisha la uhamisho wa Wachezaji kupoa kwa Vilabu vya Premier league… Lakini Usajili huo huo mchache Zimetumika pesa ndefuu!.

Licha ya Dirisha la uhamisho wa Wachezaji kupoa kwa Vilabu vya Premier league… Lakini Usajili huo huo mchache Zimetumika pesa ndefuu!.
๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡ธ Rodri (ยฃ62.6m)
๐Ÿ‡ซ๐Ÿ‡ท Tanguy Ndombele (ยฃ55.5m)
๐Ÿด๓ ง๓ ข๓ ฅ๓ ฎ๓ ง๓ ฟ Aaron Wan-Bissaka (ยฃ45m)
๐Ÿ‡ญ๐Ÿ‡ท Mateo Kovacic (ยฃ40.2m)
๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ช Youri Tielemans (ยฃ40m)
#PremierLeagueUpdates

Design a site like this with WordPress.com
Get started