PSG: NEYMAR ANAWEZA KUONDOKA IWAPO OFA YA KUNUFAISHA PANDE ZOTE ITAPATIKANA

PSG: NEYMAR ANAWEZA KUONDOKA IWAPO OFA YA KUNUFAISHA PANDE ZOTE ITAPATIKANA

Mkurugenzi wa Michezo wa Klabu ya Paris St-Germain(PSG), Leonardo amesema hayo na kuongeza kuwa hawajapokea ofa yoyote kwa ajili ya Neymar ila kulikuwa na mawasiliano madogo sana na Barcelona

Mchezaji huyo raia wa Brazil mwenye miaka 27 ambaye amekuwa akihusishwa na kutaka kurudi Barcelona, alishindwa kuhudhuria mazoezi ya kujiandaa na msimu siku ya Jumatatu na PSG ilisema itachukua hatua stahiki

Alipoulizwa kama Neymar amewasilisha maombi ya kuondoka Klabuni hapo, Leonardo amesema “Iko wazi kwa kila mtu. Lakini kwenye mpira, unasema kitu kimoja leo na kingine kesho. Iko hivyo.”

Baba wa Neymar amesema kuwa Klabu hiyo ilikuwa inajua kuwa mwanaye atakosa mazoezi ya kwanza siku ya Jumatatu kutokana na masuala yake ya msaada katika Taasisi ya Neymar na kuwa atarudi PSG Julai 15

Je, unadhani Neymar atakuwa anachezea PSG au Barcelona msimu ujao?

Paris St-Germain imesema kuwa itachukua hatua kali baada ya mshambuliaji wa Brazil Neymar kushindwa kuhudhuria mazoezi ya kwanza ya timu hiyo

Paris St-Germain imesema kuwa itachukua hatua kali baada ya mshambuliaji wa Brazil Neymar kushindwa kuhudhuria mazoezi ya kwanza ya timu hiyo… Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alitarajiwa kurudi katika mazoezi siku ya Jumatatu.
.
– Mshambuliaji huyo amehusishwa na uhamisho kurudi klabu yake ya zamani ya Barcelona… Neymar alijiunga na PSG kutoka Barcelona kwa dau lililovunja rekodi la £200m mnamo mwezi Agosti 2017. Lakini pia Neymar amehusishwa na makosa kadhaa ya utovu wa nidhamu ikiwemo kufungiwa kwa mechi tatu kwa kumpiga shabiki baada ya PSG kupoteza katika kombe la ligi ya Ufaransa…Pia atakosa kushiriki mechi tatu za Michuano ya Ulaya kwa kumtusi afisa wa mechi.
.
– Kulingana na ripoti katika vyombo vya habari vya Uhispania , Neymar amekubali kupunguziwa mshahara wake kwa £12m ili kurudi katika klabu yake ya @fcbarcelona ambapo alicheza kati ya mwaka 2013 hadi 2017.. Mabingwa wa Ufaransa PSG wamesema kuwa watamuuza Neymar kwa Klabu ambayo itafika na dau nono, kwa mujibu wa vyanzo Barça wameambiwa waambatanishe Pesa na Mchezaji mmoja Kati ya Beki, Samuel Umtiti au Mshambuliaji, Malcom katika Mazungumzo ya uhamisho wa Neymar..
#transfersUpdates #TransferNewsUpdates

Klabu ya Liverpool ipo mbioni kuzipiku Real Madrid ya Hispania na Paris St-Germain ya Ufaransa kumsajili kinda machachari kutoka klabu ya Fulham, Harvey Elliott.

– Klabu ya Liverpool ipo mbioni

kuzipiku Real Madrid ya Hispania na Paris St-Germain ya Ufaransa kumsajili kinda machachari kutoka klabu ya Fulham, Harvey Elliott.
.
– Elliott aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kukipiga kwenye Ligi Kuu Nchini Uingereza @premierleague alipoingia kama mchezaji wa akiba kwenye mchezo wa Fulham dhidi ya Wolverhampton Wanderers mwezi Mei akiwa na umri wa miaka 16 na siku 30.
.
– Kwasasa Hawezi kuwa mchezaji wa kulipwa mpaka atakapotimu umri wa miaka 17, ambayo itakuwa ni Aprili mwakani… Inatarajiwa kuwa nyota huyo atakataa ofa ya masomo ya kuendelea kusalia katika klabu ya Fulham yenye maskani yake kwenye uwanja wa Craven Cottage ili aungane na mabingwa wa Klabu Bingwa Ulaya, klabu ya Liverpool… Majogoo itawabidi wailipe Fulham dau ili wamsajili Muingereza huyo anaeitumikia timu ya taifa ya England U17.
#EPLTransfersUpdates #EPLUpdates

Matokeo ya Mechi za Michuano ya CECAFA Kagame Cup zilizopigwa hi Leo, Kigali, Rwanda 🇷🇼.

👉🏻 Matokeo ya Mechi za Michuano ya

CECAFA Kagame Cup zilizopigwa hi Leo, Kigali, Rwanda 🇷🇼.
:
FT: Azam FC 0-1 KCCA UG
FT: KMC 0-1 TP Mazembe
FT: Bandari FC 2-2 Mukura VS
20:30 Atlabara FC vs Rayon Sports
#CECAFAKagameCup #KagameCup2019

Mkuu wa timu ya taifa ya Morocco 🇲🇦, Herve Renard 🇫🇷, ameachia ngazi Kama kocha Mkuu wa timu hiyo ya taifa.

– Ripoti Mbalimbali kutoka Nchini Morocco 🇲🇦 zinaripoti kwamba, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Morocco 🇲🇦, Herve Renard 🇫🇷, ameachia ngazi Kama kocha Mkuu wa timu hiyo ya taifa.
.
– Mfaransa huyo alichukua Mikoba Rasmi ya kuinoa Morocco 🇲🇦, Mwezi Machi 2016. Kocha Renard mwezi November 2017, aliiongoza Morocco Kufuzu kucheza Kombe la Dunia kwa Mara yao ya Kwanza tangu 1998… Alisaini Mkataba Mpya mwezi uliofuata unaomfanya kusalia mpaka Mwaka 2022… Chanzo Cha kuripotiwa kutimka Ni kufanya vibaya kwa taifa hilo katika Fainali za AFCON ambapo walitupwa nje kwenye hatua ya 16 Bora walipopoteza dhidi ya Timu ya taifa ya Benin 🇧🇯..
#Updates

IRAN: TUTAJIBU HATUA YA UINGEREZA KUKAMATA MELI YETU YA MAFUTA

IRAN: TUTAJIBU HATUA YA UINGEREZA KUKAMATA MELI YETU YA MAFUTA

Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Iran, Meja Jenerali Mohammad Bagheri amesema leo kwamba hatua ya Uingereza kuikamata meli yake ya mafuta nje ya eneo la Gibraltar haitapita bila majibu

Jeshi la majini la Uingereza liliingia katika meli hiyo, Grace 1, nje ya pwani ya Gibraltar siku ya Alhamis na kuikamata kuhusiana na shutuma kwamba inavunja vikwazo kwa kupeleka mafuta nchini Syria

Iran imetaka kuachiwa mara moja kwa meli hiyo ya mafuta, huku Kamanda huyo wa Jeshi la Mapinduzi la Iran siku ya Ijumaa alitishia kukamata meli za Uingereza kwa kulipa kisasi

Design a site like this with WordPress.com
Get started