
Half Time. .
Nigeria 1-0 South Afrika .
Samuel ⚽
.
#AFCON2019

Half Time. .
Nigeria 1-0 South Afrika .
Samuel ⚽
.
#AFCON2019


Full Time. .
Senegal 1-0 Benin .
Gueye ⚽
.
#AFCON2019


Klabu ya Barcelona inadaiwa kumuwania beki wa Manchester United, Victor Lindelof kama haitafanikiwa kumsajili beki wa Ajax, Matthijs de Ligt anayeripotiwa kukubaliana mshahara na Juventus
–
Meneja wa Lindelof, Hasan Cetinkaya amesema kuwa Mchezaji huyo raia wa Sweden yupo kwenye rada ya vilabu vikubwa barani Ulaya, lakini kuondoka United inategemea na Klabu yenyewe
–
Wakati huo huo, Manchester United inadaiwa kuwa inamuangalia kwa karibu Kiungo wa Tottenham, Christian Eriksen ili iweze kumsajili iwapo mchezaji wake, Paul Pogba ataondoka klabu hapo
–
Hata hivyo, Eriksen amekuwa akihusishwa muda mrefu na kutaka kujiunga na Real Madrid huku Pogba naye akidaiwa kuwa anataka kuondoka United na kujiunga Real Madrid

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI MAREKANI AJIUZULU
–
Balozi Kim Darroch amejiuzulu ikiwa ni matokeo ya kuvuja kwa barua pepe zinazoukosoa utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump kwa kusema kuwa utawala huo hauna weledi
–
Balozi huyo, aliyeitwa ‘Mpumbavu’ na Rais Trump baada ya barua pepe hizo kuvuja amesema anataka kumaliza mzozo uliokuwepo na kuongeza kuwa uvujaji huo umefanya utendaji kazi wake kuwa mgumu
–
Amesema “Tangu kuvuja kwa nyaraka za kiofisi kutoka ubalozi huu kumekuwa na hisia kuhusu nafasi yangu na muda wangu uliobaki kama Balozi. Ninataka nizimalize hisia hizo.”
–
Barua hizo zilizofichuliwa na gazeti la Uingereza, Mail zilionesha Kim akisema “Hatuamini kwamba utawala huu(Utawala wa Trump) utakuwa sawa. Haujielewi na usiojali sana kuhusu diplomasia. Na kuhoji iwapo Ikulu hiyo itakuwa na utendaji kazi mzuri

MAREKANI KUUNDA MUUNGANO WA MATAIFA ILI KUPAMBANA NA VITISHO VYA IRAN
–
Afisa wa Juu wa Jeshi la Marekani amesema Washington itaendelea na mipango ya kuunda Muungano wa Mataifa ili kufutialia na kukabiliana na vitisho vya Iran
–
Amebainisha kuwa vitisho hivyo ni dhidi ya shughuli za usafirishaji katika eneo ghuba na mlango bahari muhimu wa Hormuz uliopo katikati ya ghuba ya Oman na Persian
–
Jenerali Joseph Dunford amesema kuwa tayari wameandaa mpango mahsusi na katika wiki chache zijazo itakuwa wazi ni mataifa yapi yatajiunga na juhudi hizo za Marekani
–
Juhudi hizo za Marekani zinafuatia wasiwasi wa utawala wa Rais Trump kwamba Iran ndiyo iliongoza mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya meli za mafuta katika eneo la ghuba

JAJI MUTUNGI: VYAMA VYA SIASA HAVIJAWAHI KULALAMIKA KWA MAANDISHI KUHUSU KUZUIWA MIKUTANO
–
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amesema ofisi yake haijawahi kupokea malalamiko ya maandishi kutoka vyama vya upinzani kuhusu kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara
–
Alisema vyama vinapaswa kutuma malalamiko yao kwa maandishi ili ofisi yake ipate cha kuanzia “Sasa wao hawalalamiki lakini waandishi mnalalamika, huoni kama wanaweza wakawaruka?”
–
Mara kadhaa, viongozi wa upinzani wamekuwa wakilalamikia jambo hilo katika maeneo mbalimbali na katika Bunge la bajeti lililomalizika Juni 28, Freeman Mbowe na Zitto Kabwe walihoji suala hilo
–
Aidha, Katibu mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji amesema “malalamiko ya mikutano ya hadhara hatujapeleka. Tunajua hana ubavu wa kuifanyia chochote kwa sababu aliyeagiza ni bosi wake.”
–
Pamoja na uamuzi huo, Dkt. Mashinji alisema kuna malalamiko mengi yanayohusu malezi ya ofisi hiyo ambayo walishampelekea lakini hayafanyiwa kazi

UBALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA KUTOSHUGHULIKIA MASUALA YA ‘VISA’
–
Ubalozi huo uliopo Jijini Dar umetangaza kwamba kuanzia Agosti 01, 2019 hautakuwa na jukumu la kushughulikia ‘visa’ za safari ‘Schengen Visa’ au ‘visa’ za Makazi kwa Watanzania wanaotaka kwenda Norway
–
Badala yake fomu zote za maombi zitakazokusanywa Tanzania zitasafirishwa kwenda Ubalozi wa Norway uliopo Nairobi, Kenya ambao ndio unashughulikia masuala ya Uhamiaji kwa Kanda ya Afrika Mashariki
–
Waombaji wote, kama ilivyo kuanzia Mei 13, 2019 wanatakiwa kufika na kupelekea fomu za maombi katika Ofisi za VFS Global zilizopo Dar, Jengo la Maktaba Square, ghorofa ya 4, Upande B
–
VFS Global itahakikisha fomu za maombi zinasafirishwa kufika Nairobi kwa ajili ya kufanyiwa kazi zaidi. Na pia Waombaji wote kupitia VFS Global wataweza kuchukua ‘Visa’ zao katika Ofisi hizo hizo
–
Kutokana na hivyo, kutakuwa na ada ya maombi na ada ya huduma kama ilivyokuwa awali ila kutaongezeka ada ya usafirishaji fomu hizo kutoka Dar hadi Nairobi, ada hiyo inalipwa kwa VFS Global siku ya kukusanya fomu za maombi
–
Aidha, kutokana na mfumo huo mpya, muda wa kusubiri ‘visa’ utaongezeka kwa maana muda wa kufanyiwa kazi kwa Schengen visa kutoka Nairobi hadi Norway kutachukua hadi siku 15 tangu siku maombi yamepokelewa Nairobi. Hivyo inashauriwa kutuma maombi yako walau wiki nne kabla ya ratiba zako za kusafiri


Timu ya Wanawake (Simba Queens) inatarajiwa kuondoka nchini siku ya Jumatatu Julai 15, 2019 kwenda nchini Ujerumani kwa ziara ya kisoka ya wiki mbili.
Msafara wa timu hiyo utakuwa na jumla ya watu 16, wachezaji wakiwa 13 na viongozi watatu, ambapo mkuu wa msafara atakuwa ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Asha Baraka.
Wakiwa nchini humo, wachezaji wa Simba Queens watapata nafasi ya kushiriki semina mbalimbali za kijamii ambazo zina lengo la kuwapa mbinu mbadala za kazi ambazo wanaweza kufanya nje ya maisha ya soka.
Pamoja na hilo pia watacheza michezo minne ya kirafiki ambapo michezo mitatu itachezwa mjini Hamburg na mwingine mmoja kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Berlin.
Baada ya semina ambayo itakuwa na manufaa makubwa kwa wachezaji wetu na michezo ya kirafiki ambayo itasaidia kuandaa kikosi kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Wanawake, msafara wa Simba Queens utarejea nchini siku ya Alhamisi Agosti mosi, 2019.
Safari ya Simba Queens imedhaminiwa na Serikali ya Ujerumani kwa kushirikiana na Simba SC. #NguvuMoja


✍️ Wachezaji Wanne tofauti wanaongoza Msimamo wa kufunga Magoli mengi katika Fainali za AFCON zinazoendelea Ambapo Sasa Ni hatua ya Robo fainali..
:
✍🏻 RATIBA ya Mechi za Robo fainali ya AFCON 2019 hii leo.
📅 Julai 10; 2019
19:00 Benin 🇧🇯 v Senegal 🇸🇳 (🏟 30 June Stadium).
22:00 Nigeria 🇳🇬 v South Africa 🇿🇦 (🏟 Cairo Int’l Stadium).
#AFCON2019 #TotalAFCON2019 #AFCONUpdates


OFFICIAL | Klabu ya KMC FC Imekamilisha Usajili wa Kiungo wa Kimataifa wa Rwanda 🇷🇼, Jean-Baptiste Mugiraneza kutoka klabu ya APR FC ya Rwanda kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Mugiraneza 28, aliwahi kuitumikia Azam FC ya Tanzania misimu michache iliyopita kabla ya kutimka Nchini Disemba 2017 na kujiunga na GOR Mahia ya Kenya kisha kutua APR FC ya kwao Rwanda 🇷🇼, Mugi Ni miongoni mwa Wachezaji 16 wa Klabu hiyo ya Jeshi waliotemwa klabuni..