Mabingwa wa Hispania 🇪🇸, Klabu ya FC Barcelona Imethibitisha Kukamilisha Uhamisho wa Bingwa wa Dunia Mwaka 2018, Antoine Griezmann

OFFICIAL | Mabingwa wa Hispania 🇪🇸, Klabu ya FC Barcelona Imethibitisha Kukamilisha Uhamisho wa Bingwa wa Dunia Mwaka 2018, Antoine Griezmann kutoka Kwa Wapinzani wao wa Laliga, Atletico Madrid… Barcelona hii leo Imevunja Kipengele Cha Uhamisho wa Mfaransa huyo ambacho Ni €120m na wao Baada ya kumpa Mkataba wameweka Kipengele Cha Kama Timu nyingine ikimtaka italipa €800m..
.
– Rekodi ya Antoine Griezmann tangu msimu wa 2014/15 mpaka mwisho wake akiwa na jezi ya Atletico Madrid..
2018/19 – Antoine Griezmann (21⚽)
2017/18 – Antoine Griezmann (29 ⚽️)
2016/17 – Antoine Griezmann (26 ⚽️)
2015/16 – Antoine Griezmann (32 ⚽️)
2014/15 – Antoine Griezmann (25 ⚽️)
#TransferNewsUpdates #transfersUpdates

Yanga yathibitisha kucheza na As vita Agosti 4.2019

OFFICIAL | Uongozi wa klabu ya YANGA SC umethibitisha kuwa kuelekea kwenye kilele Cha wiki ya Mwananchi tarehe Agosti 4, 2019 timu hiyo itacheza mchezo wa kirafiki na timu ya As Vita kutoka Congo. .
.
Ikumbukwe As Vita inanolewa na kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Congo Florent Ibenge ambaye msaidizi wake ni Mwinyi Zahera
.

Timu ya Wanawake (Simba Queens) leo imekabidhiwa bendera ya Taifa kuelekea nchini Ujerumani ambako itafanya ziara ya kisoka ya wiki mbili

T

Timu ya Wanawake (Simba Queens) leo imekabidhiwa bendera ya Taifa kuelekea nchini Ujerumani ambako itafanya ziara ya kisoka ya wiki mbili. Msafara wa timu hiyo unatarajiwa kuondoka hapa nchini Jumatatu Julai 15, 2019 na utarejea nchini Alhamisi Agosti mosi, 2019. #NguvuMoja

OFFICIAL| Legendary, Peter Crouch ametangaza Kustaafu Kucheza Mpira wa Miguu akiwa na umri wa miaka 38..

OFFICIAL| Legendary, Peter Crouch ametangaza Kustaafu Kucheza Mpira wa Miguu akiwa na umri wa miaka 38..
👕 715 Mechi
⚽️ 209 Magoli
🅰️ 69 Assists
🌍 9 Vilabu
🏆 3 Mataji
:
– Peter Crouch kafunga Magoli 53 kwa kichwa Kipindi Cha Maisha yake ndani ya Ligi Kuu Uingereza “Premier League”, Mengi zaidi kuliko Mchezaji yoyote Katika Historia ya Ligi.. Mpaka Sasa Ni Mchezaji Pekee kufunga Magoli 50+ kwa kichwa 🙌🙌🙌.. Giant.
#footballlover #Updates

Klabu ya Arsenal imewajumuisha makinda wake 10 kwenye safari yao ya North American kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Klabu ya Arsenal imewajumuisha makinda wake 10 kwenye safari yao ya North American kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.
.
🇧🇷 Gabriel Martinell
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Reis Nelson
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Bukayo saka
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Joe wilnock
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Zech medley
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Dominic Thompson
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 James onlanyika
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Emile smith
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Trycee john_joles
🇵🇹 Rorbie burton
Holla gunners👊🏽

Mshikemshike ndondo cup kuendelea leo…16 bora

Leo kwenye tutashuhudia game kali ya 16 bora ya #NdondoCup2019, ni vita ya wageni kwenye @ndondo_cup kuwania kucheza robo fainali kwa mara ya kwanza…hatari tupu!! .
.
Toroli Kombaini kutoka pande za Keko uso kwa macho na Goba Ham United kutoka Goba, hizi timu zote ni ngeni kwenye michuano hii…zimeingia mwa mara ya kwanza na kutusua hadi 16 bora.

Zimetoka na moto kuanzia hatua ya awali kabisa ya mashindano haya, zikavuka hatua ya makundi lakini leo timu moja itaenda robo fainali nyingine itabaki.

Goba Ham kwenye hatua ya AWALI ilishinda mechi mbili na sare moja ikamaliza pointi sawa na Ukwamani lakini ikabaki nafasi ya pili kwa wastani wa magoli.

KUNDI D
Ukwamani pointi 7
Goba Ham pointi 7
Taswa FC pointi 1
Rangers pointi 1

Toroli Kombaini ilitwanga mechi zake zote za hatua ya awali na kukusanya pointi zote na hatimaye kufuzu ikiwa kinara wa kundi lake.

KUNDI H
Toroli Kombaini pointi 9
Mafundi Ujenzi pointi 4
Tandika Kombaini pointi 3
Mwandege City pointi 1

HATUA YA MAKUNDI

Katika hatua ya makundi, Toroli ilifuzu tena kwa kishindo kwa kuongoza kundi baada ya kushinda mechi zake mbili na sare moja na kukusanya pointi 7 mbele ya vigogo Misosi na Keko Fenicha.

KUNDI A
Toroli Kombanini pointi 7
Misosi FC pointi 7
Keko Fenicha pointi 1
Mamu Pharmacy pointi 1

Goba Ham ilisubiri hadi siku ya mwisho ya mechi za kundi lake kujua hatma yake, ikafanikiwa kusonga mbele kwa tofauti ya magoli dhidi ya Misosi FC mabingwa wa Ndondo Cup 2017

KUNDI D
UV Temeke pointi 5
Goba Ham pointi 4
Mpakani Kombaini pointi 4
Ukwamani pointi 2

Toroli Kombaini vs Goba Ham, nani anaenda robo fainali nani anabaki?

UINGEREZA YADAI IRAN ILITAKA KUIZUIA MELI YAKE YA MAFUTA. IRAN YAKANUSHA

UINGEREZA YADAI IRAN ILITAKA KUIZUIA MELI YAKE YA MAFUTA. IRAN YAKANUSHA

Uingereza imedai kuwa tukio hilo limetokea juzi Jumatano kwenye mlango bahari wa Hormuz, muda mchache baada ya Rais Trump kurejea vitisho vyake vya kuongeza vikwazo vikali dhidi ya Iran

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema mashua tatu za Iran zilijaribu kuizuilia njia meli hiyo iitwayo British Heritage inayomilikiwa na Kampuni ya mafuta ya Uingereza, BP lakini zikaondoshwa na meli yake ya Kivita, HMS Montrose

Jeshi la Iran lilikana taarifa hizo likisema hakukuwa na makabiliano katika muda wa masaa 24 na meli yoyote ya kigeni, ikiwa ni pamoja na meli za Uingereza

Tukio hilo linakuja ikiwa ni takribani wiki moja tangu Irani iseme hatua ya Uingereza kuikamata meli yake ya mafuta nje ya eneo la Gibraltar kwa madai ilivunja vikwazo kwa kupeleka mafuta Syria, haitapita bila majibu

Aidha, siku chache zilizopita Marekani imesema itaendelea na mipango ya kuunda Muungano wa Mataifa ili kufutialia na kukabiliana na vitisho vya Iran dhidi ya shughuli za usafirishaji katika eneo Ghuba na mlango bahari wa Hormuz

RAIS WA UGANDA KUFANYA ZIARA BINAFSI, NCHINI

RAIS WA UGANDA KUFANYA ZIARA BINAFSI, NCHINI

Rais Yoweri Kaguta Museveni Kesho, Julai 13, 2019 atafanya ziara binafsi ya siku moja hapa nchini kwa kumtembelea Rais Magufuli

Atamtembelea Rais Magufuli Kijijini kwake, Mlimani katika Wilaya ya Chato, Mkoani Geita na akiwa huko atafanya mazungumzo na mwenyeji wake huyo

Design a site like this with WordPress.com
Get started