Paris Saint-Germain wamerudi mawindoni kumuwinda Kiungo, Idrissa Gana Gueye wa Everton

– Paris Saint-Germain wamerudi mawindoni kumuwinda Kiungo, Idrissa Gana Gueye wa Everton, Kwa mujibu wa L’Equipe, Gueye anawindwa kwa dau la uhamisho wa €30m (£27m / $34m) na majadiliano kati ya timu zote mbili yanaendelea.
:
– PSG walimfuata Gueye mwenye umri wa miaka 29 wakati wa dirisha lililopita la Januari, lakini hawakuweza kupata Saini ya Kiungo huyo wa Kimataifa wa Senegal 🇸🇳.. tayari Everton imeanza majadilio na Klabu ya Southampton wakimtaka Kiungo wao wa Kimataifa wa Gabon 🇬🇦, Mario Lemina Kama mbadala wa Gueye.. kwenye uhamisho wa Lemina watakutana na upinzani kutoka kwa Arsenal na Manchester United ambazo zote zinamuhitaji..
#EPLTransfersUpdates #EPLUpdates

SOMALIA: HOTELI YASHAMBULIWA KWA ZAIDI YA SAA MOJA‬

SOMALIA: HOTELI YASHAMBULIWA KWA ZAIDI YA SAA MOJA‬

Hoteli ya Kismayo imeshambuliwa na Al-Shabaab na kusababisha vifo vya watu 26 hadi sasa na majeruhi 50‬

Waathirika wapo Watanzania, Wakenya, Wamarekani na raia wa Canada pamoja na Briton

Taarifa zinadai Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na Mahad Abdulahi Nur(Pichani), Mkurugenzi Mtendaji wa Paradise Holiday Resort ya Bagamoy‬o

Aidha, Mgombea Urais katika Chaguzi zijazo ameuawa pia katika shambulio hilo ambapo kulikuwa na mkusanyiko wa kisiasa katika hoteli hiyo‬

Azam fc kukutana uso kwa uso na Rayon sport….robo fainal …#KAGAME CUP

✍️ Mabingwa watetezi wa Michuano ya CECAFA Kagame Cup na Wawakilishi wa Tanzania 🇹🇿 katika Mashindano hayo, Azam FC Baada ya Kufuzu Robo fainali ya Michuano hii, Sasa inatarajia kukutana na Wenyeji na Mabingwa wa Rwanda 🇷🇼, Rayon Sports..
.
✍️ Jumanne hii ya Julai 16, Miamba hao wanaenda kukutana katika mtanange wao wa tano huku Azam ikiwa Haina Historia ya Ushindi mbele ya Rayon Sports.. Wamekutana Mara moja katika Mchezo wa Kirafiki Mwaka 2017 na Azam FC kupoteza kwa kufungwa 4-2.. Mara tatu Wamekutana katika Mashindano haya ya CECAFA Kagame Cup, Sare Mara moja ya 0-0 Mwaka 2014 na Azam kupigwa game zote mbili, 4-2 (2018) na 3-1 (2011).
#CECAFAKagameCup #KagameCup2019
@Sokawaytz_

Beki kinda wa Kimataifa wa Uholanzi, Matthijs de Ligt muda wowote anatarajia kuwa Mchezaji Mpya wa Juventus

De Ligt kutua Juventus!! ⚪️⚫️
✍️Beki kinda wa Kimataifa wa Uholanzi, Matthijs de Ligt muda wowote anatarajia kuwa Mchezaji Mpya wa Juventus akikamilisha uhamisho wake kutoka ARC Ajax..
✍️Makubaliano ya Jumla tayari wanefikiana baina ya Vilabu viwili Juventus na Ajax… Atasaini Mkataba utakao muweka Turin mpaka June 2024 akipokea €12M kwa Kila msimu..
✍️ Muda wowote Nyota huyo atawasili Italia kukamilisha vipimo vya afya…✍️.
#TransferNewsUpdates

Mshambulaji wa Manchester United raia wa Jamhuri ya Ireland Mipo Odubeko (16) amekataa kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo. .

Mshambulaji wa Manchester United raia wa Jamhuri ya Ireland Mipo Odubeko (16) amekataa kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo. .
.
Kinda huyo mwenye uwezo wa hali ya juu wa kusakata kabumbu alifunga mabao 35 msimu uliopita akiwa na Academy ya klabu hiyo (Mail)

Klabu ya Arsenal imerudi kuwania saini ya beki wa Benfica Ruben Dias (22) ili kurithi mikoba ya Laurent Koscielny anayetajwa kuondoka klabuni hapo.

Klabu ya Arsenal imerudi kuwania saini ya beki wa Benfica Ruben Dias (22) ili kurithi mikoba ya Laurent Koscielny anayetajwa kuondoka klabuni hapo. .
Hata hivyo Arsenal inatarajiwa kukabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa Manchester Utd ambao nao wameonyesha nia ya kumtaka mlinzi huyo (Mail)

Klabu ya Arsenal imesema inataka kulipwa dau la £8.8m endapo kama kuna timu itamhitaji beki wake Laurent Koscielny (33)

Klabu ya Arsenal imesema inataka kulipwa dau la £8.8m endapo kama kuna timu itamhitaji beki wake Laurent Koscielny (33) ambaye alikataa kuondoka na wenzake kuelekea Marekani tayari kwa mechi za maandilizi ya msimu ujao. (London Evening Standard)

Design a site like this with WordPress.com
Get started