
Simba imetangaza kuwaacha wachezaji wake 13, akiwemo mfungaji bora wa Uganda katika fainali za Afcon, Emmanuel Okwi.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori alisema kati ya wachezaji hao, sita wametolewa kwa mkopo na saba wamemaliza mikataba.
“Waliomaliza mikataba klabu haikuhitaji kuendelea nao, isipokuwa Asante Kwasi ambaye mkataba wake unamalizika Novemba.
“Kwasi amepata timu na klabu tumeamua kuachana naye baada ya makubaliano ya pande zote mbili ili akaendelee na maisha mengine,” alisema Magori.
Aliwataja wachezaji wengine walioachwa rasmi kuwa Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi, Nicholaus Gyan, Zana Coulibaly, James Kotei na Salim Mbonde.
Wachezaji waliowatoa kwa mkopo ni Mohamed Ibrahim (Mo), Marcel Kaheza, Mohamed Rashid, Adam Salamba, Paul Bukaba na Abdul Athumani wa timu ya vijana ya