



Rais wa Fc Barcelona Bartomeu akihudhuria mazoezi ya klabu hiyo mapema hapo jana. #barca #fcbarcelona #spain




Rais wa Fc Barcelona Bartomeu akihudhuria mazoezi ya klabu hiyo mapema hapo jana. #barca #fcbarcelona #spain


Unamfahamu vizuri Juma Kaseja Juma?
Yule aliyewalaza njaa Waarab wa Zamalek pale kwenye ardhi yao Cairo baada ya kuokoa mikwaju miwili ya penati.
Ni Kaseja ambaye ndiye kipa wa mwisho kuwapa taji Watanzania baada ya kuiongoza Kilimanjaro Stars kubeba ubingwa wa Kombe la CECAFA Chalenji mwaka 2010 akiwa kama nahodha.
Ni Kaseja, kipa pekee aliyefanikiwa kuzidakia Simba na Yanga kwa mafanikio makubwa katika nyakati tofauti akibeba medali za ubingwa pande zote.
Alikuwa na kila sababu ya kuwemo kwenye kikosi cha Stars. Amechezea timu zote za taifa kuanzia ile ya miaka 17 hadi ya wakubwa.
Amekuwa na msimu bora uliomalizika akicheza jumla ya mechi 24 na KMC kwenye kombe la FA na Ligi Kuu ambapo kati ya hizo, 15 hakuruhusu nyavu zake kutikiswa.
Ndio bingwa wa kucheza mipira ya krosi na penati kuliko kipa yeyote nchini. Wala hajaitwa kwa bahati mbaya kwenye kikosi cha CHAN.
Kama Taifa tumeamua jambo moja kwa pamoja, #TunakanyagaMpakaCHAN |🇹🇿
@kawambwa_jr
@pascal_kabombe
@jamestupatupa
@alikamwe
@giftmacha_official
@karim_boimanda
@charlesabel24
@2official6
@zechicharito1
@yossima_sports
@bill_shankly_1892
@anwarbinde
@fatmalikwata
@baraka_mpenja
@kichunafatma
@Abdulmkeyenge
@boiplusmedia
@bintisuleimani
@zechicharito1
@samuel_.samuel
@paulurio_barcelona
@officialpriscakishamba

MINO RAIOLA MZEE WA DONE DEAL
NA MESHACK MELELE
Nikijua timu inamtaka mchezaji aliye chini yangu, nawafuata nawambia mchezaji huyu anatakiwa na timu saba, nikitoka hapo naenda kwa kila timu hizo saba kuwaambia namna mchezaji wangu anavyohitajika nawashauri wamchukue pia ” Si maneno yangu bali ni maneno ya Mino Raiola.
Mwanadamu anayepiga pesa kupitia kuijaza karatasi nyeupe wino wa mikataba ya wachezaji, ni wakala maarufu wa wachezaji wengi wakubwa ulaya, Zlatan Ibrahimovic pamoja na ubabe wake wote akifika hapa anatulia, anajua huyu ndo alimpatia maisha, amewezesha dili la mchezaji chipukizi Matthis de ligt kwenda Juventus akitokea Ajax , huku yeye akiweka mfukoni euro milioni 10 maisha yanataka nini kwake.
Haikua rahisi kwa yeye kufanikiwa, kupitia maandazi aliyoyauza katika mgahawa wa baba yake ndo siri kubwa kwake kufanikiwa, yalimfanya ajue kuzungumza lugha saba duniani zinazomwezesha kukamilisha dili mbali mbali za wachezaji.
Simu yake iko busy masaa 24 , ikipokea ofa kutoka kwa makocha wa timu mbali kutokana na ubora wa wachezaji walio katika timu yake, Paul pogba, matuidi, Moise kean, Lukaku, Mkhitaryan, Lorenzo Isigne, Marco Veratti wote hawa wako chini yake, anachokifanya ni kuweka simu yake chaji kipindi hichi cha usajili huku pembeni yake akila Baga na soseji.
Amehusika katika dili zilizozalisha zaidi ya paundi milioni 630, anajua kucheza na mahesabu haswa, dili nyingi zikihusisha vilabu vya PSG, Juventus, Ajax, siku zote anaiacha kalamu yake ifanye kazi, ukitaka kumrofisha mwambie mchezaji aliye chini yake si Bora.
Anajua kutetea dili za wachezaji wake, siku aliyoulizwa na mwandishi wa habari anaitwa nani alijibu ” whatever you want, just as long as you pay me” yani vyovyote vile utavyoamua kunita nite ilmradi unanilipa huyo ndo mino raiola mwanadamu anaejua harusu ya pesa ikoje.


– Juventus Imethibitisha Rasmi kukamilisha uhamisho wa Beki wa Kimataifa wa Uholanzi, Matthijs de Ligt akitokea AFC Ajax.
.
– Beki huyo mwenye umri wa Miaka 19, alihusishwa kutakiwa na Manchester United na FC Barcelona, lakini Sasa kasajiliwa na Mabingwa hao wa Italia kwa Mkataba wa Miaka Mitano.
.
– Juventus italipa €75m (£67.8m) Kama dau la uhamisho wa Beki huyo, kwa dau hilo la uhamisho linamfanya De Ligt kuwa Ni Beki ghali zaidi wa muda wote Katika Ligi Kuu ya Nchini Italia..
#transfersUpdates
@Sokawaytz_


OFFICIAL| Klabu ya, Petro Atletico de Luanda ya Nchini Angola Imethibitisha Kukamilisha Usajili wa Mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda 🇷🇼, Jacques Tuyisenge kutoka Katika Klabu ya GOR Mahia ya Nchini Kenya.
.
– Tuyisenge anaondoka GOR Mahia Baada ya kuifungia Magoli 64 Katika Mechi 129 akiwa na jezi ya Klabu hiyo. Miamba hao wa Angola wamemsajili kwa dau la Kshs 15M (Tshs 335m / US $146k).
#TransferNewsUpdates
@Sokawaytz_


– Arsenal yaitwanga Bayern Munich na kukataa udhaifu dhidi yao… Baada ya Ushindi huo The Gunners watarejea Dimbani Julai 21 kukipiga dhidi ya Fiorentina ya Italia, Wakati Bayern Munich wao watakipiga na Real Madrid ya Hispania..
#ICC2019


✍🏻 Ebwana!! Kabadilishwa tenaa! Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” limebadili kwa Mara ya tatu mwamuzi ambaye atachezesha fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika “AFCON” kwa Mwaka huu 2019 Nchini Misri… Kwa Mara ya Kwanza Alitangazwa, Bamlak Tessema kutoka Ethiopia 🇪🇹 na Jana katangazwa mwamuzi Victor Gomes kutoka Afrika Kusini 🇿🇦.
:
✍🏻 Hii leo CAF imetoa taarifa mpya kwamba, Mwamuzi bora wa Mwaka 2017 Barani Afrika, Alioum Sidi Alioum kutoka Cameroon 🇨🇲 ndiye atasimama katikati kuamua Bingwa mpya wa Afrika katika Mtanange utaowakutanisha Algeria 🇩🇿 wakikipiga dhidi ya Senegal 🇸🇳, Mchezo huo unatarajia kupigwa Kesho Ijumaa Julai 19 ndani ya Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
:
✍🏻 Mwamuzi huyo mwenye umri wa Miaka 37, atasaidiwa na Evarist Menkouande na Elvis Guy Ngeugoue wote kutoka Cameroon 🇨🇲…. Fourth Official anatoka Nchini Gabon mwamuzi Maarufu, Eric Arnaud Castane OTOGO na Mwamuzi Msaidizi Namba tatu Ni Waleed Ahmed Ali kutoka Sudan Wakati Kamishina wa Mechi atakokea Nchini Misri, Ahmed Mohamed Megahed Osman…Papa Bakary Gassama kutoka Gambia yeye atakuwa mwamuzi Msaidizi wa Teknolojia ya VAR na Dixon Okello kutoka Uganda 🇺🇬 yeye Ni Afisa wa Ulinzi.
:
✍️ Mechi alizosimama katikati Katika AFCON ya Mwaka huu 2019 Ni pamoja na…Hatua ya Makundi, Misri anashinda 1-0 dhidi ya Zimbabwe na Morocco anashinda 1-0 dhidi ya Ivory Coast. Pia kachezesha Robo fainali, Madagascar anapoteza Mechi kwa 3-0 mbele ya Tunisia..
#TotalAFCON2019 #AFCON2019 #AFCONUpdates
@Sokawaytz_


Ole Gunnar alisema kama watasajili mchezaji mwingine basi kuna uwezekano wakauza mchezaji mwingine kwa mujibu wa mipango ya klabu.
:
Bruno Fernandes anakadiriwa kufikia dau la £50m. Je unadhani nani anapaswa kumpisha kiungo huyu wa Sporting ambaye msimu uliopita aliongoza kwa viungo wote mwenye magoli mengi Ulaya (28).


#DealDone Aliyekuwa mchezaji wa Alliance Fc Rajabu Kibela amejiunga na Dodoma Jiji Fc kwa mkataba wa mwaka mmoja.


#DealDone Ally Ahmed Shiboli amejiunga na Dodoma Jiji Fc akitokea JKT Tanzania kwa mkataba wa mwaka mmoja.