
Wachezaji 26 wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ walioteuliwa na kocha Etienne Ndayiragije wameanza kuripoti kambini leo tayari kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Kenya wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za CHAN utakaopigwa Julai 28, uwanja wa Taifa
Kulingana na taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo, Stars inatarajiwa kuweka kambi kwenye Hotel ya APC, Mbweni kujiandaa na mchezo huo
Wachezaji saba wa Simba ambao wako Afrika Kusini kwenye kambi ya mabingwa hao wa Tanzania Bara, watalazimika kurejea nchini kuungana na wenzao
Nyota wa Simba walioitwa kwenye kikosi cha Stars ni Aishi Manula, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassani Dilunga, Ibrahim Ajib na John Bocco
















