Kiungo wa klabu ya Liverpool na James Milner mwenye umri wa miaka 33 amesema mpaka sasa hajui hatma yake ndani ya klabu hiyo

Kiungo wa klabu ya Liverpool na James Milner mwenye umri wa miaka 33 amesema mpaka sasa hajui hatma yake ndani ya klabu hiyo licha ya kwamba anataka kusalia. (Liverpool Echo)

Klabu ya Beijing Guoan ya China imetoa ofa ya mshahara wa £1m kwa mwezi ili kupata saini ya mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale

Klabu ya Beijing Guoan ya China imetoa ofa ya mshahara wa £1m kwa mwezi ili kupata saini ya mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale ambaye hayupo kwenye mipango ya Zidane msimu huu. (Mirror)

Zana coulibally ..ajiuna na miamba As vita club

OFFICIAL | Aliyekuwa Beki wa Klabu ya Simba SC ya Tanzania 🇹🇿, Zana Coulibally Amewasili Jijini Kinshasa Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa N’djili ( N’djili International Airport) kukamilisha Usajili wake wa kujiunga na Klabu ya AS Vita Club 🇨🇩… Simba SC imeachana na Beki huyo wa Kimataifa wa Ivory Coast..
#TransferNewsUpdates

CUF yavuruga ratiba ya simba day

Kitendo cha Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) kuipanga Simba hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa, kimevuruga ratiba ya timu hiyo kuelekea Tamasha la SIMBA DAY linalofanyika kila mwaka

Simba inapaswa kusafiri kwenda nchini Msumbiji kuumana na USD Songo katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ambao utapigwa kati ya tarehe 09, 10 au 11 mwezi wa nane

Hivyo hakuna uwezekano SIMBA DAY kufanyika August 08 kama lilivyofanyika miaka yote

Hata hivyo msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema Tamasha hilo litafanyika, lakini huenda kutakuwa na mabadiliko ya tarehe

Simba kuanza na US songo ligi yamabingwa africa

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wataanza kampeni ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwa kumenyana na US Songo ya Msumbiji katika mchezo wa hatua ya awali

Simba itaanzia ugenini katika mchezo wa kwanza utakaopigwa kati ya August 09-11 na itamalizia mchezo wa pili uwanja wa Taifa kati ya August 23-25

Kama Simba itafanikiwa kuvuka raundi ya awali, katika raundi ya kwanza itamenyana na mshindi wa mchezo kati ya Platinuma Fc ya Zimbabwe dhidi ya Nyasa Bullets ya Malawi

Ushindi katika hatua hiyo utaipeleka Simba hatua ya makundi

Mwanzo kulikuwa na taarifa kuwa Simba ingeanzia raundi ya kwanza.

Hata hivyo kulingana na droo iliyofanywa na CAF, itacheza kuanzia hatua ya awali

Simba kuwa na viwanja viwili bunju

Achana na kiwanja cha nyasi bandia ambacho kinasubiri kutandikwa nyasi hizo baada ya zoezi la kuweka miundombinu kukamilika

Mabingwa wa nchi Simba, huko Bunju watakuwa na viwanja viwili ambapo wakati huu tayari ujenzi wa kiwanja kingine kitakacho-pandwa nyasi asili unaendelea

Kisima cha maji yatakayotumika kumwagilia kiwanja hicho kimechimbwa na sasa zoezi la kutandaza mbolea linaendelea kabla ya nyasi hizo kupandwa

Uongozi wa Simba umedhamiria kumaliza ujenzi wa viwanja hivyo haraka kwani mradi huo ulipaswa kuwa umekamilika tangu mwezi wa pili

Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu, uwanja huo utakuwa tayari kwa matumizi

Design a site like this with WordPress.com
Get started