

– Herve Renard amejiuzulu kama kocha mkuu wa Morocco baada ya timu hiyo kutolewa mapema katika Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika…Morocco ni mojawapo wa timu zilizopigiwa upatu kabla ya kuanza kwa mahsindano hayo Misri 2019 lakini ilishindwa kufanya vema baada ya kutolewa kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Benin katika hatua ya 16 Bora.
.
– Renard, raia wa Ufaransa amewahi kushinda mataji mawili ya AFCON akizifundisha timu za taifa za Zambia Mwaka 2012 na Ivory Coast mnamo mwaka 2015, Kocha huyo alikiongoza kikosi cha Morocco tangu Februari 2016, na Pia Renard aliitoa Morocco kutoka nafasi ya 81 katika orodha ya Viwango vya Ubora wa soka vya FIFA Duniani hadi katika nafasi ya 47.
.
– Aliyewahi kuwa kocha Mkuu wa Klabu ya PSG, Laurent Blanc ameripotiwa kuwepo Katika Mazungumzo na Shirikisho la Soka Nchini Morocco 🇲🇦 kwa ajili ya kuchukua Mikoba hiyo iliyo wazi kwasasa..
#Updates #transfersUpdates

















