Klabu ya Everton ipo mbioni kumsajili Mshambuliaji wao wa Kimataifa wa Italia, Moise Kean. .

– Klabu ya Everton ipo kwenye Mazungumzo na klabu ya Juventus kumsajili Mshambuliaji wao wa Kimataifa wa Italia, Moise Kean.
.
– Kean ambaye ana Umri wa miaka 19, Klabu ya Juventus imemuwekea thamani ya kiasi cha €40M (£36M/$45m) na klabu hiyo ya Juventus Katika Makubaliano yao, inataka Kipengele cha kumnunua tena kijumuishwe kwenye dili hilo.
.
– The Toffees, bado wanasaka Mshambuliaji Ambaye atakuja kuziba pengo la kinda wao, Ademola Lookman aliyejiunga na Klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani..
#TransferNewsUpdates
@Sokawaytz_

Mwinyi Zahera ) Awasili Mkoani Morogoro

– Mkuu wake Klabu ya Yanga SC, Mwinyi Zahera jioni hii Amewasili Mkoani Morogoro ambako ndipo Kikosi Cha Klabu hiyo kimepiga kambi ya Maandalizi ya Msimu Mpya was ligi kuu na Mashindano ya Kimataifa!..
.
– Zahera Alikuwa nyumbani kwake Nchini Ufaransa Katika likizo ya Siku 15 Baada ya Kumalizika kwa Michuano ya AFCON huku yeye akiwa Kocha Msaidizi was DR Congo 🇨🇩… Yanga kwasasa inajiandaa na Mchezo was Klabu Bingwa Barani Afrika dhidi ya Mabingwa wa Botswana, Township Rollers.
#TPLUpdates

FULL-TIME | Reading 3 – 4 Chelsea

.

.FULL-TIME | Reading 3 – 4 Chelsea
[ Josh Baret, Michael Morrison, Sam Baldock | Ross Barkley ⚽, Kennedy ⚽, Mason Mount ⚽⚽ ]
:
– Mitambo ya Chelsea imekubali, Magoli mawili ya bwana mdogo Mason Mount akitokea Benchi anaipatia Ushindi The Blues na yeye mwenyewe kujihakikishia kusalia klabuni hapo…. JUMATANO hii @chelseafc v Red Bull.
#FriendMatch #chelseafc #chelsea

Sadio Mane ajenga shule huko nchini kwao Senegal

– Mshambuliaji wa klabu ya @liverpoolfc, Sadio Mane anajenga shule huko nchini kwao Senegal katika kijiji cha Bambali…. Mane pia Alichangia Pesa za Matibabu kwa wagonjwa waliopo hospitali za mtaa huo, amejenga vituo vya starehe na vifaa vya mpira kwa timu ndogo ndogo za huko Kijijini kwao, Pia Amewasaidia Wananchi wengine wenye kipato Cha Chini… Haya yote huwa anafanya Kila Baada ya Kumalizika kwa Msimu akiwa mapumzikoni kwao Senegal!.. 😍
#updates #liverpool
@Sokawaytz_

FULL-TIME | Arsenal 1 – 2 Lyon [ P.A Aubameyang ⚽ | Moussa Dembele ⚽⚽ ] :

FULL-TIME | Arsenal 1 – 2 Lyon
[ P.A Aubameyang ⚽ | Moussa Dembele ⚽⚽ ]
:
– Arsenal wanaangukia “Pua” Mchezo wa fainali ya Emirates Cup Mbele ya Lyon ya Ufaransa iliyoibuka na Ubingwa, Baada ya kuongoza Mpaka Mapumziko, Kipindi Cha Pili Dembele akitokea Benchi anakuja kugeuza ubao!… Arsenal ilikuwa Mabingwa wa Kombe Hili Mara Mbili mfululizo, na Sasa wamevuliwa Ubingwa 🙄🙄..
#Arsenal #lyon #ol #Updates
@Sokawaytz_

Kocha Mkuu wa Klabu ya Arsenal, Unai Emery, ametoa Taarifa juu ya Majeraha , Alex Lacazette

– Kocha Mkuu wa Klabu ya Arsenal, Unai Emery, ametoa Taarifa fupi juu ya Majeraha ya Mshambuliaji was Klabu yake, Alex Lacazette aliyopata hii leo.
🗣️ “Daktari aliniambia atamfanyia vipimo kesho”.
Emery alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya mchezo.
🗣️ “Ni majeraha kwenye kifundo chake, atafanyiwa tathmini kwa siku chache zijazo – sio majeraha mabaya Sana”.
.
– Mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Ufaransa, alipata Majeraha hayo Dakika ya 12 tu ya Mchezo huo wa fainali ya Emirates Cup dhidi timu yake ya zamay, Lyon… Arsenal ilipoteza Mchezo huo kwa kufungwa 2-1.
#Arsenal #Updates
@Sokawaytz_

Mkurugenzi mtendaji wa Klabu ya Arsenal, Vinai Venkatesham amekanusha madai kuwa klabu hiyo ina bajeti ya £40m tu

Mkurugenzi mtendaji wa Klabu ya Arsenal, Vinai Venkatesham amekanusha madai kuwa klabu hiyo ina bajeti ya £40m tu ya kutumia kufanya Usajili msimu huu wa joto.
.
– Venkatesham aliwaambia Mashabiki wa Klabu hiyo Katika Kipindi Cha Maswali na Majibu ya papo kwa papo:
“Sitambui takwimu hii ya pauni 40m, nimeisoma sana Taarifa hiyo. Hiyo haitokei kwetu, hiyo haiji kutokea kwa klabu yetu”.
.
– The Gunners kwasasa wapo Katika Mazungumzo na Muwakilishi wa Winga wa Kimataifa wa Ivory Coast, Nicholas Pepé juu ya kujiunga na Klabu hiyo kwa dau la uhamisho wa €80m kutoka Lille ambayo wamefikia Makubaliano na Arsenal..
#EPLTransfersUpdates #transfersUpdates

Design a site like this with WordPress.com
Get started