BALAA LA NICOLAS PEPE, BUNDUKI MPYA YA ARSENAL?? •

JE UNAFAHAMU BALAA LA NICOLAS PEPE, BUNDUKI MPYA YA ARSENAL??

Achana na mafundi wote unaowajua wewe kwenye ligi bora tano za Ulaya. Weka pembeni Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Eden Hazard, na Mohamed Salah.

Huyu Mshika bunduki mpya wa Arsenal ni moto wa kuotea mbali. Cheki hizi takwimu zake

Katika ligi tano bora za Ulaya, Nicolas Pepe ndio mchezaji pekee aliepiga mashuti takribani 100+ yaliyolenga lango. (MOST SHOTS ON TARGET)
– Arsenal wamelamba dume.

Katika majaribio yake ya kuwapita mabeki, amefanya vizuri kuliko mchezaji yeyote katika ligi tano bora za ulaya. Amefanya hvyo mara 100+. (MOST TAKE-ONS). Arsenal itarudi UEFA.

Ni winga pekee katika ligi tano bora za ulaya ku-win mpira na kuanzisha mashambulizi kutoka kwa mpinzani wake. Amefanya hvyo mara 100+.

TAKWIMU HAZIDANGANYI.

JE TUTEGEMEE ARSENAL KUCHUKUA UBINGWA WA EPL, UEFA CHAMPIONS LEAGUE NA FA CUP Msimu huu

Herve Renard Rasmi Amethibitisha kuwa Amesaini Mkataba wa kuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Saudi Arabia 🇸🇦..

Herve Renard Rasmi Amethibitisha kuwa Amesaini Mkataba wa kuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Saudi Arabia 🇸🇦..
.
– Kocha huyo Raia wa Ufaransa mwenye umri wa Miaka 50, amezifundisha timu Nne tofauti za taifa, Akitwaa Ubingwa wa Afrika Mara Mbili na timu Mbili tofauti akiweka Rekodi ya kuwa Kocha Pekee Kufikia mafanikio hayo..
Angola 🇦🇴 Ivory Coast 🇨🇮 Morocco 🇲🇦 Zambia 🇿🇲
#TransferNewsUpdates

2/2: KUTOKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI NA KLABU YA @simbasctanzania.

2/2: KUTOKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI NA KLABU YA @simbasctanzania.
:
“Siku ya tarehe 5 / Agosti saa 9:30 alasiri kutakuwa na mkutano na wanahabari, saa 10:30 Simba watafanya mazoezi Uwanja wa Taifa na saa 11:30 jioni watawapisha wenzao. Siku hiyo hiyo timu ya Simba Queens itatembelea Shule ya Makongo kuwapa hamasa wanafunzi”- CEO Magori.
.
“Siku ya Simba Day tunataka nchi nzima tuvae nguo nyekundu, na tunaongea na wadhamini kwenye viwanja mikoani tuweke screen kubwa ili mashabiki waangalie mpira pamoja”- CEO Magori..
.
“Milango itafunguliwa saa 4 au 5 asubuhi, kutakuwa na wasanii ikiwepo bendi ya Twanga Pepeta. Tutakuwa na mechi tatu, ya kwanza Simba Queens wakiwa wametoka Ujerumani, itafata Simba U20, ambayo kwasasa ina wachezaji bora sana. ”- CEO Magori.
.
“Saa 10:30 jioni tutaanza kutambulisha wachezaji wapya, na mechi itaanza saa 11:30 ili hata wanaotoka kazini wapate nafasi. Siku ya tarehe 7/ Agosti tutakuwa na chakula cha usiku na wageni wetu Power Dynamos kwenye hoteli ya Serena kuwashukuru na kuwaaga”- CEO Magori.
.
“Mechi yetu ya Msumbiji ya Ligi ya Mabingwa itakuwa tarehe 10/ Agosti, tunafanya utaratibu kwenda na ndege kucheza baada ya mchezo tunarudi. Tungeweza kufanya Simba Day tarehe 3 lakini tungewakosa wachezaji wetu wa timu ya Taifa, hatufanyi nusu nusu”- CEO Magori.
.
“Kila mwaka tuna kauli mbiu ya Simba Day wiki hii inaitwa SPORTPESA SIMBA WEEK. Matarajio yetu hili jambo litakuwa endelevu kwa miaka yote ya Simba SC. Jambo jema linaigwa, ni vyema kuiga jambo zuri”- Haji Manara.
.
“Kaulimbiu yetu itakuwa ni IGA UFE, THIS IS NEXT LEVEL. Tutakuwa na kaulimbiu hiyo kwa Wanasimba wote kila ambacho tutapost tutumie hiyo.”- Haji Manara.
.
“Simba kujaza uwanja hakutegemei siku iwe weekend au katikati ya wiki na bahati nzuri Wanasimba siku hiyo wanakuja kumuona Kahata, Shiboub, Wabrazil na wengine wengi”- Haji Manara.
#SimbaSC #Updates

Yanga yaweka rekodi mpya……wiki ya wananchi

Follow #yanga_4g
Yanga imefanikiwa kufanya kile kilichotarajiwa baada ya wapenzi, wanachama na mashabiki wake kuitikia wito wa kujitolea kufanya shughuli mbalimbali za kijamii katika wiki ya Wananchi iliyoanza juzi

Wiki ya Wananchi imekuwa na manufaa makubwa kwa jamii kwani shughuli zinazofanywa zinanufaisha jamii yote bila ya kujali ikikadi

Kwa miaka mingi watani zao Simba wamekuwa wakifanya tukio hili lakini halikubeba sura ya kitaifa kama linavyofanywa na Yanga sasa

Leo hii mkoa wowote ukifika lazima utakuta kuna shughuli za kijamii zinafanywa na Wanayanga

Kinachofanywa sasa na Wanayanga kinadhihirisha msemo kuwa timu hiyo ni ya Wananchi

Na pengine ule mjadala wa kati ya Yanga na Simba ni timu ipi yenye mashabiki wengi nchini unaweza ukapata majibu kupitia hiki kinachoendelea sasa

Aidha huenda August 04 historia ikaandikwa uwanja wa Taifa kwa idadi kubwa ya mashabiki kujitokeza kushuhudia siku ya kilele cha wiki hii ambapo siku hiyo Yanga itatambulisha kikosi chake kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kariobangi Sharks kutoka Kenya
.
.
#Usifositufanane

Makamu wa Rais Zanzibar akutana na viongozi wa Yanga

*

Makamu wa Rais Zanzibar akutana na viongozi wa Yanga*

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameunga mkono mfumo wa Klabu Maarufu ya Mchezo wa soka ya #YangaSC wa kuanzisha Miradi ya kujitegemea katika azma ya kuiondoshea na utegemezi Klabu hiyo.

Alisema tabia ya kutembeza kutegemea Mtu binafsi mara zote huleta migogoro baina ya Wanachama na Viongozi na hatimae uwajibikaji au malengo ya Klabu hukosekana na kubakisha huzuni kwa Wanachana pamoja na Wapenzi wa Klabu.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo Ofisini kwake Vuga-Zanzibar wakati akizungumza na Uongozi wa Klabu ya Dar es salaam Young African ambao ulikuwepo Zanzibar kushiriki uzinduzi wa Shughuli ya Wiki ya Mwananchi ya kuchangia Yanga.

Balozi Seif alisema kwa kuwa Klabu hiyo ina dhamira sahihi ya kuendeleza Wachezaji wake katika azma njema ya kuimarisha ustawi wao yeye binafsi pamoja na Serikali iko tayari kusaidia nguvu zake ili kuona malengo iliyojipangia yanafanikiwa vizuri.

Akizungumzia uimarishaji wa Wachezaji Vijana kwenye Klabu hiyo Kongwe Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliukumbusha Uongozi huo wa Yanga kuzingatia suala hilo ambalo ni muhimu kwa Taasisi yoyote ya Michezo.

Mapema Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dr. Mshindo Msolla alimueleza Balozi Seif kwamba Uongzi Mpya wa Klabu hiyo umelenga kuyasimamia mambo matano makubwa yatakayosaidia kuipeleka Klabu hiyo katika mafanikio makubwa.

Dr. Msolla aliyataja mambo hayo kuwa ni pamoja na kuleta Umoja katika kuipeleka Timu kwa Wanachama, kuimarisha Miradi iliyopo Klabuni na kubuni mengine mipya, uwajibikaji na Utawala Bora pamoja na kuiendeleza miradi iliyopo Visiwani Zanzibar.

Alisema katika mfumo huo Mpya utakaoanzishwa, Wanachama watakuwa na uwezo wa kujua mapato na matumizi ya Klabu kupitia Mtandao wa Kisasa wa Habari na Mawasiliano utakaokwenda sambamba na kuongeza Wanachama kutoka 17,000 hadi kufikia Milioni 1,000,000.

Mwenyekiti alisisitiza kwamba mpango maalum utaandaliwa katika matumizi sahihi ya Nembo ya Klabu ambapo itatolewa tenda na Kampuni itakayoshindaitakuwa na haki ya kuuza Jazi zenye Rangi ya Klabu na kila Jezi moja kutakuwa na asilimia ya Klabu.

Credit: Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Zanzibar.

Michy Batshuayi anatarajia kusalia Chelsea msimu

👉🏻 Michy Batshuayi anatarajia kusalia Chelsea msimu huu na kupiganiana nafasi dhidi ya Tammy Abraham na Olivier Giroud katika kikosi Cha kwanza kama mshambuliaji mkuu wa kocha, Frank Lampard.
.
👉🏻 Chelsea wanatumikia marufuku yao ya kusajili Wachezaji kwa dirisha hili na linalokuja, lakini hawateteleki kwa kiasi kuhusu Hilo Ni Baada ya kuwa na rundo la Wachezaji Vijana waliowekezwa na Klabu hiyo, ndani ya Academy yao na wengine walitolewa kwa mkopo Vilabu Mbalimbali takribani 40+… The blues imefanya Usajili wake kwa Wachezaji wawili tu, Christian Pulisic na Kiungo, Matteo Kovacic Ambaye alicheza kwa mkopo klabuni hapo hivyo ikawa ruksa kumsajili na Pulisic alisajiliwa Mwezi January kabla ya kufungo kuwakuta.
.
👉🏻 Tammy Abraham amerejea kutoka kwa mkopo Aston Villa na Michy Batshuayi amerejea kutoka kwa mkopo Crystal Palace… Kinda mwingine Mason Mount karejea kutoka kwa mkopo Derby County na ana uhakika kusalia na The Blues msimu huu Baada ya kufanya vema Katika Mechi za Pre-Seasons..
#EPLUpdates
@Sokawaytz_

KUTOKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI NA KLABU YA @simbasctanzania.

1/2: KUTOKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI NA KLABU YA @simbasctanzania.
.
CO; Jamani leo nitaongea. Nikimaliza ataongea Haji mwisho wadhamini wetu. Kikubwa leo tumewaita hapa juu ya Simba wiki. Huu ni mwaka wa kumi kila mwaka tunafanya matamasha haya. Hili la mwaka huu Haji ataongea. Wiki hii itaanza 31/7/2019 wachezaji watarejea toka south Africa. Siku hiyo hiyo tutasaini mkataba na mdhamini wa jezi mkataba ni wa miaka miwili. Muda utakuwa saa tano hapahapa Serena. Tutaweka wazi kila kitu. Siku hiyo hiyo saa sita usiku Simba ita lounge jezi mpya ya msimu ujao. Jezi zote tatu. Tarehe moja sasa jezi zitaanza kuuzwa nchi nzima na wakati tuna saini tutawajuza maduka gani yatauza jezi nchi nzima.
.
Tarehe hiyo hiyo moja tutakuwa na press hapa hapa tuta lounge Kadi mpya za clab ambazo ni za electronic cards. Tutaeleza kila kitu kuhusu hizo kadi. Fans card ndio hii card baadae zitamuwezesha mwanachama kujiunga. Siku hiyo hiyo tutaanza kuuza card za vingilio. Tutakuwa na platinum za aina mbili. 150,000 na 100,000.
.
Tarehe mbili sports pesa watatembelea watoto yatima. Simba itatembelea Hospitali ya Ocean road. Tunawaomba wana Simba tarehe tatu hiyo nchi nzima wafanye tendo hili la kuchagua hospitali na kuwajulia hali wagonjwa saa tatu asubuhi. Tunampango wa kuchangia damu na tutawajulisha vituo vikubwa. Wenzetu wafanye hivyo hospitali kubwa. Siku hiyo ya tarehe tatu tutazindua wimbo wa timu. Bado huo wimbo upo unapikwa hadi sasa.
.
“Tarehe 03/ Agosti nchi yote Wanasimba wote nchini twendeni mahospitali tukawasaidie ambao hawana uwezo. Tunaongea pia na watu wa damu hiyo siku tukatoe Damu”- CEO Magori.
.
“Tarehe 3/ Agosti tuna wimbo ambao ukiimbwa unamgusa kila mtu kuanzia mchezaji, shabiki na kiongozi. Tutaanza mazoezi mapema ili ukipigwa tarehe 6 watu 60,000 tukiuimba wimbo huo”- CEO Magori.
.
“Tarehe 4/ Agosti kwa watakaonunua tiketi za Platinum na Platinum Plus watapiga picha na wachezaji wakiwa wamevaa jezi za mechi. Hii inaitwa Photoshoot with Stars”- CEO Magori..
.
“Tarehe 4/ Agosti pia wachezaji watatembelea vituo vya watoto yatima ili kutoa misaada, lakini pia siku hiyo tutaipokea Power Dynamos ikitokea Kitwe, Zambia”- CEO Magori..
#Updates
#SimbaSC

Design a site like this with WordPress.com
Get started