




🔙 SIKU KAMA YA LEO: Mnamo Julai 30, 2010, Klabu ya Real Madrid Ilithibitisha kukamilisha uhamisho wa Kiungo wa Kimataifa wa Ujerumani, Sami Khedira kwa ada ya uhamisho isiyojulikan kutoka VFB Stuttgart ya kwao Ujerumani, na kusaini mkataba hadi mwaka 2015…
.
✍🏻 Khedira alicheza kwa Mara ya kwanza Agosti 13 kwenye mchezo wa Kirafiki dhidi ya Bayern Munich, ambayo Real Madrid ilishinda 4-2 kwa Mikwaju ya Penati. Game yake ya kwanza kabisa ya ligi ya Laliga ilikuja siku kumi na sita baadaye, katika mchezo uliomalizika kwa 0-0 dhidi ya Mallorca.. Alicheza mechi 40 katika msimu wake wa kwanza nchini Uhispania na alishinda Ubingwa wa kwanza na Klabu mnamo Aprili 20, 2011 wakati timu yake ilipotwaa kombe la Copa del Rey dhidi ya wapinzani wao wa El Clásico, Klabu ya FC Barcelona.
.
✍🏻 Alifunga bao lake la kwanza la Kimashindano akiwa Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa, mnamo Oktoba 18, 2011 dhidi ya Olympique Lyonnais… Alifunga bao lake la kwanza la Copa del Rey dhidi ya Málaga katika ushindi wa 3-2 nyumbani wakati Real Madrid walipofungwa Ugenini 0-2, na bao lake la kwanza la ligi dhidi ya RCD Espanyol katika ushindi wa 5-0 nyumbani… Mnamo Aprili 21, 2012, Khedira alifunga bao lake la pili la ligi, dhidi ya Barcelona; goli hilo lilikuwa la 108 la Real Madrid kwa msimu huo wa ligi, walivunja rekodi yao katika La Liga ya kufunga Magoli 107 iliyowekwa na wao msimu wa 1989-90… Alishinda Kila Kombe Aliloshiriki na Klabu hiyo ya Real Madrid..
La Liga: 🏆
Copa del Rey: 🏆🏆
Supercopa de España: 🏆
UEFA Champions League: 🏆
UEFA Super Cup: 🏆
FIFA Club World Cup: 🏆
:
Mnamo Juni 8, 2015, Baada ya Kumalizika kwa Mkataba wake Santiago Bernabeu, Mabingwa wa Italia, Juventus walitangaza kwamba Khedira amesaini mkataba wa miaka minne kwa uhamisho wa bure… Mpaka hii leo kadumu na vibibi hivyo vya Turin!.
#tbt❤️ #tbtfootball #Juventus #RealMadrid
@Sokawaytz_