Kauli ya zlatani wakati akionfoka LA Galaxy

#JichoLaMwewe • Rudini mkaangalie BaseBall 🤔
.
✍️ Kipindi Zlatan Ibrahimovic A.KA. IbraCadabra anaondoka Marekani kunako klabu ya LA Galaxy alisema maneno ambayo yalionekana kama ni dharau kwa mashabiki wa Galaxy, kwamba yeye anaondoka basi mashabiki warudi kuangalia #BaseBall 🤔, akiwa na maana ya kwamba mashabiki walikuwa wakijaa uwanjani kumtazama yeye tu, Sasa #JichoLaMwewe limetupa jicho lake na kufikiria Je..!! Zlatan siku akitaka kuondoka AC Milan timu yake mpya kwa sasa atawaambia warudi kuangalia nini “BaseBall” au ? 🤔 .
.
✍️ Katika mechi 5 alizocheza hadi hivi sasa akiwa na AC Milan ameingia kambani mara 2.
.
#bakinasisi__ #NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

Ronaldo aweka rekodi mpya

#Cr7Updates • Mechi 10 Za Mwisho .
.
✍️ Katika mechi 10 za mwisho za ligi (Serie A) alizocheza Christiano Ronaldo ikiwapo na ya jana dhidi ya Fiorentina, Ronaldo amefunga mechi zote mfululizo. .
.

* ⚽️
* ⚽️
* ⚽️⚽️
* ⚽️
* ⚽️⚽️⚽️🅰️
* ⚽️
* ⚽️⚽️
* ⚽️
* ⚽️⚽️
.
#bakinasisi__ #NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

⛹Dondoo za soka na Dominick Salamba ⛹

.
💥Yanga yaendelea kujiimarisha #vpl yaitandika Mtibwa taifa,Azam na Mbeya City hakuna mbabe,zatoshana nguvu huko Samora Iringa..
.
💥Man City yapoteana kwa Spars 2-0, Mashuti 15 kwenye tageti bila goli,Morinho atamba asema mpira magoli….
.
💥Inter Millan yaichapa Udinese 2-0 huko kwenye #serieA Lukaku hakamatiki,anatupia tu…
.
💥Barcelona yaishushia kipigo Levante kwenye #laliga yaichapa 2-1, Ansu Fati aibuka shujaa ….
.
💥Pochetino aendelea kuhusishwa na Manchester United,imefahamika anaweza kupewa kazi kwenye majira ya kiangazi….
.
💥Bruno Fernandez alisafiri mpaka ureno kuangalia mechi ya timu yake ya zamani,Sporting ikicheza wikiendi hii,hiyo ni baada ya kuitumikia united dhidi ya Wolves….
.
💥Ansu Fati ndiye mchezaji mdogo zaidi kuwahi kufunga magoli mawili kwenye mchezo mmoja wa #laliga anaweka historia yake ndani ligi hiyo pendwa…
.
💥Kwenye #vpl Ndanda,Singida utd zipo mkiani mwa msimamo,zitaendelea kubaki huko na hatimaye kushuka? muda utatuambia…
.
#bakinasisi__ #njookwetu #TupoNawePaleUlipo

Operesheni Matata Ya Juventus. Wataweza Kweli ?

.
✍️ Taarifa kutoka Italy kwa Kibibi kizee cha Turini Juventus zinadai kuwa imetemga kitita cha Pauni 150 milioni kwa ajili ya kumng’o beki kisiki wa Liverpool Van Dijk na kumvuta kwao katika dirisha kubwa la usajili, huku pia kibibi hiko kikipanga kutumia kitita kama hicho kwa ajili ya kiungo Mashetani wekundu Paulo Pogba. . .
.
✍️ Klabu hiyo inaami kuwa endapo kama ikipata huduma za wakali hao wawili, basi kikosi chao kitakuwa kimekamilika kubeba taji hilo la Ulaya.
.
Unauonaje huu mpango wa Juventus?

.

Kona Ya kiUfundi Yanga Vs Mtibwa

#…
.
1. Ilikuwa mechi nzuri sana ,ilitawaliwa na mbinu zaidi,kila kocha alikuja na mbinu ambazo zilimuweka sehemu salama zaidi,hata kwa wale wasiojua ufundi sana naamini wamefurahia mechi…
.
2. Mtibwa walikuja na 4:1:3:2 hii iliwapa sana wakati mgumu yanga,pamoja na kuwa na viungo watatu wabunifu Riphat,Ally Makarani pamoja na Salum Kihimbwa lakini bado waliubana uwanja muda mwingi wa mchezo jambo lililoipa Yanga wakati mgumu kupitia kati…
.
3.Yanga walikuja na 4:2:3:1 mwanzoni iliwapa shida sana kufika kwenye final third yao,hii ilitokana na ubora wa Ally Makarani,kuna wakati viungo wa Yanga walilazimika kila mmoja kumtolea macho,aliwavuruga sana….
.
4.Yanga wanafaidika sana na uwepo wa Niyonzima kwenye eneo la chini,timu inakuwa na utulivu mno,lakini wanapata hasara kubwa kwa kukosekana kwa kiungo huyo maestro kwenye eneo la juu,nyuma ya washambuliaji,mtu wa namna ya Niyonzima bado anahitajika sana kwenye eneo la ubunifu….
.
5.Humud 🙌 alivyocheza leo ndivyo hasa anavyopaswa kucheza kiungo mkabaji,lazima awe na roho mbaya,nadhani Morrison anaweza kutusimulia zaidi ubora wake,anafika, anaintercept,anaanzisha mashambulizi yani alikuwa full package…
.
6. Balama anahitaji kukomaa zaidi,benchi la ufundi la Yanga limeamini kuwa Kipenseli ndiye anayeweza kuwapa huduma ya Niyonzima,bado anahitaji kuboreka zaidi,,utaona dakika ya 62,Balama aliupata mpira,alichotakiwa ni kuwasaprise Mtibwa kwa kufanya counter boxing badala yake yeye alimpa mpira ule Niyonzima,kisha niyonzima akamuonesha kuwa hakupaswa kumpasia mpira ule,alichokifanya Niyo ni kuuwahisha kwa Molinga lakini akiwa tayari amechelewa,kama Balama angeuwahisha ule mpira basi pengine Yanga wangeweza kupata goli…
.
7.Kuingia kwa Ditram Nchimbi kulitosha kuwaonesha benchi la ufundi la Yanga kuwa halipaswi kumtumia Molinga peke yake,wanamtaabisha bure,Molinga anavitu lakini hakuna matumizi sahihi ya energy yake….
.
8. Morrison karibi ligi kuu Tanzania Bara,hawa wamanyema wanagonga sana,Yanga wakipata plani nzuri ya kukutumia utawanufaisha sana..
.
NB: Kona hii kwa leo inawapa 👊 Molinga na Humud,walikuwa bora sana leo….
.
.
#bakinasisi__ #njookwetu #TupoNawePaleUlipo

Mambo 10 nilioyaona Yanga Vs Mtibwa

1: Mechi ya Mbinu🙌 4-2-3-1 ya Luc Aymael dhidi ya 4-1-4-1 ya Katwila. Tofauti ya hii mechi ilikua nguvu, kasi na pasi sukari ya Ditram Nchimbi
.
.
2: Mtibwa walikua bora walipokua na mpira, wakawa dhaifu mno bila mpira. Kama si uwezo wa Humud, kwenye kuwapress viungo wa Yanga, Mtibwa ingekuwa kwenye madhara makubwa mno
.
.
3: Yanga wamebadilika sana kimuundo. Build up wanafanya watu watatu mpaka wanne. Top level kabisa hii🙌 Changamoto kubwa waliobaki nayo ni kwenye ‘penetration phase’. Bado movement za mastraika hazijakua bora kupokea pasi bora za viungo .
.
4: Shomari Kibwana🙌 Dakika 90 bora sana kutoka kwake👏 Alimuweka Morrison kwenye mfuko wa kushoto, mfuko wa kulia, akatoa silaha zake kuishambulia ngome ya Jafari Mohamed

4: Ubora wa Jafari kimbinu kwenye nidhamu ya kukaba ulimpa wakati mgumu Kihimbwa kukimbia kwenye nafasi, lakini Jafari aliwanyima Yanga faida ya Morisson kukabwa na watu wawili

5: Humud🙌 Mechi bora sana kwake. One of the best Holding Midfielder wa kisasa kwenye Ligi yetu kwa sasa. Anakuwepo kuanzisha build up, anakuwepo kupress timu inapokosa mpira. Amenikosha sana👏

6: Makapu🙌 Aisee. Inavutia kumtazama Makapu huyu. Amebadilika mno. Timing zake kuwania mpira zimeimarika mno. Utulivu umerejea. Bila shaka Lamine Moro ana mchango kwenye mabadiliko haya kama beki kiongozi wa Yanga

7: Kama Katwila angekua na uthubutu mapema wa kuanza na ‘double striker’, pengine angeikamata Yanga mahala pabaya. Ali Makarani hakumpa msaaa mzuri Riphat Msuya, kipindi cha kwanza

8: Leo Nimeona talent mpya🙌 ni yule dogo namba 21 wa Mtibwa.. Somebody Omari Hassan. That Kid is fantastic aisee🙌 Mguu wake wa kushoto una mengi ambayo bado hajatuonyesha, acha niendelee kumsubiri

9: Molinga Falcao👏 Tofauti yake na Yikpe ni kunusa hatari kwenye eneo la mwisho. Nje ya hapo, Tariq Seif anaweza kuja kuwaweka wote benchi siku akirejea uwanjani

10: Niyonzima Haruna, Papy Tshishimbi ndio roho ya plan ya Luc Aymael. Kuimaliza Yanga ni kuimaliza ile nafasi anayoachwa Niyonzima akiwa na mpira

Nb: Alichofanikiwa kupanda leo ni basi la timu tu😀

Design a site like this with WordPress.com
Get started