Klabu ya Manchester City imefufua tena mazungumzo na Juventus ili kuinasa saini ya beki wa kulia Mreno João Cancelo (20) .

Klabu ya Manchester City imefufua tena mazungumzo na Juventus ili kuinasa saini ya beki wa kulia Mreno João Cancelo (20)
.
Man City bado wanatarajia kumjuisha mlinzi wao Danilo ili kufanikisha dili hilo kama msimamo wao ulivyokuwa awali lakini Juventus wao wanataka dau la €60M bila kuhusisha mchezaji yeyote ili kumruhusu mlinzi huyo

Klabu ya @simbasctanzania imeingia mkataba na benki ya Equity

Klabu ya @simbasctanzania imeingia mkataba na benki ya Equity ambao utawezesha benki hiyo kusimamia mradi wa kadi mpya za wanachama na mashabiki ambazo zitaitwa Simba Card.
.
Kadi hizo zitatumiwa na wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuweka akiba ye pesa na kutoa pindi wanapotaka kutumia, lakini pia kulipa ada ya kila mwaka, kununua tiketi za kuingia mpirani, na kupata punguzo la mpaka 10% kwenye maduka makubwa ambayo watashirikiana nayo.
.
Faida kubwa kwa klabu katika kadi hizo ni makato yanayopatikana wakati wa kufungua akaunti, kukusanya ada kisasa na mara moja kwa mwaka, na kupata takwimu sahihi za mashabiki iwapo kila shabiki atafungua akaunti.
.
Kadi hizo zitaanza kutolewa Septemba mosi mwaka huu kwa kuwabadilishia kadi wanachama wa sasa na baadae litaendelea kwa wanachama wapya na mashabiki. #SportPesaSimbaWeek #SimbaSC

Arsenal Imethibitisha Rasmi kukamilisha uhamisho wa winga, Nicolas Pepe

OFFICIAL | Arsenal Imethibitisha Rasmi kukamilisha uhamisho wa winga, Nicolas Pepe kutoka Klabu ya Lille kwa dau la Rekodi ya uhamisho wa Klabu, £72m.
.
– Nyota huyo wa Kimataifa wa Ivory Coast anaekuwa Ni Mchezaji wa Nne kusajiliwa na Arsenal Msimu huu, Amesaini Mkataba wa Miaka Mitano kuwatumikia Miamba hao wa Emirates!..
#EPLTransfersUpdates
@Sokawaytz_

Klabu ya Al Ittihad Alexandria Club Imethibitisha ..ukamilisha Usajili waKEmmanuel Okwi

#BREAKING
Klabu ya Al Ittihad Alexandria Club Imethibitisha Kukamilisha Usajili wa Mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi..
.
– Okwi Ambaye Alikuwa Ni Mchezaji wa Mabingwa wa Tanzania, Klabu ya Simba SC, Amejiunga na Klabu hiyo ya Ligi Kuu Nchini Misri kwa Mkataba wa Miaka Miwili Kama Mchezaji huru!..
#TransferNewsUpdates
@Sokawaytz_

Tottenham imeingia Katika mbio za kuwania saini ya Kiungo wa Kimataifa wa Ureno, Bruno Fernandes

BREAKING NEWS….
Tottenham imeingia Katika mbio za kuwania saini ya Kiungo wa Kimataifa wa Ureno, Bruno Fernandes kutoka Klabu ya Sporting Lisbon… Wameripoti @skysports.
.
– Kwa mujibu wa Ripoti Ni kwamba hii leo Muwakilishi wa Klabu ya Tottenham Amewasili Jijini Lisbon kufanya Mazungumzo na Klabu ya Sporting kuhusu uhamisho wa Mchezaji huyo… Manchester United Pia Ni miongoni mwa Vilabu vinavyomuhitaji Nyota huyo…
#TransferNewsUpdates
@Sokawaytz_

Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Etienne Ndayiragije amefanya mabadiliko madogo

Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Etienne Ndayiragije amefanya mabadiliko madogo katika kikosi kutokana na baadhi ya wachezaji kuwa majeruhi.
.
– Wachezaji walioondolewa katika kikosi kwasababu ya kuwa majeruhi ni Beki David Mwantika, Kipa, Aishi Manula na Mshambuliaji, Ibrahim Ajibu ambao nafasi zao zinazibwa na Mohamed Ally Yusuf (Lipuli),Oscar Godfrey Masai (Azam FC) na Haruna Shamte “Terminator” (Lipuli)..
#TaifaStars
@Sokawaytz_

Nicolas Pepé Anakuwa Mchezaji wa Nne Kuiwakilisha Nchi ya Ivory Coast 🇨🇮 Katika Ligi Kuu Nchini Uingereza

Nicolas Pepé Anakuwa Mchezaji wa Nne Kuiwakilisha Nchi ya Ivory Coast 🇨🇮 Katika Ligi Kuu Nchini Uingereza, @premierleague katika Klabu ya Arsenal, Baada ya..
Emmanuel Eboue 🇨🇮
Kolo Toure 🇨🇮
Gervinho 🇨🇮
🆕 Nicolas Pepé 🇨🇮
:
– Nicolas Pepé Anakuwa Mchezaji ghali zaidi wa muda wote kusajiliwa ndani ya Klabu ya Arsenal Katika Premier League:
🇨🇮 Nicolas Pepe (£72m) 🆕
🇬🇦 Pierre-Emerick Aubameyang (£56.1m)
🇫🇷 Alexandre Lacazette (£52.7m)
🇩🇪 Mesut Ozil (£42.5m)
🇩🇪 Shkodran Mustafi (£35m).
:
– Nicolas Pepé Anakuwa Mchezaji ghali zaidi wa muda wote Katika historia ya Premier league kwa Wachezaji kutoka Bara la Afrika!!.
🇨🇮 Nicolas Pepe (£72m) 🆕
🇩🇿 Riyad Mahrez (£60m)
🇬🇦 Pierre-Emerick Aubameyang (£56.1m)
🇬🇳 Naby Keita (£52.75m)
🇪🇬 Mohamed Salah (£36.9m).
#transfersUpdates #EPLTransfersUpdates #EPLUpdates
@Sokawaytz_

Design a site like this with WordPress.com
Get started