Dele Alli atakosa mwanzo wa msimu wa Ligi Kuu England 2019/20

– Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino amethibitisha Kiungo wa Kikosi hicho, Dele Alli atakosa mwanzo wa msimu wa Ligi Kuu England 2019/20 kutokana na Majeraha ya Musuli, na kuongeza kuwa atakuwa nje “kwa wiki chache”.
.
– Sababu ya Majeraha hayo, Alli hakuwa Katika Kikosi hicho kilicho cheza game ya mwisho ya Pre-Seasons wakipoteza mechi hiyo ya mwisho dhidi ya vijana wa Antonio Conte, Inter Milan.
.
– Ni Kwa Mara ya nne kwake kupata maumivu ambayo amekuwa nayo ndani ya misimu mitatu ya hivii karibuni na shida hiyo ya misuli ya paja pia ilimfanya kukosa Kipindi kirefu Cha Msimu uliopita 2018/19… Pochettino amesema kuwa, Bado ana umri mdogo, hivyo matatizo Kama hayo kwake Ni Jambo la kawaida!.
#EPLUpdates #Tottenham #premierleague

RATIBA YA SOKA HII LEO JUMANNE!.

.

– Champions League – Qualification
20:00 APOEL Nicosia
Qarabag FK
20:00 PAOK Thessaloniki FC
Ajax
21:00 Dinamo Zagreb
Ferencvaros
21:30 Club Brugge
Dynamo Kyiv
21:45 FK Crvena Zvezda
FC Koebenhavn
.
– Europa League – Qualification
18:00 Ararat Armenia
Saburtalo
19:00 Riga FC
HJK
21:15 Sutjeska
Linfield
.
– England – EFL Cup
21:45 Portsmouth
Birmingham City
.
Italy – Coppa Italia
21:30 Reggina
Vicenza
.
– International – Club Friendlies
16:00 Simba SC
Power Dynamos
19:00 VfL Benrath
Fortuna Düsseldorf
21:00 Celta Vigo
Tenerife
.
– South Africa – Premier League
20:30 Bidvest Wits
Baroka FC
.
MATOKEO YA SOKA JANA
– England – Championship.
FT Huddersfield Town 1 – 2 Derby County
#fixtures #updates
@Sokawaytz_

Yanga yatoa shukrani zao baada ya wiki ya mwananchi kukamilika

SALAMU ZA SHUKRANI*

Uongozi wa klabu ya Yanga unatoa shukrani za dhati kwa Wanayanga wote, Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wote kwa namna walivyoipokea wiki ya Mwananchi, na kujitokeza kwa wingi katika ushiriki shughuli mbalimbali za kijamii katika wiki ya Mwananchi zilizofanyika nchini kote Tanzania Bara na Visiwani.

Kama mnavyofahamu, shughuli nyingi zimefanyika kwenye wiki hii ambazo zimehusisha mambo yafuatayo;
1. Ukarabati wa Majengo ya Hospitali,Vituo vya afya,zahanati na majeno ya taasisi za umma.
2. Kutoa misaada kwa makundi maalum yenye uhitaji katika jamii.
3. Kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya wazi, ya umma kote nchini .
4. Kuchangia damu na kuhamasisha umma wa watanzania kushiriki katika zoezi la uchangiaji damu katika Benki ya damu.

Tunaishukuru Serikali katika ngazi zote kwa kuruhusu Wanayanga kufanya mambo waliyokusudia katika wiki hii, vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa waliyoifanya wiki nzima hadi jana siku ya Kilele, Tunavishukuru Vyombo vya Habari nchi nzima kwa kazi nzuri waliyoifanya kuwahabarisha Wananchi juu ya matukio mbalimbali ya Wiki ya Mwananchi.

Tunaishukuru kamati ya Hamasa pamoja na kamati ya `utendaji ya Yanga kwa kazi kubwa ya uratibu wa shughuli hii, na zaidi tunawashukuru sana Wanayanga kwa kujitokeza kwa wingi jana kwenye hitimisho la wiki ya Mwananchi. Shukrani hizi pia ziende pamoja na pongezi za dhati za Uongozi wa Yanga kwa makundi hayo kwa kazi zao ambazo zimeipa heshima na faraja klabu yetu.
Tunafahamu sote kwamba Wiki ya Mwananchi imefikia tamati jana kwa mafanikio makubwa sana, lakini niwakumbushe tena kwamba mbele yetu kuna jukumu linguine la mchezo wa Kimataifa dhidi ya TownShip Rollers ya Botswana siku ya `jumamosi tarehe 10.08.2019 . Hivyo basi Tunawaomba Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga, kwa ari,upendo na mshikamano ule ule wa jana na hamasa ya Wiki nzima iendelee kwenye mchezo huo, tujitokeze kwa wingi sana kuipa nguvu timu yetu siku ya mchezo huo ili kuhakikisha tunapata ushindi.

Uongozi unaamini kwamba hamasa hii haitapoa kuelekea kwenye mchezo huo na hata Ligi itakayoanza baadaye mwezi huu. *Dr. Mshindo Msolla*
*Mwenyekiti-Young* *Africans Sports Club*

Thaban Kamusoko. Aaga yanga rasmi

Asanteni, natumaini tutakutana tena” Aliyekuwa Kiungo wa Klabu ya Yanga SC, Thaban Kamusoko Raia wa Zimbabwe, amewaaga Wanayanga!.
.
– Kamusoko Amejiunga na Mabingwa wa Zambia, Klabu ya ZESCO United ambao wakiwafunga Black Mamba ya Eswatini watakutana na Mshindi Kati ya Yanga SC aliyokuwa akiicheza au Township Rollers ya Botswana Katika mechi za Klabu Bingwa Afrika!.
.
#Repost @kamusokothabani
Napenda kuchukua na fasi hii kushukuru viongozi wa @yangasc,wanachama namashabiki kwakuweza kunipa nafasi yakuonyesha uwezo wangu ndani ya 4 years..it has been great to play for one of the biggest teams in East Africa.kila la kheri kwenye msimu mpya. Asanteni sana wote 🙏 and i hope will meet again..

Ajax. Yasajili mserbia Dusan Tadic

OFFICIAL | Klabu ya AFC Ajax kupitia kwa Kocha wao Mkuu, Erik Ten Hag Amethibitisha kuwa Mshambuliaji wao wa Kimataifa wa Serbia, Dusan Tadic ndiye Nahodha wao Mpya ndani ya Kikosi hicho… Hii imekuja Baada ya Aliyekuwa Nahodha wao, Matthijs De Ligt kujiunga na Juventus ya Italia.. “The Machine” @dt10_official 👊💪.
#afcajax #ajax #updates
@Sokawaytz_

Yanga yasikitishwa na utendaji kazi wa kampuni ya Selcom

Uongozi wa Yanga umesikitishwa na utendaji kazi wa kampuni ya Selcom kutokana na hali halisi iliyojitokeza hapo jana katika zoezi la ukataji wa tiketi.

Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Fredrick Mwakalebela amesema kwamba tiketi za mchezo wao dhidi ya Kariobang Sharks baadhi zimekuwa zikiuzwa mara mbili huku tiketi nyingine zikiwa ni kwa ajili ya mechi ya Simba kesho lkn ziliuzwa kwa ajili ya mechi hiyo.

Amesema kwamba kupitia tiketi hizo wamekamatwa baadhi ya watendaji kutoka Selcom ambao ndio walikuwa wauzaji.

Aidha alisema kwamba uongozi wa Yanga umeamua kuiandikia barua serikali kuwajulisha jambo hilo ambalo anaamini halina tija kwa maendeleo ya mpira wa miguu.

Kuhusu mapato ya mechi amesema kwamba bado hawajapata taarifa rasmi kutoka Selcom ambao ndio wamesimamia mchakato huo.

Chanzo : @daboten

Design a site like this with WordPress.com
Get started