Philippe Coutinho. Kutoka barcelona kwa mkopo

Kuna Kila Dalili kwamba FC Barcelona ipo Kwenye mipango ya kumtoa kwa mkopo Kiungo wao wa Kimataifa wa Brazil, Philippe Coutinho Katika Dirisha hili la uhamisho lililobakisha Siku chache tu kabla ya kufungwa!.
.

– Kwa mujibu wa ripoti, ni Vita ya Vilabu viwili kutoka London, Arsenal na Tottenham wapo Kwenye kinyang’anyiro Cha kumtaka Nyota huyo wa zamani ndani ya Premier league akiwika na Majogoo wa Anfield, @liverpoolfc.
#EPLTransfersUpdates #EPLUpdates
@Sokawaytz_

Kocha mkuu wa gor mahia ajiuzuru

– Rasmi, Hassan Oktay amejiuzulu rasmi kama Kocha mkuu wa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) Klabu ya GOR Mahia.
.

– Mkufunzi huyo wa Kituruki ameomba Klabu hiyo imwachilie katika jukumu lake hilo baada ya kuomba kuondoka… Oktay aliteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa GOR Mahia mnamo Disemba 2018 akichukua Mikoba ya Dylan Kerr, ambaye pia alijiuzulu wadhifa wake baada ya msimu mmoja tu.
#TransferNewsUpdate
@Sokawaytz_

Crystal Palace imeshinda mbio za kumsajili. Gary Cahill…

– Crystal Palace imeshinda mbio za kumsajili Aliyekuwa Beki na nahodha wa zamani wa Chelsea, Gary Cahill… Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 amekuwa Hana timu tangu atemwe na Chelsea wakati mkataba wake ulipomalizika mwishoni mwa mwezi wa Juni.
.
– Cahill hapo awali alikuwa akihusishwa na kuhamia Burnley, lakini kwasababu, James Tarkowski ameamua kubaki viunga hivyo vya Turf Moor, shauku ya klabu ya Lancashire kumsajili Cahill ikatoka wakaamua waachane na mpango huo… Sasa Crystal Palace imemnasa Muingereza huyo!.
.

– Cahill alicheza mechi mbili tu za Ligi Kuu kwa Chelsea msimu uliopita… kwa ujumla alikaa misimu saba na nusu huko Stamford Bridge, akiwa kama mchezaji muhimu ndani Kikosi Cha The Blues, akitwaa mataji mara mbili ya Ligi Kuu, Europa league na Ligi ya Mabingwa Ulaya Mara moja!..
#TransferNewsUpdate #EPLTransfersUpdates
@Sokawaytz_

Burnley na Derby Country..kuwania saini ya Wayne Rooney

✍🏻 Klabu ya Burnley imeungana na Derby Country Katika mbio za kuwania saini ya Nahodha wa zamani wa England, Wayne Rooney mwenye umri wa Miaka 33.
.
✍🏻 Burnley inamtaka Rooney kama Mchezaji Ambaye kwasasa anakipiga Ligi kuu Nchini Marekani Katika Klabu ya DC United huku Derby Country ikimuwinda Rooney kuja kuwa Kocha Mchezaji ndani ya kikosi hicho huko Championship!..
.

✍🏻 Wakati huo huo, yeye mwenyewe Rooney hajaweka Siri juu ya Mipango yake kwamba anataka kuwa Kocha, na Derby inatumia fursa hiyo kumshawishi Legendary huyo wa Manchester United.. Mpaka Sasa hakuna Makubaliano rasmi zaidi ya kuwepo kwa Mazungumzo ya Awali Kuendelea!.
#EPLUpdates #burnley #dcunited #derbycounty
@Sokawaytz_

Design a site like this with WordPress.com
Get started