Ajib ..manura kurejea.kikosini

Fundi wa mpira Ibrahim Ajib na mlinda lango Aishi Manula wanatarajiwa kurejea kikosini wiki hii kuendelea na maandalizi ya mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Daktari wa Simba Yassin Gembe, Ajib na Manula wako kwenye hatua za mwisho za matibabu yao

Lakini ni wazi wataukosa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Jumamosi, August 17 2019

Aidha mshambuliaji Wilker Da Silva yeye hali yake bado na anaendelea na matibabu

Nilikua naikopesha TFF asema.malinzi

Aliyekuwa rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (59), amedai mahakamani kuwa wakati anaingia madarakani shirikisho hilo lilikuwa na hali ngumu kiuchumi iliyosababisha madeni makubwa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kusababisha akaunti zake kufungwa kila wakati na kusema kuwa siku chache kabla ya kukamatwa, aliikopesha TFF Sh. Milioni 15.

Malinzi alitoa madai hayo jana wakati akijitetea dhidi ya mashtaka ya kughushi na kutakatisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Richard Rweyongeza, Malinzi alidai hali hiyo ilikuwa ikimlazimu kuikopesha TFF fedha zake binafsi na alikuwa akifanya hivyo kupitia akaunti waliyoifungua kati yake na shirikisho hilo.

Amedai kiasi hicho cha sh. Milioni 15, zilikuwa ni kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kufuzu fainali za Afrika kati ya Tanzania na Lesotho.Amedai akiwa rais, alihakikisha shughuli mbalimbali za timu zinakwenda hadi kushiriki michuano mbalimbali ya kimataifa ambapo ili kufanikisha hilo, mara nyingine ilikuwa ikimlazimu kutumia fedha zake za mfukoni ili kuweza kuinusuru TFF.

Malinzi alidai kuwa aliikopesha TFF kutokana na hali ngumu ya kifedha iliyokuwa ikiikabili na hivyo kulazimika kutumia fedha zake binafsi, kukopa kwa watu binafsi ama kamati ya utendaji ili kunusuru hali hiyo hasa katika matukio muhimu yanayoikuta TFF na timu ya Taifa (Taifa Stars).

Akiendelea kutoa utetezi wake, alidai, baadhi ya matukio ambayo alilazimika kutoa fedha zake na kuikopesha TFF mojawapo ni ile ya kulikomboa basi la TFF ambalo lilikuwa linashikiliwa na kampuni ya udalali ya Yono kufuatia amri ya mahakama la kuilipa Kampuni ya Pachi Line iliyokuwa ikitoa huduma za tiketi uwanjani.

Aliendelea kudai kuwa, aliilipa sh milioni 20 kampuni ya udalali ya Yono ambapo TFF ilikuwa ikidaiwa na TRA na walitaka kukamata basi hilo ambalo lilitolewa na wafadhili wao, Kampuni ya Bia ya TBL.

Pia alilipia Tsh milioni 40 za tiketi za ndege kw Kampuni ya Ethiopia Airline, za wachezaji wa TΓ ifa Stars waliokuwa wanakwenda nchini Nigeria katika Mashindano ya Afrika yaliyokuwa ya kufuzu kucheza fainali nchini Misri.

Aidha, aliongeza kudai kuwa aliwahi kuikopesha TFF, Dola za Marekani 7,000 wakiwa Harare, Zimbabwe, baada ya wachezaji waTaifa Stars kutolewa mizigo yao nje ya hoteli waliyokuwa wamefikia kwa sababu Shirikisho la Mpira la Zimbabwe lilikuwa likidaiwa na hoteli hiyo, na akaongeza kwamba hata baadhi ya mashahidi waliowahi kutoa ushahidi mahakamani hapa walithibitisha hilo akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa TFF, Daniel Masangi.

Aliwataja mashahidi wa upande wa mashtaka waliodhibitisha jambo hilo mahakamani akiwemo Katibu Mkuu, Wilfred Kidao, Hellen Adam na Sareki Yonasi.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, Karani Flora Rauya na Selestine Mwesigwa.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 15 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya uamuzi wa kupokelewa kwa kielelezo cha nyaraka ya taarifa ya madeni kati ya TFF na Malinzi ama la.

GPL

Klabu ya Marseille..yamtimua beki wake Adil Rami

– Klabu ya Marseille Imethibitisha kumtimua ndani ya timu hiyo Beki wa Kimataifa wa Ufaransa, Adil Rami Mwenye umri wa Miaka 33 kwa utovu wa nidhamu, hii imekuja Baada ya Mchezaji huyo kuacha kwenda mazoezini na kwenda kushiriki katika kipindi cha Televisheni cha Fort Boyard.
.
– Marseille hawakujua ukweli huo mpaka pale show iliporushwa kwenye TV ambapo Mfaransa huyo ameonekana katika show hiyo ambayo walikuwa wakicheza mieleka kwenye matope, πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ Show hiyo ilirekodiwa mwezi Mei mwaka huu siku ambayo alitakiwa kuwepo mazoezini lakini akasingizia kuwa ni yeye majeruhi.
#Updates #marseille #Ligue1Updates
@Sokawaytz

MATOKEO YA SOKA JANA JUMATANO! UEFA

– Super Cup.
AET Liverpool * 2 – 2 Chelsea
.
– Europa League – Qualification.
FT Atromitos 0 – 2 Legia Warszawa
FT Saburtalo 0 – 2 Ararat Armenia
FT Vitoria de Guimaraes 6 – 0 Ventspils
.
– South Africa – Premier League.
FT Chippa United FC 1 – 1 Mamelodi Sundowns FC
FT Polokwane City 0 – 1 Bidvest Wits
FT SuperSport United 3 – 0 Orlando Pirates
.
RATIBA YA HII LEO ALHAMISI!.
Europa League – Qualification.
19:00 HJK
Riga FC
19:30 Dinamo Tbilisi
Feyenoord
19:45 Spartak Moscow
Thun
20:00 AIK
FC Sheriff
20:00 Apollon Limassol
Austria Wien
20:00 BATE Borisov
FK Sarajev
20:00 Bnei Yehuda Tel Aviv
FK Neftchi
20:00 Mlada Boleslav
FC FCSB
20:00 Shakhtyor Soligorsk
Torino
20:00 Suduva
Maccabi Tel Aviv
20:00 Yeni Malatyaspor
Partizan Beograd
20:00 Zorya Luhansk
PFC CSKA-Sofia
20:00 Zrinjski Mostar
Malmoe FF
20:30 Hapoel Beer Sheva
IFK Norrkoeping
20:30 TNS
Ludogorets Razgrad
20:30 Trabzonspor
Sparta Prague
21:00 AEK Athens
CS Universitatea Craiova
21:00 Valletta
FC Astana
21:00 Viktoria Plzen
Royal Antwerp
21:30 AZ Alkmaar
Mariupol
21:30 Aris Thessaloniki
Molde
21:30 Eintracht Frankfurt
FC Vaduz
21:30 Gent
AEK Larnaca
21:30 PSV Eindhoven
FK Haugesund
21:30 Strasbourg
Lokomotiv Plovdiv
21:45 Aberdeen
Rijeka
21:45 SC Braga
Broendby IF
21:45 Rangers
FC Midtjylland
21:45 Wolverhampton Wanderers
Pyunik
22:00 RCD Espanyol
Luzern
.
– Algeria – Ligue 1.
19:00 NA Hussein Dey
JS Kabylie
22:00 JS Saoura
CS Constantine
22:00 NC Magra
ASO Chlef
22:00 USM Alger
ES Setif
22:30 CA Bordj Bou Arreridj
CR Belouizdad
23:00 US Biskra
Paradou AC
#Updates #fixtures
@Sokawaytz

Ligi yamabingwa yaleta panga pangua ratiba ligi kuu..TPL

Mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Simba dhidi ya JKT Tanzania ambao awali ulipangwa kupigwa August 23 kwenye uwanja wa Taifa, sasa utapigwa August 29

Mabadiliko hayo yametokana na Simba kukabiliwa na mchezo wa ligi ya mabingwa, dhidi ya UD Songo

Mchezo huo wa marudiano utapigwa August 25 kwenye uwanja wa Taifa

Tayari TFF imeziarifu Simba na JKT Tanzania kuhusu mabadiliko hayo

Barcelona yapata pigo

OFFICIAL: Barcelona Imethibitisha kuwa mlinda lango wao Namba Mbili wa Kimataifa wa Brazil, Neto anatarajia kufanyiwa Upasuaji Katika mkono wake hivyo atakuwa nje ya Uwanja kwa Kipindi Cha Wiki Sita Mpaka Nane…
:
– Neto Alijiunga na Mabingwa hao wa Hispania Juni 27,2019 kwa Ada ya uhamisho wa €26m akitokea Valencia… Ameumia kabla ya hata kuanza kwa @LaLiga kacheza mechi moja tu dhidi ya Napoli Katika Ziara ya BarΓ§a huko MarekaniπŸ™Œ!.
#fcbarcelona #Updates
@Sokawaytz

Biashara united kuvaana na Singifa united Leo.

.

..Leo siku ya jumatano…kutakua na mchezo wa kirafiki kati ya biashara united kutoka mkoani mara na Singida united kutoka mkoani singida…..ambapo mchezo huo unatarajiwa kupigwa majira ya saa kumi (10) jioni katika uwanja wa karume uliopo mjini msoma mkoani mara

Fika bila kukosa ili uweze kujionea mtanange huo ..ambao ni moja kati ya maandalizi kuelekea ligi kuu soka tanzania bara mwaka 2019/20…..inayotarajiwa kuanza mwezi August

@habarizamichezo

Vigogo waliotupwa nje ..kuwania kucheza champions league

πŸ‘‰ Baadhi ya timu Maarufu Barani Ulaya tayari zimetupwa nje ya Michuano ya Champions League Kwenye harakati zao za kuwania Kufuzu kucheza hatua ya Makundi!.
❌ πŸ‡³πŸ‡± PSV
❌ πŸ‡ΊπŸ‡¦ Dynamo Kyiv
❌ πŸ‡¨πŸ‡­ Basel
❌ πŸ‡ΉπŸ‡· Istanbul Basaksehir
❌ 🏴󠁧󠁒󠁳󠁣󠁴󠁿 Celtic
❌ πŸ‡΅πŸ‡Ή Porto
#UCL #ChampionsLeague
@Sokawaytz

Design a site like this with WordPress.com
Get started