






























Klabu ya Yanga SC kesho itashuka dimbani saa kumi jioni kupambana na klabu ya polisi Tanzania ukiwa ni mchezo wa kirafiki.
Mchezaji Pato Ngonyani atakua akiwakaribisha mabosi wake wa zamani Yanga SC baada ya kuwatumikia kwa miaka kadhaa sasa amejiunga na polisi Tanzania.
@pato_ngonyani @ditram_nchimbi29
@polisitzfc @yangasc

– Frank Lampard juu ya Penati ya Tammy Abraham kuokolewa na mlinda lango wa Liverpool, Adrian Katika mechi ya Fainali ya UEFA Super Cup!.
:
🗣 ‘Nilimwambia asiwe na wasiwasi.. Nimekosa penati hapo awali, mtu yeyote anaweza kukosa, lakini ninachotaka kuona ni kujiamini kwa mchezaji yeye Kama mchanga na kupiga hatua”
:
🗣 “Kukosa ni sehemu kuwa mchezaji katika kiwango cha juu, ambapo ndipo Tammy yupo sasa. Wakati huu unakuja na tunapaswa kumuunga mkono kwa sababu huo ndio mpira wa miguu”.
:
– Klabu ya Chelsea ilipoteza Mechi ya Fainali ya UEFA Super Cup kwa Mikwaju ya Penati 5-4 baada ya Sare ya 2-2 ndani ya Dakika 120.. Mlinda lango Namba Mbili wa Liverpool, Adrian aliokoa mkwaju wa tano uliopigwa na Abraham na Liverpool kupata yao ya tano Iliyopigwa na MO Salah!.
#Updates #supercup #liverpool #chelsea
@Sokawaytz

Naamini tutafanya vizuri tena na katika Champion league kutokana na uzoefu tulioupata katika mashindano haya msimu uliopita.
Kuhusu Mchezo wa marudiano dhidi ya UDSongo Aishi anasema kuwa Nguvu ya mashabiki ni kubwa na hakika itawapa nguvu ya kushinda Mchezo wao ujao dhidi ya UD Songo ambao utachezwa katika Uwanja wa taifa kwani anaamini mashabiki watakuja kwa wingi kuwapa sapoti.
@28_manula @simbasctanzania

Imeripotiwa kuwa Bodi ya Ligi Tanzania bars imevifungia viwanja vitatu, uwanja wa Mwadui (Shinyanga), Manungu Complex (Morogoro) na Mabatini wa mlandizi Mkoani (Pwani) kutumika katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara 2019/20 hadi hapo vitakapofanyiwa marekebisho
:
Ruvu shooting itautumia uwanja wa meja samoyo uliopo mbweni Jijini Dar es laam huko shinyanga klabu ya Mwadui Fc itakua ikitumia uwanja wa Kambarage mjini shinyanga na klabu ya Mtibwa sugar itakua ikiutumia uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.
@mtibwaofficial @ruvushootingfootballltd @mwadui_football_club

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema ana matumaini makubwa kuwa timu yake msimu huu itakuwa bora kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kuliko msimu uliopita
Aussems amesema wamefanya kazi kubwa ya kujiimarisha kimfumo hasa wanapocheza ugenini
“Msimu uliopita hatukuwa na matokeo mazuri kwenye michezo ya ugenini. Ukiondoa mchezo dhidi ya Mbabane Swallows, tulipoteza michezo yote tuliyocheza ugenini,” amesema
“Lakini msimu huu tumefanya maboresho, kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa kwani kwenye mchezo wetu wa kwanza hatukuruhusu bao”
“Bado tunajiimarisha zaidi lakini nadhani msimu huu tutakuwa imara sana katika michezo ya ugenini kwenye ligi ya mabingwa”
Simba imeanza vyema kampeni ya ligi ya mabingwa msimu huu kwa kulazimisha suluhu ya bila kufungana dhidi ya UD Songo katika mchezo uliopigwa Msumbiji
Mabingwa hao wa Tanzania Bara watarudiana na UD Songo uwanja wa Taifa, August 25 2019
Kwa sasa kikosi cha Aussems kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa keshokutwa dimba la Mkapa

– Usajili mpya wa Klabu ya Juventus, Beki wa Kimataifa wa Brazil, Danilo ameweka wazi kuwa alijaribu kuitaka jezi namba Saba (7) ndani Klabu yake hiyo mpya kutoka kwa Cristiano Ronaldo anayeivaa kwasasa, lakini alitambua kuwa mshindi huyo wa mara tano wa Ballon d’Or angegoma kwa vyovyote vile.
:
– Wakati wowote, Klabu yoyote, Cristiano Ronaldo anacheza yeye ndiye bosi wa Jezi Namba Saba, Danilo Nae alijaribu kuchukua jezi hiyo kwa kumuuliza mchezaji mwenzake (Cr7) kwamba anaitaka jezi namba saba.
:
– Wawili hao Ni Marafiki kwani walicheza pamoja huko Real Madrid kwa miaka miwili, na kushinda Ligi ya Mabingwa mara mbili, kabla ya Mbrazil huyo kuhamia Manchester City… Danilo Mwenye umri wa miaka 28 alifafanua kuwa mazungumzo yake na Ronaldo yalimsaidia kufanya uamuzi wa kuhamia Turin..
#Updates #Juventus #SerieAUpdates
@Sokawaytz

Mshambuliaji wa Klabu ya Liverpool na Senegal, Sadio Mané amekuwa Mchezaji wa Kwanza Kutokea Barani Afrika kufunga Goli Katika mechi ya Fainali ya UEFA #SuperCup tangu 2006, Mane alifunga Magoli yake Mawili usiku wa jana Katika mechi ya Fainali dhidi ya Chelsea; Mara ya mwisho Alifunga Mshambuliaji wa Kimataifa wa Mali, Frédéric Oumar Kanouté akiwa na Sevilla Katika Fainali dhidi ya FC Barcelona huko Stade Louis II Katika Jiji la Monaco 🇫🇷!.
.
✍🏻 Kanouté, Ambaye amestaafu Soka hivii Sasa, Ni Mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika Mwaka 2007 na Kuwa Mchezaji wa Kwanza kuzaliwa nje ya Afrika (Ufaransa) lakini Ni Muafrika kuitwaa tuzo hii, Alifunga goli moja Kati ya Matatu ya Sevilla waliokuwa Mabingwa wa Europa league Mwaka uliopita wakiinyuka Barça waliokuwa Mabingwa wa Champions League Mwaka Uliopita!.
.
✍🏻 Hii ilikuwa ni Fainali ya tatu Katika historia kupigwa kwa timu mbili kutoka Nchini Moja… Na hapa ndipo Barça walipo ingia Katika mawindo ya kumnasa Dani Alves aliyewatesa Katika mechi na Kuwa “Man of the Match”.. walifanikiwa 2008!
#uefasupercupfinal #supercup
@Sokawaytz

✍🏻 Luka Jovic anaweza kutolewa kwa mkopo kutoka ndani ya klabu yake ya Real Madrid, Ni miezi miwili tu imepita tangu kusajiliwa na klabu hiyo ya Uhispania kwa £62m akitokea Frankfurt ya Ujerumani… Kwa mujibu wa ripoti katika nchi yake ya Serbia, kupitia Marca, Mshambuliaji huyo anaweza kutolewa kwa mkopo kufuatia Kocha mkuu wa Madrid, Zinedine Zidane ameripotiwa kutoshawishika na Mshambuliaji huyo!.
.
✍🏻 Jovic alikuwa Ni moja ya jina kubwa kusajiliwa na Los Blancos, Hii Ilikuja Baada kufanya vibaya ya msimu wa 2018/19, ambapo tulishuhudia Madrid wakiachana na mameneja wawili kabla ya kurudi kwa Zidane… Wachezaji wengine walio unda Madrid Mpya Ni Kama vile mshambuliaji, Eden Hazard kutoka Chelsea, Mabeki, Eder Militao na Ferland Mendy, kutoka Porto na Lyon na kinda, Rodrygo alisaini, baada ya kukubali Maslahi binafsi mwaka jana na Madrid!.
.
✍🏻 Jovic alisaini mkataba wa miaka sita huko Bernabeu lakini ujumuishaji wake katika timu hiyo unaweza Kuwa hafifu kwani Zidane ni shabiki mkubwa wa Karim Benzema, licha ya ada kubwa kulipwa kwa Mshambuliaji huyo wa zamani wa Frankfurt!.
#TransferNewsUpdate #RealMadrid #LaligaUpdates
@Sokawaytz