Maboresho kanuni ligi kuu tanzania 2019/2020

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi, wameboresha kanuni za ligi ambazo zitatumika kuanzia msimu unaoanza mwishoni mwa wiki

Maboresho muhimu;

1. Wachezaji wa kigeni wanaendelea kubaki 10 na wote wanaweza kutumika kwenye mchezo mmoja. Sharti mchezaji wa kigeni anayesajiliwa awe anacheza timu ya Taifa au Ligi Kuu ya nchi husika. Wanaotoka Ulaya na Amerika angalau wawe wanatoka Ligi daraja la tatu au inayolingana na hiyo

2. Timu za Ligi Kuu zitapungua hadi 18 msimu ujao. Timu nne msimu huu (2019/20) zitashuka daraja moja kwa moja yaani aliyeshika nafasi ya 17/18/19/20 anashuka moja kwa moja kwenda ligi daraja la kwanza huku aliyeshika nafasi ya 15/16 atacheza Play Off na timu za ligi daraja la kwanza.

Msimu wa 2020/21 ligi kuu itashirikisha timu 18 ikiwa timu 14 zilizobaki ligi kuu, timu 2 ambazo zimepanda daraja moja kwa moja kutoka ligi daraja la kwanza na timu 2 washindi wa jumla wa Play Off ya timu zilizoshika nafasi ya 15/16 ligi kuu na washindi wa wa jumla wa Play Off ya ligi daraja la kwanza.

3. Kuanzia msimu ujao makocha wa timu za TPL watapaswa kuwa na leseni A ya CAF au inayolingana na hiyo

4. Kocha akionyeshwa kadi nyekundu atakosa mechi tatu na hataruhusiwa kuingia hata kwenye vyumba vya kubadilishia nguo pia atatozwa faini ya laki tano

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana, Junior Agogo afariki

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana, QPR na Zamalek Junior Agogo amefariki dunia akiwa huko Uingiereza akiwa na umri wa miaka 40.
:
Agogo alikuwa akisumbulia na maradhi ya moyo mara baada ya kushikwa na shinikizo la damu tokea mwaka 2015.
.

Agogo mpaka anafariki alifanikiwa kucheza vilabu 15 lakini hakuwahi kucheza EPL licha ya kucheza vilabu mbalimbali vya England. .

Agogo alicheza kwa mafanikio timu ya taifa ya Ghana mwaka 2006-2009. Alicheza michezo 28 na kufunga magoli 12 huku mwaka 2008 akiisaidia Ghana kumaliza nafasi ya 3 AFCON. .

Aliisaidia Nottingham Forest kufuzu ligi daraja la kwanza baada ya kufunga magoli 13 kabla ya kutimkia Zamalek

Sasa PSG kuitafuta saini na Paulo Dybala kwa nguvu

Klabu ya PSG itatuma maombi ya kumsajili mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala endapo Neymar Jr ataondoka klabuni hapo.
:
Imeelezwa kuwa PSG wamepanga kutumia dau la €73m hadi €80m ili kumpata nyota huyo lakini pia Juventus wao wapo tayari kutoa kiasi cha €100m pamoja na nyongeza ya huyo huyo Dybala ili kupata saini ya Neymar Jr
:
Patamu hapo !!
:
Unafikiri PSG wanaweza wakapiga chini ofa ya Juventus?

Haruna niyonzima. Kuukosa mchezo wa KMC

Nyota wa rwanda haruna hakizimana niyonzima anaekipiga katika klabu ya As kigali ya rwanda ataukosa mchezo wa shirikisho unaotarajiwa kupigwa hapo kesho hii ni baada ya Kocha mkuu wa klabu ya As Kigali kuthibitisha kuwa nahodha wake Haruna Niyonzima ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya KMC kutokana na kukosa leseni itakayomuwezesha kuitumikia klabu hiyo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

:

Haruna ataruhusiwa kuitumikia timu yake kwenye michuano hiyo endapo watafuzu hatua inayofuata

Fernk.Domayo asemaFasil Kenema ya Ethiopia hawachomoki

#KaziTunamalizaChamazi Kazi ya chumvi katika mapishi ni kuongeza ladha kwenye chakula, basi utamu wa pambano la Azam FC dhidi ya Fasil Kenema ya Ethiopia, linaongezewa ladha na Nahodha Msaidizi, Frank Domayo ‘Chumvi’, ambaye amejipanga vilivyo kuwapa raha mashabiki watakajitokeza kwa wingi katika mchezo huo keshokutwa Jumamosi.

Kiungo huyo anayesifika kwa mashuti ya mbali na kukata umeme katikati ya uwanja, ni mmoja wa nyota wa Azam FC wanaoomba sapoti yenu mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani watakapowavaa Wahabeshi hao saa 10.00 jioni.

Shoo yote ya kibabe kwa wababe hao wa Azam Complex, utaweza kuishuhudia kwa viingilio vya Sh. 3,000 kwa majukwaa ya mzunguko, Sh. 10,000 kwa V.I.P A na B na V.I.P C Sh. 5,000.

Tiketi zote zitaanza kuuzwa leo Alhamisi jioni katika vituo vya Magomeni Ice Cream Center, Azam Shop Kariakoo, Mbagala Rangi Tatu na zitakazobakia zitauzwa siku ya mchezo uwanjani.

Azam FC ni ya Tanzania. Tanzania ni ya Watanzania. Twendeni kwa wingi tukawashangilie Watanzania wenzetu.

SHIKALO WA YANGA NA FRANCIS KAHATA WA SIMBA WAITWA TIMU YA TAIFA YA KENYA

Kikosi cha Awali cha Harambe Stars kitakacho ingia kambini kuwavaa Uganda Mwezi ujao kwa ajili ya Mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Magolikipa :

Patrick Matasi (St. George SC, Ethiopia), John Oyemba (Kariobangi Sharks, Kenya), Faruk Shikalo (Young Africans SC, Tanzania)

Walinzi :

Joseph Okumu ( Real Monarchs FC, USA), Mike Kibwage (KCB FC, Kenya), Joash Onyango (Gor Mahia FC, Kenya), Benard Ochieng (Wazito FC, Kenya), Abud Omar (Sepsi OSK Sfantu Gheorghe, Romania), Erick Ouma (Vasalunds IF, Sweden) Nicholas Meja (Bandari, Kenya), Samuel Olwande (Kariobangi Sharks, Kenya)

Viungo :

Victor Wanyama (Tottenham Hotspurs FC, England), Francis Kahata (Simba SC, Tanzania), Boniface Muchiri (Tusker FC, Kenya), Kenneth Muguna (Gor Mahia FC, Kenya), Duke Abuya (Kariobangi Sharks FC, Kenya), Ismael Gonzales (UD Las Palmas FC, Spain), Cliffton Miheso (Gor Mahia FC, Kenya), Johanna Omolo (Cercle Brugge, Belgium), Ayub Timbe (Beijing Renhe FC, China), Cliff Nyakeya (FC Masr, Egypt), Erick Johanna (IF Brommapojkarna, Sweden), Moses Mudavadi (Kakamega Homeboyz FC), Whyvone Isuza (AFC Leopards SC)

Washambuliaji

:

Michael Olunga (Kashiwa Reysol FC, Japan), Jesse Were (Zesco United, Zambia), John Avire (Sofapaka FC, Kenya)

Kocha Francis ametangaza kikosi cha akiba kwa ajili ya wachezaji watakaopata majeruhi.

Magolikipa :

Timothy Odhiambo (Ulinzi Stars, Kenya)

Walinzi

:

Johnstone Omurwa (Wazito FC, Kenya), Brian Otieno (Bandari, Kenya), David Owino (Mathare United, Kenya), Hillary Wandera (Tusker, Kenya)

Viungo

:

Dennis Odhiambo (KCB, Kenya), Lawrence Juma (Gor Mahia, Kenya), Washambuliaji

:

Nicholas Kipkirui (Gor Mahia, Kenya), Enosh Ochieng (Ulinzi Stars, Kenya), Timothy Otieno (Tusker, Kenya)

Prepared

by @officialchristz

Powered by @bikotanzania

Kahata kujumuika harambe stars kuiva Uganda

Kiungo mahiri wa Simba Francis Kahata ni miongoni mwa wachezaji walioitwa kuunda kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars ambacho kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Uganda mwezi ujao

Kocha Mkuu wa Harambee Stars Francis Kimanzi pia amewajumuisha Victor Wanyama anayechezea Tottenham Hotspurs na Michael Olunga anacheza soka la kulipwa huko Japan

Pia yumo mlinda lango wa Yanga Farouk Shikalo

Wakati Kenya ikijipima na Uganda, Taifa Stars itakuwa na kibarua cha kusaka nafasi ya kujumuishwa kwenye makundi ya kusaka tiketi ya kombe la dunia 2022

Stars itaanzia ugenini dhidi ya Burundi Septemba 02 na mchezo wa marudiano kupigwa uwanja wa Taifa Setemba 08

Uganda na Kenya ni miongoni mwa timu ambazo zitaingia moja kwa moja hatua ya makundi

AUSSEMS AENDELEA KUIMARISHA KIKOSI KUIVA UD SONGO

Katika michezo miwili iliyopita wengi wameonyesha mashaka kwa safu ya ulinzi ya Simba hasa kati inayoongozwa na wakongwe Paschal Wawa na Erasto Nyoni

Simba imeonyesha kukamilika pembeni, idara na kiungo na ushambuliaji lakini kumekuwa na udhaifu kwa mabeki wa kati kukosa maelewano

Ni wazi hakuna maelewano mazuri kati ya Wawa na Nyoni ambapo kwa mfano katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc, kulikuwa na makosa mengi sana yaliyopelekea Azam kupata nafasi nyingi za wazi

Kama sio umahiri wa Kakolanya kuwahi kutoka kuondoa hatari, na uzembe wa washambuliaji wa Azam Fc, pengine Azam ingefunga zaidi ya mabao mawili

Wengi wametoa maoni kwa kocha Patrick Aussems kuwajaribu walinzi wengine kwenye nafasi ya Wawa

Licha ya Aussems kupendelea kuanza na walinzi hao, Simba ina walinzi wengine Kennedy Juma, Yusufu Mlipili, Gerson Fraga na Tayrone Da Silva

Tyrone alianza na Wawa mechi ya Simba Day dhidi ya Power Dynamo wakati Fraga amekuwa akiingia ‘sub’ katika mechi zote alizocheza

Hata hivyo Fraga na hata Tyrone wameonyesha uwezo mzuri tu

Wengi wana matumaini kuwa Aussems atafanyia kazi changamoto iliyojitokeza katika safu ya ulinzi mchezo dhidi ya Azam Fc

Jumapili UD Songo hawapaswi kufunga goli kwani bao lao moja litawanufaisha kama ikitokea matokeo yakawa sare

Msimu huu Simba imedhamiria kufika mbali zaidi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, bila shaka changamoto hizi zilizoonekana mapema inapaswa zishughulikiwe ili malengo yatimizwe

Maula.yuko fiti….nani.kukaa goloni

Mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula amepona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua na juzi alianza mazoezi ya kikosi cha kwanza

Manula alipata majeraha akiwa kambini nchini Afrika Kusini, majeraha ambayo yalimfanya akose mechi za Stars michuano ya CHAN dhidhi ya Kenya

Daktari wa Simba Yassin Gembe amesema mlinda lango huo pamoja na kiungo Ibrahim Ajib wako ‘fit’ hivyo ni uamuzi wa benchi la ufundi kuwatumia au kutowatumia mchezo wa Jumapili dhidi ya UD Songo

Kurejea kwa Manula kunafanya ushindani eneo la golikipa uzidi ‘kunoga’ kwani Beno Kakolanya ameonyesha uwezo wa hali ya juu katika michezo aliyoitumikia Simba wakati Manula akiwa mgonjwa

Je Jumapili Simba iendelee na Kakolanya au imrejesha Manula langoni? hilo ni swali ambalo majibu yatatolewa na kocha Patrick Aussems Jumapili siku ya mchezo dhidi ya UD Songo

Design a site like this with WordPress.com
Get started