SABABU YA JKT TANZANIA KUBADILI UWANJA MBELE YA COASTAL UNION HII HAPA

MCHEZO wa leo wa Ligi Kuu Bara kati ya JKT Tanzania dhidi ya Coastal Union uliopaswa uchezwe kwenye Uwanja wa Isahmuyo majira ya saa 10:00 sasa ni rasmi utachezwa Uwanja wa Uhuru.

Ofisa Habari wa JKT Tanzania, Jamila Mutabazi amesema kuwa sababu kubwa ya mchezo huo kuhamishiwa Uwanja wa Uhuru ni maji kujaa kwenye Uwanja wa Isahmuyo.
“Tulipaswa tucheze kwenye Uwanja wa Ishmuyo ila kwa sasa hautachezeka tena kutokana na maji kujaa eneo la kuchezea, tumeamua kuupeleka Uwanja wa Uhuru, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,” amesema.
JKT Tanzania mechezo wake wa mwisho ilichapwa bao 1-0na Polisi Tanzania pia Coastal Union nao walichapwa mabao 2-0 mbele ya Simba.

Visit website

AZAM FC V TANZANIA PRISONS KESHO TAIFA NI MOTO

AZAM FC, kesho Uwanja wa Taifa itakuwa na kazi ya kumenyana na Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

AzaM FC itashuka Uwanjani ikiwa na kumbukumbu za kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mbeya City Uwanja wa Samora Iringa huku Prisons ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 mbele ya KMC.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ushindani ili kuzipata pointi tatu huku Adolf Rishard Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons amesema kuwa ana imani kazi itakuwa ngumu ila watapambana.

Visit website

KAGERE AFIKILIA MAAMUZI MENGINE JUU YA SIMBA


MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa hana habari na tuzo ya mfungaji bora ila anachotazama ni rekodi mpya kwa timu yake kutwaa taji la Ligi Kuu Bara.
Simba imetwaa mataji 20 ya ligi ikiachwa kwa jumla ya mataji 7 na wapinzani wao Yanga wenye mataji 27, endapo watafanikiwa kulitwaa msimu huu watabakiza deni la mataji sita kufikia rekodi ya watani zao.
Msimu wake wa kwanza Bongo 2018/19, Kagere alifunga mabao 23 katika ligi na timu yake ilitwaa kombe kwa mara ya pili mfululizo ikimaliza na pointi 93, huku ikifunga mabao 77.
Kagere alisema kuwa anashukuru Mungu kwa kumpa nafasi ya kufanya kile anachokipenda akiwa uwanjani jambo ambalo kwake ni furaha.
“Nafasi yangu na kazi yangu inaniruhusu kufunga na kutengeneza mabao, ninamshukuru Mungu kwa hili, mashabiki pia nawashukuru kwa kuwa wananipa sapoti ila nitazidi kupambana kufikia malengo kwani kazi bado inaendelea,” alisema Kagere

Baba mzazi wa samatta aibuka na ujumbe mzito kwa mwanae


MZAZI wa mshambuliaji wa Aston Villa ya nchini Uingereza, Mbwana Samatta, Mzee Ally Samatta, amemtaka kijana wake huyo abadili mwenendo katika klabu yake hiyo mpya ili kuhakikisha anakuwa bora zaidi ya alivyokuwa KRC Genk ya Ubelgiji alikotokea.
Samatta amesajiliwa katika Klabu ya Aston Villa hivi karibuni, akitokea Genk kwa dau la pauni milioni 8.5 huku akijiwekea rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kujiunga na timu inayoshiriki Ligi Kuu ya England.
Aidha nahodha huyo wa Taifa Stars tayari ameshaichezea timu yake hiyo mechi mbili, ikiwa ni dhidi ya Leicester katika nusu fainali ya Carabao Cup ndani ya dakika 65 huku akishindwa kufumania nyavu licha ya kukosa bao moja la wazi.
Pia, juzi Jumamosi, Samatta alifumga bao lake la kwanza tangu ajiunge na timu hiyo, pia likiwa ni bao pekee kwa Aston Villa ambao hata hivyo walishindwa kutamba ugenini mbele ya Bournemouth ambao waliibuka na ushindi wa bao 2-1.
Mzee Samatta alifunguka kuwa, kama mzazi amejisikia vyema kuona mtoto wake huyo anakipiga katika ligi kubwa duniani lakini amemtaka aongeze juhudi zaidi ya alivyokuwa mwanzo.
“Nimefurahi kuona mwanangu anakuwa Mtanzania wa kwanza kuchezea ligi kubwa duniani, kwani mzazi yeyote amekuwa akipenda kuona mwanawe anafikia mafanikio.
“Kitu ambacho nimemtaka akifanye kwa sasa ni kuhakikisha anaongeza juhudi mara mbili zaidi ya ile aliyokuwa akiifanya Genk kwa kuwa ligi hiyo ni kubwa na ina ushindani zaidi, hivyo ajipange kuhakikisha anakuwa katika kiwango bora,” alisema mzee Samatta.

Ungozi wa simba sc yaweka wazi juu yawachezaji wao ambao hawacheza mwez January

Uongozi wa Simba Sc umedai kuwa wachezaji wake watatu ambao hawajacheza mechi yoyote kwa mwezi January 2020, Mzamiru Yasin, Miraji Athumani na Deo Kanda bado ni majeruhi na siyo vinginevyo.

Uongozi umefunguka maneno hayo baada ya taarifa zilizokuwa zikisambaa mitandaoni kuwa mchezaji kama mzamiru alibolonga siku ya mechi ya watani wa jadi. #fullsokatzupdates

Ijue kampuni yakukuza vipaji vya soka afrika

Alex Morfaw ambaye ni mkuu wa kampuni ya uwakala wa wanamichezo vijana kutokea Afrika inayojulikana kwa jina la Rainbow Sports iliyojikita katika kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana wa Afrika.

Alex Morfaw amejikita katika program za kutoa elimu za soka kwa vijana, mara kadhaa amekuwa akiihesabu Tanzania kwa bara la Afrika kama nyumbani kwake pia (second home) kutokana na kuwa muwakilishi wa wachezaji wengi vijana watanzania barani Ulaya kama wakala wao.

Inawezekana wengi hawafahamu lakini Alex Morfaw amefanikiwa pia kufanya kazi bega kwa bega na wakala anaetambulika na FIFA Kambi Zuberi kutoka @cambiassosports na ndio wakala nyuma ya vipaji vya wachezaji wakitanzania kama Ally Ng’anzi, Abdallah Shaibu, Theonasy Tepsi Evans, Onditi Samweli Jackson, Hamoud Nassor, Caminero Kapilima, Said Hamis na wengine wengi.

@alexmorfow @alexmorfow
@rainbow.sports @cambiassosports
#AlexmorfowinTz

Design a site like this with WordPress.com
Get started