NCHIMBI ABADILI GIA YANGA

STRAIKA mpya wa Yanga, Ditram Nchimbi, amekuja na wazo jipya katika kuhakikisha mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara anatoka ndani ya kikosi chao, hivyo yeye amejipa rasmi kazi ya kuwatengenezea wenzake mabao ili watwae Kiatu cha Dhahabu.
Katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Nchimbi alitoa pasi ya bao lililofungwa na mshambuliaji mwenzake, David Molinga, ambaye amefikisha idadi ya mabao sita mpaka sasa.
Nchimbi alisema nafasi hiyo ni muhimu kwake lakini kwa sasa yupo kwa ajili ya timu zaidi hivyo anatamani kuona anakuwa na mchango mkubwa katika kumtoa mfungaji ndani ya kikosi chake.
“Si rahisi kusema nafukuzia ufungaji bora, lakini ukiangalia wapo ambao wana mabao mengi na wenye nafasi hiyo zaidi yangu, ukweli mimi nitafurahi nikiona anakuwa sehemu ya mafanikio ya mchezaji wa timu yangu akipata nafasi hiyo,” alisema Nchimbi.
Nchimbi aliyetua Yanga akitokea Polisi Tanzania ameongeza kuwa amekuwa na wakati mzuri ndani ya timu kutokana na ushirikiano uliopo kati yake na wachezaji wenzake, sambamba na benchi la ufundi hali inayozidi kumfanya ajiamini zaidi.
Kwasasa nafasi hiyo hiyo bado inafukuziwa na straika wa Simba, Meddie Kagere, mwenye mabao 12 akifatiwa na Paul Nonga pamoja na Daruwesh Saliboko wote kutoka Lipuli kila mmoja akiwa na mabao nane.

Visit website

Wenger kurejea katika ulimwengu wa soka

Meneja wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger anaweza kurejea katika soka la ushindani , huku Rennes akiripotiwa kumlenga kuchukua nafasi ya Olivier Letang kama mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo .
………Rennes alitangaza mnamo Ijumaa kwamba Letang ataihama klabu hiyo ,huku ripoti zikisema kwamba Wenger anaongoza kwenye orodha hiyo ya kuwania nafasi ya kuwa mkurugenzi wa michezo ……
…….Meneja huyo wa zamani wa Gunners hivi karibuni alichaguliwa kuwa mkurugenzi mpya wa ufundi wa FIFA, lakini alisema kwamba kama akipata nafasi ya kurudi kwenye soka angezingatia zaidi

MANCHESTER UNITED KUUZA CHRIS SMALLING

#Updates •
_
Kwa mujibu wa Team Talk, imeripotiwa kuwa MANCHESTER United wanataka “si chini ya” pauni milioni 15 ili wakubali kumuuza beki wao, Chris Smalling (30), ambaye yupo Roma kwa mkopo.
_
United imeweka ngumu kwa beki huyo na kusisitiza kwamba haitakubali kumpiga beki wake, Chris Smalling kwenda AS Roma ya Italia kama tu haitakuwa imewekewa mezani mkwanja unaoanzia Pauni 15 milioni.
_
Smalling 30, ambaye alikosa namba ya kudumu kwenye kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer baada ya kuwasili kwa beki wa kati, Harry Maguire Old Trafford. Jambo lilimfanya Smalling aondoke kwenda kukipiga kwa mkopo huko AS Roma, mahali ambako ameonyesha kiwango kizuri na kuwafanya Wataliano hao kufikiria kumbeba jumla.
_
Kwenye kikosi hicho cha Roma, Smalling amefunga mabao mawili na kuasisti mara moja katika mechi 22 alizocheza na kutokana na mpango wa timu hiyo kutaka kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, hivyo inamtaka beki huyo aendelee kubaki kwenye kikosi chao. Lakini shida inakuja sehemu moja tu, Man United haipo tayari kushusha bei kutoka kiwango inachomuuza cha Pauni 15 milioni.
_
Kwa Roma pesa hiyo inaonekana kuwa kubwa na jambo hilo linahatarisha mpango wa Smalling kutua jumlajumla Italia. Staa huyo atafikisha umri wa miaka 31 Desemba, ukijumlisha pesa anayouzwa pamoja na mshahara jambo hilo linaifanya AS Roma kujiona ina mlima mrefu kwenye kunasa saini ya Mwingereza huyo.

#bakinasisi__ #NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

Vita Ya Vinara Leo _Bundesliga…ujerumani leo

_
_
✍️ Leo katika dimba la Alianz Arena kunako majira ya saa 2 Usiku kutakuwa na kipute cha maana katika muendelezo wa ligi kuu Ujerumani.
_
✍️ Ni pale vinara wa ligi hiyo Bayern Munich (42 pts) watakapo wakaribisha washika nafasi ya pili RB Leipzig (41pts)
_
✍️ Bayern ni kama gari limeshika kasi unaambiwa katika mechi 4 za mwisho za mwaka 2020 Bayern imetembeza vichapo vizito huku ikifanikiwa kufunga magoli 16 ndani ya mechi Hizo 4 tu. RB Leipzig wao katika mechi hizo nne za mwisho wameshinda 1 sare 1 na kipigo mechi 2 wakifunga magoli 9 tu (MASHINDANO YOTE).
_
✍️ Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski ndio hatar zaidi ameweka kambani goli 22 hadi hivi Sasa, huku yule wa Leipzig Timo Werner akiwe ameingia kambani mara 20 tu.
_
✍️ Mechi tatu za mwisho walizokutana miamba hii Bayern kashinda 1, sare 2 na Leipzig hajashinda mchezo wowote. Hivyo katika mechi hizo tatu za mwisho Bayern Munich ndio Mbabe wa Leipzig.
_
✍️ Lewandowski na Timo Werner wameingia Kwenye Rekodi ya kufunga magoli zaidi ya 20+ tangu Franc Brungs na Johannes Lohr walipofanya hivyo msimu wa 1967/68 katika ligi hiyo ya Ujerumani hii ikiwa ni baada ya mechi 20 tu.
________’
✍️ Utabiri wa Vikosi vya leo Bayern: Neuer (c), Pavard, Boateng, Alaba, Davies , Kimmich, Thiago, Müller, Goretzka, Gnabry, Lewandowski
_
Hawachezi leo (Majeruhi) Martinez, Perisic, Süle.
_
Huenda wakacheza au La (50/50) Coman
_
Coach : Hansi Flick
______
______
✍️ Upande wa RB Leipzig kikosi Gulacsi, Mukiele, Klostermann, Upamecano, Halstenberg, Laimer, Adams, Sabitzer (c), Nkunku, Werner, Schick
_
Hawachezi (Out) Kampl , Konate, Orban
_
Coach: Julian Nagelsmann
_
#bakinasisi__ #NjooKwetu #TukoNawePaleUlipo

Wenye Hat-trick Zao Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu Huu _

#VplUpdates • Wenye Hat-trick Zao Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu Huu
_
_
✍️ Kelvin Sabato – Kiduku (Kagera Sugar) akitokea ligi daraja la kwanza akisajiliwa msimu huu na Wanankurukumbi Kagera Sugar, alifunga Hat-trick yake ya kwanza Vs Singida UTD, Singida Ikilala kwa goli 3-0 Kaitaba.
_
✍️ Obray Chirwa (Azam FC) Vs Alliance FC, Azam wakiitungua Alliance goli 5-0 Katika dimba la Nyamagana.
_
✍️ Darueshi Saliboko (Lipuli) Vs Singida UTD. Lipuli ikiitungua goli 5-1 Singida United katika Uwanja wa Samora mjini Iringa.
_
✍️ Ditram Nchimbi (Polisi Tanzania) kwa sasa yupo kwa wananchi Yanga, Nchimbi ndiye aliyekuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat trick wakati timu yake ikitoshana nguvu ya mabao 3-3 dhidi ya Yanga katika Uwanja wa Uhuru.
_
#bakinasisi__
#NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

Klabu ya Toronto yasajili mArgentina Pablo Piatti kutoka RCD Espanyol

Klabu ya Toronto FC ligi kuu ya Marekani imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Pablo Piatti kutoka RCD Espanyol kama mchezaji huru

Piatti mwenye umri wa miaka 30 kwa sasa pia aliwahi kuvitumikia vilabu mbali mbali kama Valencia, Almeria, Estudiantes pia aliwahi kuitumikia timu ya taifa ya Argentina na alianza rasmi mwaka 2016

Powered by @sports_lady_tz

Design a site like this with WordPress.com
Get started